Karibuni Dar es Salaam wageni mnaokuja kutafuta maisha na kufanya biashara

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,931
22,901
Dar ni jiji ninalolifananisha na Jikoni kwa Tanzania hii, nadhani wote tunajua sifa ya jiko ni mahali panapoandaliwa na kupikwa vyakula vyote tunavyovipenda na tusivyovipenda.

Dar ni mkoa ambao naupa heshima ya kupafananisha na jiko kwasababu ni mkoa ambao ni chanzo cha kila kitu.

Ukitaka ma Pro watenda Dhambi utawapata Dar,

Ukitaka ma Pro wamwabudu Mungu utawapata Dar,

Ukitaka kila unachokijua wewe duniani taarifa zake ukiwa dar huwezi kosa.

Sasa basi kwa sifa hizo leo napenda kuwakaribisha vijana hasa wale wanaotamani kuanza maisha na hawana hata senti mfukoni.

Leo nitaongelea na kuwakaribisha zaidi wale wageni wanaotaka kuja kutafuta maisha dar/kufanya biashara dar ndio Lengo hasa la thread hiii.

Huwa ninapooongea na vijana wenzangu nawambia kwamba kama kuna kijana yeyote yupo dar ametafuta maisha,ametafuta pesa akaikosa Basi nimhakikishie ana asilimia chache sana za kutoboa kama akienda ktika mikoa mingine tofauti na dar.

KWANINI DAR?
Dar ni sehemu ambayo watu sio washamba wala hawashangai shangai

Hii ni faida sana kwako wewe kijana unaetaka kuanza maisha na una aibu, watu wengi hufeli katika maisha kwasababu ya aibu kuogopa watu kuona haya watu watamchukuliaje/watamuonaje,nk nk

Mikoani ukiokota makopo unaonekana chizi,ukiokota Chuma unaonekana kapurwa lakini DAR ni tofauti..

Wakazi wa dar ukipta ukiokota makopo wakikuona watajua wewe ni mtafutaji,wengine watakuita kukupa hata chupa zao za maji ambazo zimeisha, Ukiokota chuma hawatokuita kapurwa Watakuona ni kijana unaejitaftia zako riziki,nk nk

Kwanini wewe kijana ulie huko mkoani usije dar kuanza maisha? Unaogopa nini? Unahofia nini?

HUNA MTAJI?

Sawa kabisa, hata mimi wakati nakuja dar sikua na mtaji japo sikuja kiutafutaji nilikuja kimasomo nikajikuta nipo dar.

baada ya kumaliza masomo yangu nilijikuta mkononi nina Laptop 1,Sub woofer 1 na simu yangu.

sina hata senti 5 ila nina hivyo vitu,nilichofanya wala si kuviuza maana hata kama ningeviuza hela yake najua ningeikula pyuuuu nikabaki mweupe.

Nilichofanya ni kutafuta mtu niliewahi kumuamini (najua hata wewe unaesoma hii unae huyo mtu wa hivyo) nikaenda kumwambia naomba kaa na subwoofer yangu na hii laptop yangu.

Mkononi nikawa nimebaki na mzgo m1 ambao ni simu. Nikajiuliza maswali kadhaa kuhusu ile simu yangu Je. Hii simu naitumia kumtafuta nani? je Sasa hivi huyo ninaemuwaza kwamba ni wa muhimu Yuko wapi?

Nilijiuliza maswali kadhaa ila mwisho nilitoa laini yangu Nikaikata vipande kisha nikaanza tafuta mteja wa ile simu yangu.

Nakumbuka nili iuza kwa bei ndogo sana, baada ya kuiuza nikawa Freeman sina chochote mkononi zaidi ya mimi na miguu yangu.

Kazi ya kuanza tafuta kazi ikaanza,Kama unavyojua nawambia nyie wageni DAR watu hawashangai shangai Dar kila mtu na mishe zake.. Ukitaka attention ya watu wa Dar wasikie tu neno MWIZIIIIIIIIIIIIIII ndio utaona watu wa dar walivyo na ushirikiano wasikiapo hilo neno.

ila kama hawajasikia hilo neno kamwe huwezi chukua attention ya wakazi wa dar kizembe zembe Hiyo MAANA YAKE NINI?

Dar hutakiwi kuwa MWIZI au MDOKOZI kama kweli unataka kuja Kuishi kwa amani DAR.

