Karibuni Dar es Salaam wageni mnaokuja kutafuta maisha na kufanya biashara

Dar ni jiji ninalolifananisha na Jikoni kwa Tanzania hii, nadhani wote tunajua sifa ya jiko ni mahali panapoandaliwa na kupikwa vyakula vyote tunavyovipenda na tusivyovipenda.

Dar ni mkoa ambao naupa heshima ya kupafananisha na jiko kwasababu ni mkoa ambao ni chanzo cha kila kitu.

Ukitaka ma Pro watenda Dhambi utawapata Dar,

Ukitaka ma Pro wamwabudu Mungu utawapata Dar,

Ukitaka kila unachokijua wewe duniani taarifa zake ukiwa dar huwezi kosa.

Sasa basi kwa sifa hizo leo napenda kuwakaribisha vijana hasa wale wanaotamani kuanza maisha na hawana hata senti mfukoni.

Leo nitaongelea na kuwakaribisha zaidi wale wageni wanaotaka kuja kutafuta maisha dar/kufanya biashara dar ndio Lengo hasa la thread hiii.

Huwa ninapooongea na vijana wenzangu nawambia kwamba kama kuna kijana yeyote yupo dar ametafuta maisha,ametafuta pesa akaikosa Basi nimhakikishie ana asilimia chache sana za kutoboa kama akienda ktika mikoa mingine tofauti na dar.

KWANINI DAR?
Dar ni sehemu ambayo watu sio washamba wala hawashangai shangai

Hii ni faida sana kwako wewe kijana unaetaka kuanza maisha na una aibu, watu wengi hufeli katika maisha kwasababu ya aibu kuogopa watu kuona haya watu watamchukuliaje/watamuonaje,nk nk

Mikoani ukiokota makopo unaonekana chizi,ukiokota Chuma unaonekana kapurwa lakini DAR ni tofauti..

Wakazi wa dar ukipta ukiokota makopo wakikuona watajua wewe ni mtafutaji,wengine watakuita kukupa hata chupa zao za maji ambazo zimeisha, Ukiokota chuma hawatokuita kapurwa Watakuona ni kijana unaejitaftia zako riziki,nk nk

Kwanini wewe kijana ulie huko mkoani usije dar kuanza maisha? Unaogopa nini? Unahofia nini?

HUNA MTAJI?

Sawa kabisa, hata mimi wakati nakuja dar sikua na mtaji japo sikuja kiutafutaji nilikuja kimasomo nikajikuta nipo dar.

baada ya kumaliza masomo yangu nilijikuta mkononi nina Laptop 1,Sub woofer 1 na simu yangu.

sina hata senti 5 ila nina hivyo vitu,nilichofanya wala si kuviuza maana hata kama ningeviuza hela yake najua ningeikula pyuuuu nikabaki mweupe.

Nilichofanya ni kutafuta mtu niliewahi kumuamini (najua hata wewe unaesoma hii unae huyo mtu wa hivyo) nikaenda kumwambia naomba kaa na subwoofer yangu na hii laptop yangu.

Mkononi nikawa nimebaki na mzgo m1 ambao ni simu. Nikajiuliza maswali kadhaa kuhusu ile simu yangu Je. Hii simu naitumia kumtafuta nani? je Sasa hivi huyo ninaemuwaza kwamba ni wa muhimu Yuko wapi?

Nilijiuliza maswali kadhaa ila mwisho nilitoa laini yangu Nikaikata vipande kisha nikaanza tafuta mteja wa ile simu yangu.

Nakumbuka nili iuza kwa bei ndogo sana, baada ya kuiuza nikawa Freeman sina chochote mkononi zaidi ya mimi na miguu yangu.

Kazi ya kuanza tafuta kazi ikaanza,Kama unavyojua nawambia nyie wageni DAR watu hawashangai shangai Dar kila mtu na mishe zake.. Ukitaka attention ya watu wa Dar wasikie tu neno MWIZIIIIIIIIIIIIIII ndio utaona watu wa dar walivyo na ushirikiano wasikiapo hilo neno.

ila kama hawajasikia hilo neno kamwe huwezi chukua attention ya wakazi wa dar kizembe zembe Hiyo MAANA YAKE NINI?

