karibuni Kivuko.com wana JF wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

karibuni Kivuko.com wana JF wote

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kivuko, Nov 6, 2009.

 1. Kivuko

  Kivuko Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Karibuni Kivuko.com

  Uongozi wa kivuko.com unapenda kuchukua fursa hii nzito ya JF kuwakaribisha watanzania kwenye mtandao wa kivuko.com.

  Tunajitambulisha kwa kujibu baadhi ya maswali yalioulizwa na baadhi ya wana JF kupitia PM au kwenye thread nyinginezo.

  Kivuko.com ni "duka" au "soko"?

  Kivuko.com ni zaidi ya duka na si kama soko ulilolizoea.
  Hatuuzi bidhaa zetu kwenye "traditional brick and mortal shops".Duka letu lipo www.kivuko.com.
  Ofisi zetu haziifadhi bidhaa za wateja,zinatumika kama kiunganisho cha "end suppliers" na mtumiaji.Kwa hiyo ofisi yetu haifanani na maduka tuliyoyazoea,ingawa tunauza bidhaa.
  kwa anuani ya ofisi zetu tazama hapa.

  Pindi mtu anapoweka oda yake kivuko.Sisi hupitia mlolongo maalum wa kuitoa bidhaa hiyo kutoka kwa watengenezaji/wasambazaji (distributors/suppliers) hadi kwa mtumiaji.
  Kwa lugha rahisi kivuko.com inafanya kazi ya kuunganisha watumiaji na vyanzo bora vya bidhaa.


  Je kivuko ni "soko?"

  Bidhaa zinazouzwa kivuko ziko chini ya usimamizi wa kampuni ya kivuko,ambayo inachukua "responsibility" ya bidhaa zote tunazoziuza.

  Ingawa kuna Baadhi ya bidhaa zinapatikana kupitia ma-vendor wetu.kwa sasa idadi yao ni ndogo na asilimia kubwa ya wasambazaji wetu wako nje ya Tanzania.

  Ingawa kuna uwezekano wa kuwa na mavendor sio kila mtu anaweza kuwa vendor/supplier wa kivuko.Nia yetu ni kufupisha "supply chain" ya bidhaa ili kupunguza gharama kwa mtumiaji.Tunazingatia sana authenticity,kiwango,ubora na uhalisi wa bidhaa kabla ya kukubali mtu/kampuni kuwa vendor wetu.(lakini tunapenda kuwakaribisha wote wenye nia na wanaofikia vigezo kuwa ma-vendor wa kivuko)

  kwa hiyo ingawa kivuko ina tabia za duka na soko kihalisia haifananani na duka wala soko.

  Kivuko kwa lugha ya kigeni ni B2C au Business 2 consumers.

  Tunamuunganisha mteja na chanzo cha bidhaa halisi,bila kutumia "middle men".

  sasa kama hatuweki bidhaa dukani zinamfikiaje mtumiaji?wa zanzibar kwa mfano?

  Wakati wa kuweka oda yako,utahitajika kujaza anuani yako na namba ya simu.Taarifa hizi zinatusaidia kufikisha Bidhaa kule inakotakiwa kwenda.

  Bidhaa nyingi zina "option" ya "free shipping",kutoka kwa Msambazaji/mtengenezaji hadi kwako mtumiaji,na nyingine zinahitaji kulipia gharama kidogo za usafirishaji.
  kwa mfano laptop itahitaji $10 kwa "standard shipping".

  Kivuko ni Salama?

  Kwa tafisri ya kimtandao,kivuko ni moja kati ya mitandao salama zaidi hapa nchini kwetu kwani tumejitahidi kutumia "industry standard" security measures ili kuwezesha watu na taarifa zao binafsi kuendelea kuwa salama katika kipindi chote wanachokuwa kivuko.com.

  Moja ya vitu tunavyotumia ni 256-bit secure encryption SSL kulinda taarifa zako ukiwa kivuko.com.

  njia za malipo?

  Tunatumia payment gateways za "paypal" na "2checkout".hii inamaanisha kwa wale wanaotumia Credit Cards.Taarifa zao zinalindwa na na makampuni bingwa ya E-commerce duniani".

  Na kwa wale wasio na Credit card, hamna shaka tunapokea malipo kupitia M-PESA,Z-PESA,Paypal,Kulipia ukipokea (Cash on Delivery),gift certificates, na kupitia Benki.

  Vipi kuhusu ubora wa Bidhaa?

  Bidhaa zilizopo Kivuko.com ni za "genuine" na zenye "warranty za muda mrefu.na kama ukipokea bidhaa yenye matatizo basi unaweza kubadilisha mpya ndani ya siku 7.

  kuna tofauti kati ya kivuko na mitandao mingine ya E-commerce?
  Tofauti zipo nyingi,kwani kivuko.com tunaamini katika uboreshaji wa huduma kama njia bora ya kuhudumia wateja wetu.Tunatoa pia huduma za "after sales Consultancy" na online live chat na mmoja kati ya wahudumu wetu.

  zaidi ya hapo hauhitaji kuwa mwanachama wa kivuko.com ili kuweza kufanya manunuzi ya bidhaa zako, ingawa wanachama wa kivuko.com watajipatia faida za ziada zinazokuja na uanachama wao.moja kati ya faida hizo ni kuweza kukusanya point kwa kila bidhaa wanayonunua kivuko.com,kujipatia mapunguzo na promosheni nyingine nyingi zinazoelekezwa kwa wanachama.

  Kwa wana JF napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribishaKivuko.com,Tanzania Online Gateway.

  Endelea kutazama ukurasa huu kwani watumiaji wa JF watapokea punguzo maalum kwa kuelewa umuhimu wao katika ukuaji wa teknohama.

  wasalam,

  cheers!

  Kivuko.com
   
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  dah, safi sana mkuu!.
  ila bidhaa mngetuwekea kwa pesa zetu za madafu bana, mambo ya US$ noma. nimeona kwamba zingine ziko kwa Tsh zingene kwa US$
   
 3. Kivuko

  Kivuko Member

  #3
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu George mbona Bidhaa zipo kwenye Madafu Pia?!Tazama Kushoto kwenye Homepage utaona Currency Converter,bonyeza Bendera ya Tanzania,Bei zote zitabadilika kuwa kwenye fedha za Kitanzania.

  kwa sasa tumeweka USD ili kuwezesha wale wanaotumia Credit Cards na Paypal kufanya hivyo bila usumbufu,

  Tunashauri kwa watanzania wote hasa wale waliopo ndani ya jamhuri watumie Tshs.ni option bora zaidi kwao.na kwa wale wanaonunua Gift certificates kwa wapendwa wao wa Tanzania si vibaya wakitumia $USD au Euro
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  yah yah mkuu nilikua siajiona hiyo, sasa niko clear!. kitu safi sana ujue online unapunguza mambo mengi.
  keep it growing mkuu
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  hahahahahahaaaaaaaaaaaaa
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  Safi sana mkuu - nimepita huko, imekaa vizuri
   
Loading...