Basi baada ya kujua wakazi wa dar hawana tofauti na wa New York nikaingia mtaani Dear Mgeni unaesoma hii thread Hamna kazi unaijua sijaifanya, ya kudharaulika ambayo sidhani kama wewe mgrni utaweza ifanya.

Lakini nilifanya kazi zote hizo nikiwa na malengo ya siku 1 niwe na changu niajiri watu,niliamini Baada ya kumaliza masomo ya Chuo kuna Chuo kingine kinaitwa DUNIA UNIVERSITY.

Hiki chuo elimu yake ni bure ila itacost UTU wako,itacost HESHIMA yako,itacost kila unachokithamini sasa.

Ukija DAR lazima iku cost kama ndio umeamua na kudhamiria kuja tafuta maisha.

Kwahiyo nilikubaliana na nafsi yangu lazima nipitie yote hayo ili nitakapopta niwe na stori ya kusimulia.

Mgeni unaekuja DAR jiandae kisaikolojia kuliko kimwili, kuna torturing kwa wingi sana huu mkoa kuliko ufikiriavyo lakini zisikukatishe tamaa maana zote zakupasa uziptie ili uje kuwa mtu ktk watu siku 1.

Ukija Dar jiepushe na makundi na elewa hili ni jiji lisilo na huruma, kama ulifikiri utaomba mtu sh 500 akupe SI KWA DAR kama ulifkiri utaomba chakula chabure si kwa dar so jiandae ktk hilo ukija fahamu unaenda sehemu utakayo tritiwa kama Mtu usieaminika wala kuonewa huruma.

Ukija dar Usichague kazi, kazi zipo nyingi sana zifanye hizo na hakikisha una save pesa zako usikae bila kazi dar kazi zipo everywhere ni wewe tu kuzifata na kuzifanya.

DAR yakupasa uwe na ujasiri! ondoa mashaka na uoga lakini usiache kusema ukweli wa maisha yako endapo utaulizwa na yeyote kuhusu ulipotokea imekuaje hadi ukawa hapo ulipo usiogope ongea kwa uhuru na usionyeshe kuhitaji msaada wake Chukulia hicho unachomuambia n kama unampgia tu stori.

ukionyesha tu huruma za kutaka akusaidie "ndio umekosa msaada" so stay strong ongea mapito yako kwa ujasiri usitilie tilie huruma.

Nimeshakwambia Wakazi wa DAR hawana huruma maana Huruma zao zimeshawaponza sana sana sana. Kwahiyo Usitegemee kwamba utampa mkazi wa dar stori ya dada ako aliebakwa au wewe ulivyobakwa akakuonea huruma.

Zaidi Zaidi ndio utazidi jianika na kumfanya akuweke ktk kundi la "handle with a great care" mkazi wa dar ukimletea tu stori za huruma huruma ujue kama alikua anataka kukusaidia basi ndio ataacha so STAY STRONG AS CROCODILE.

Naamini Dar ni sehemu ya Utafutaji na wala si sehemu ya kuishi kwahiyo Njoo DAR na mission yako 1 ambayo ni "kutafuta" ukishazipata your free to go dear ukazipge pesa mkoani.

Nasemaga mimi dar ni sehemu yakutafutia mtaji ukishapata mtaji kama unajiona huelewi elewi kimbia mkoani huko anzisha biashara kwa mtaji ulioupatia DAR.

Japo kwa mimi sina mpango wa kuhama Dar hata kwa bastola ila pia sina mpango wakutulia tu dar kibiashara ni lazima nipanuke kufika mikoa yote hii nchi KWANINI unajua?

Mtaji wangu ni JIJI LA DAR uwepo wa hili jiji ni pesa, siogopi lolote ninapokua dar Hata nianguke sasa nianze SIFURI sitochukua muda mrefu tena kusimama.

KWANINI?

DAR ndipo mahali pesa za Nchi hiii zinejificha, watu huzamia meli kwenda Ulaya nashangaa sana kuona kuna mtu yupo bush hana channel anashndwa zamia LORI aje dar.

Tokeni hapo ulipo ukiwa kama kijana una nguvu kimbia haraka DAR jichanganye chapa kazi kama punda ndani ya mwaka mmoja wenye siku 365 nakuhakikishia utakua na mtaji wa kuanzisha biashara yako Nzuri.

Kubali kuteseka mwaka 1 tu ukiwa dar then the rest itabaki story.

Dar inakuhitaji wewe,njooo na akili yako TU/adabu/uaminifu/nk kisha Pesa utazikuta huku huku.