Dar hutakiwi kuwa MWIZI au MDOKOZI kama kweli unataka kuja Kuishi kwa amani DAR.

Basi baada ya kujua wakazi wa dar hawana tofauti na wa New York nikaingia mtaani Dear Mgeni unaesoma hii thread Hamna kazi unaijua sijaifanya, ya kudharaulika ambayo sidhani kama wewe mgrni utaweza ifanya.

Lakini nilifanya kazi zote hizo nikiwa na malengo ya siku 1 niwe na changu niajiri watu,niliamini Baada ya kumaliza masomo ya Chuo kuna Chuo kingine kinaitwa DUNIA UNIVERSITY.

Hiki chuo elimu yake ni bure ila itacost UTU wako,itacost HESHIMA yako,itacost kila unachokithamini sasa.

Ukija DAR lazima iku cost kama ndio umeamua na kudhamiria kuja tafuta maisha.

Kwahiyo nilikubaliana na nafsi yangu lazima nipitie yote hayo ili nitakapopta niwe na stori ya kusimulia.

Mgeni unaekuja DAR jiandae kisaikolojia kuliko kimwili, kuna torturing kwa wingi sana huu mkoa kuliko ufikiriavyo lakini zisikukatishe tamaa maana zote zakupasa uziptie ili uje kuwa mtu ktk watu siku 1.

Ukija Dar jiepushe na makundi na elewa hili ni jiji lisilo na huruma, kama ulifikiri utaomba mtu sh 500 akupe SI KWA DAR kama ulifkiri utaomba chakula chabure si kwa dar so jiandae ktk hilo ukija fahamu unaenda sehemu utakayo tritiwa kama Mtu usieaminika wala kuonewa huruma.

Ukija dar Usichague kazi, kazi zipo nyingi sana zifanye hizo na hakikisha una save pesa zako usikae bila kazi dar kazi zipo everywhere ni wewe tu kuzifata na kuzifanya.

DAR yakupasa uwe na ujasiri! ondoa mashaka na uoga lakini usiache kusema ukweli wa maisha yako endapo utaulizwa na yeyote kuhusu ulipotokea imekuaje hadi ukawa hapo ulipo usiogope ongea kwa uhuru na usionyeshe kuhitaji msaada wake Chukulia hicho unachomuambia n kama unampgia tu stori.

ukionyesha tu huruma za kutaka akusaidie "ndio umekosa msaada" so stay strong ongea mapito yako kwa ujasiri usitilie tilie huruma.

Nimeshakwambia Wakazi wa DAR hawana huruma maana Huruma zao zimeshawaponza sana sana sana. Kwahiyo Usitegemee kwamba utampa mkazi wa dar stori ya dada ako aliebakwa au wewe ulivyobakwa akakuonea huruma.

Zaidi Zaidi ndio utazidi jianika na kumfanya akuweke ktk kundi la "handle with a great care" mkazi wa dar ukimletea tu stori za huruma huruma ujue kama alikua anataka kukusaidia basi ndio ataacha so STAY STRONG AS CROCODILE.

Naamini Dar ni sehemu ya Utafutaji na wala si sehemu ya kuishi kwahiyo Njoo DAR na mission yako 1 ambayo ni "kutafuta" ukishazipata your free to go dear ukazipge pesa mkoani.

Nasemaga mimi dar ni sehemu yakutafutia mtaji ukishapata mtaji kama unajiona huelewi elewi kimbia mkoani huko anzisha biashara kwa mtaji ulioupatia DAR.

Japo kwa mimi sina mpango wa kuhama Dar hata kwa bastola ila pia sina mpango wakutulia tu dar kibiashara ni lazima nipanuke kufika mikoa yote hii nchi KWANINI unajua?