Asiekubali kuanzia chini kamwe asitegemee kufika Juuu, Ukija dar kubali anzia CHINI tena chini chini kweli kweli.

Utaonewa/dharauliwa lakini usijali Akili ipo kichwani mwako.
 
Kama una mtaji mdogo karibu Pia Dar cha kwanza kabla ya chochote Panga room unapokua na makazi ni rahisi kwako kufanikiwa kuliko yule anaekuja kwa kutegemea kuanza kama kina sie.

Dar room zinaanzia 15,000 ni bei fair sana kwa mtafutaji / Mpambanaji.

Sikushauri upange room yenye umeme unapoanza anzia na room ya giza na usinunue chochote kwenye hiyo room.

zaidi ya hilo godoro ulilolalia/Net na Mswaki na ndoo za kuogea na kufulia...

Komaaa hapo hapo kwenye room yako ukiwa na vitu hvyo hvyo Kumbuka kilichokuleta dar ni Kutafuta PESA kwanza kisha mengine yatafata baadae.

Usichanganywe na vitu vya nnje Funga macho make pesa yako kila senti utakayopata Tunza ndani ya siku 365 utakua na mtaji wakua zisha moja ya biashara ambayo ndugu zako wakija kuiona lazima wakuulze ulitoa wapi mtaji wa hiyo biashara.

Akiba tu ndio itakayokuokoa. Epuka MARAFIKI wakwepe kama ukoma Rafiki yako awe Kazi yako TU wengine urafiki wenu uwe wa salamu TU.

kumbuka dar huna ndugu watu wa dar hasa vijana wengi sio watu wazuri hasa wa huko mitaani kwahyo unaweza jilinda ukawa hufanyi kosa lolote lkn rafiki ako akakuponza.

Nilishawahi kupata rafiki enzi hizo nikamuona mtu ila alivyonisababisha kwenda lock up sijui mpaka na leo ila nilijifunza kwamba DAR si sehemu salama ya ku make friends otherwise hakikisha huyo mtu unaetaka kuwa na ukaribu nae u amjua in and out.

Utanishukuru baadae kama utafata huu ushauri.
 
Kuna jamaa alikua anapambania tenda ya kutengeneza vipepeperushi vya kampuni moja ya simu akiwa huko mkoa fulani kanda ya ziwa,kila akijaribu anadunda,mfanyakazi mmoja wa hiyo kampuni akamwambia amia huku Dar alafu aanze michakato akiwa Dar,jamaa akafata ushauri wa huyo mfanyakazi,fasta tu akapata tenda.sahivi anakula tenda pia za kampuni nyingine.Dar kwa Bongo ndo kilakitu.
 
Kitendo cha kusema tu upo dar Mtu anajua una experience na unachokifanya hata kama ndio kwanza umeanza kifanya leo ila UTAAMINIKA.
 
Kama una mtaji mdogo karibu Pia Dar cha kwanza kabla ya chochote Panga room unapokua na makazi ni rahisi kwako kufanikiwa kuliko yule anaekuja kwa kutegemea kuanza kama kina sie.

Dar room zinaanzia 15,000 ni bei fair sana kwa mtafutaji / Mpambanaji.

Sikushauri upange room yenye umeme unapoanza anzia na room ya giza na usinunue chochote kwenye hiyo room.

zaidi ya hilo godoro ulilolalia/Net na Mswaki na ndoo za kuogea na kufulia...

Komaaa hapo hapo kwenye room yako ukiwa na vitu hvyo hvyo Kumbuka kilichokuleta dar ni Kutafuta PESA kwanza kisha mengine yatafata baadae.

Usichanganywe na vitu vya nnje Funga macho make pesa yako kila senti utakayopata Tunza ndani ya siku 365 utakua na mtaji wakua zisha moja ya biashara ambayo ndugu zako wakija kuiona lazima wakuulze ulitoa wapi mtaji wa hiyo biashara.

Akiba tu ndio itakayokuokoa. Epuka MARAFIKI wakwepe kama ukoma Rafiki yako awe Kazi yako TU wengine urafiki wenu uwe wa salamu TU.

kumbuka dar huna ndugu watu wa dar hasa vijana wengi sio watu wazuri hasa wa huko mitaani kwahyo unaweza jilinda ukawa hufanyi kosa lolote lkn rafiki ako akakuponza.