Mtaji wangu ni JIJI LA DAR uwepo wa hili jiji ni pesa, siogopi lolote ninapokua dar Hata nianguke sasa nianze SIFURI sitochukua muda mrefu tena kusimama.

KWANINI?

DAR ndipo mahali pesa za Nchi hiii zinejificha, watu huzamia meli kwenda Ulaya nashangaa sana kuona kuna mtu yupo bush hana channel anashndwa zamia LORI aje dar.

Tokeni hapo ulipo ukiwa kama kijana una nguvu kimbia haraka DAR jichanganye chapa kazi kama punda ndani ya mwaka mmoja wenye siku 365 nakuhakikishia utakua na mtaji wa kuanzisha biashara yako Nzuri.

Kubali kuteseka mwaka 1 tu ukiwa dar then the rest itabaki story.

Dar inakuhitaji wewe,njooo na akili yako TU/adabu/uaminifu/nk kisha Pesa utazikuta huku huku.

Asiekubali kuanzia chini kamwe asitegemee kufika Juuu, Ukija dar kubali anzia CHINI tena chini chini kweli kweli.

Utaonewa/dharauliwa lakini usijali Akili ipo kichwani mwako.
Yeap Yeap nakubal kaka
 
Dar watu wanafanya biashara za mitaji ya 30,000

Watu wanafanya Biashara za mitaji ya 50,000

Watu wanafanya biashara za mitaji ya 10,000

Hao wote kupitia biashara zao.kila mmoja wao jioni anarudi nyumbani kwake na chochote kitu.

Nimekupa mifano ya hao watatu uione kisha utajipima mwenyewe na huo mtaji wako ulio nao ukija utatoboa au lah...

Nadhani Dar inahitaji UTAYARI wako tu kuyatafuta maisha DAR hai hitaji capital (pesa)

Maana wapo/Tupo tulioanza from ZERO na sasa atleast tuna mudu 3 meals na tulikuja with nothing.

Jiulize swali 1, Nipo tayari kuyatafuta maisha? Kisha jibu lako litakuinua hapo ulipo sasa na kuanza kulifanyia kazi kwa vitendo.

Mil.1 usiifikirie sana tena usiiweke hata kwenye mahesabu Njooo akili yako ukiwa umeielekeza kwenye utafutaji na usiweke roho na macho yako kwenye hyo 1.3M

Maana unaweza Fika DAR tu leo Paaap Kwa mazingira ambayo hutoyajua wala kuelewa ukajikuta huna hiyo 1.3M una nguo ulizovaaa TU.

Usitake kujua zitaenda wapi, (huo ni mfano tu) inaweza isiwe kweli, sasa kama wakikwapua hizo hela Si utakuja dar uzimie ufe mkuuu?

Lakini kama akili yako uliiweka ktk kutafuta Utajisemea MIMI NI MTAFUTAJI 1.3M ni kitu gani? nimeshapoteza vingapi? utajiuliza maswali ya kijasiri kisha utaingia tena Mzigoni kutafuta pesa kama kijana mpambanaji.

Sishauri mgeni anaekuja DAR hata awe na mtaji wa 20M aanze biashara yyte, dar iko full of FAKE PEOPLE kila sehemu kila kona kila chobingo kila sehemu...

Kabla hujaanzisha biashara Dar kwa mgeni Kubali kuanza chini Jifanye mjinga Poteza hata mwaka mzima ukiusoma MJI na Watu wake.. Mwaka ni mrefu lkn utakuja siku 1 kujua umuhimu wa kusoma watu na mazingira ya eneo ulilopo.

Biashara inahitaji Research huwezi pata majibu sahihi ya utafiti unaoutaka dar kama utajitia umekuja ki don don una mipesa umeifcha bank.

Ili upate real info ni lazima ukubali kushuka ukubali kuanzia chini kule mchangani kwenye matope,kubali kudharaulika kidogo uje uheshimike Milele.

Dar inahitaji Akili si vinginevyo.
Mkuu nimebarikiwa sana kwa nondo zako, asante sana.
 
Back
Top Bottom