Nilishawahi kupata rafiki enzi hizo nikamuona mtu ila alivyonisababisha kwenda lock up sijui mpaka na leo ila nilijifunza kwamba DAR si sehemu salama ya ku make friends otherwise hakikisha huyo mtu unaetaka kuwa na ukaribu nae u amjua in and out.

Utanishukuru baadae kama utafata huu ushauri.
Kaka samahani wapi naweza kupata room ya 15k kwa hapa dar,mimi ni mgeni
 
Kaka samahani wapi naweza kupata room ya 15k kwa hapa dar,mimi ni mgeni
Kwa msuguli
Kimara
Golani/bulula
Mpiji
kibamba
magomeni mapipa
tandale
mbagala
Mtongani
chamazi
Kibo
Makoka
Goba
Manzese
kinyerezi
nk nk nk nk....

si rahisi kuvipata hv vyumba kama utasema uzunguke mwenyewe,tumia dalali watakusaidia maana n sehemu za ndani ndani sna.
 
Bless up
 
Kama una mtaji mdogo karibu Pia Dar cha kwanza kabla ya chochote Panga room unapokua na makazi ni rahisi kwako kufanikiwa kuliko yule anaekuja kwa kutegemea kuanza kama kina sie.

Dar room zinaanzia 15,000 ni bei fair sana kwa mtafutaji / Mpambanaji.

Sikushauri upange room yenye umeme unapoanza anzia na room ya giza na usinunue chochote kwenye hiyo room.

zaidi ya hilo godoro ulilolalia/Net na Mswaki na ndoo za kuogea na kufulia...

Komaaa hapo hapo kwenye room yako ukiwa na vitu hvyo hvyo Kumbuka kilichokuleta dar ni Kutafuta PESA kwanza kisha mengine yatafata baadae.

Usichanganywe na vitu vya nnje Funga macho make pesa yako kila senti utakayopata Tunza ndani ya siku 365 utakua na mtaji wakua zisha moja ya biashara ambayo ndugu zako wakija kuiona lazima wakuulze ulitoa wapi mtaji wa hiyo biashara.

Akiba tu ndio itakayokuokoa. Epuka MARAFIKI wakwepe kama ukoma Rafiki yako awe Kazi yako TU wengine urafiki wenu uwe wa salamu TU.

kumbuka dar huna ndugu watu wa dar hasa vijana wengi sio watu wazuri hasa wa huko mitaani kwahyo unaweza jilinda ukawa hufanyi kosa lolote lkn rafiki ako akakuponza.

Nilishawahi kupata rafiki enzi hizo nikamuona mtu ila alivyonisababisha kwenda lock up sijui mpaka na leo ila nilijifunza kwamba DAR si sehemu salama ya ku make friends otherwise hakikisha huyo mtu unaetaka kuwa na ukaribu nae u amjua in and out.

Utanishukuru baadae kama utafata huu ushauri.
Ndiyo maana mimi rafiki yangu ni jamii forum
 
Niliwahi sikiliza kisa Cha mshikaji tbc Taifa, jamaa anasema alitoka mkoani kwao nakuja Dar ingawa wazazi wake walitia ngumu, alipofika Dar alienda kwa rafiki yake yaani ndiye aliyempokea basi mwishowe yule rafiki yake alianza kumuonyesha vitimbi vya hapa na pale

Ikafika kipindi yule rafiki yake akawa anakuja na demu then anamwambia mshikaji atafute pakulala jamaa akakaa akafikiria akufukuzae akwambiii toka,

Akawa anaenda k/ Koo kupiga mbonji kwenye magori ya watu asubuhi anaingia kwenye mishe ndipo akapata kazi yakumenya viazi Buguruni ikaenda akawa anakaanga kabisa mwishowe akaajiliwa na kuanza kupata mtonyo wa 6000 kila wakifunga mahesabu na zile alizobana akawa anaondoa na 15k

Hatimae alipanga chumba na mwishowe alimake vyakutosha akanzaa kuuza mihogo yakukaanga nayeye akaajiri watu hatimae akanunu matakataka yoote yagheto, inshort mchizi akawini maisha kimtindo kwani alipata na mwenza kabisa na wakabarikiwa kupata watoto

Akatoa wito kwa vjana ukiondoka kijijini hakikisha unaaga ili kupata baraka za wazi anasema yeye wazazi wake walitia ngumu lakini hii Leo anawasaidia kidogo anachopata.

The End
 
Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom