hasan124
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 716
- 128
- Thread starter
- #121
Tatizo sio rangi Christina na mwenzio tatizo ni ubunifu hakuna mmecopy kila kitu bado sera tu
Sehemu ya Katiba yetu inasemaje haya yafuatayo:
1. Ukomo WA Uongozi: Vipindi viwili vya miaka mi5 mi5 kwa uongozi WA Kitaifa.
2. Kiongozi kutangaza Mali zake ndani ya KIPINDI cha MIEZI MITATU mara baada ya kuchaguliwa.
3. Kufukuzana: Kutakua na CHOMBO cha Kutatua migogoro ya chama nje ya chama kitakachokuwa CHINI ya Uongozi WA Mwanasheria AMA jopo la wanasheria ili kukwepa personal interest ie: makundi hivyo suala la kutimuana kiholela halitokuwepo katika chama Chetu.
4. KATIBA pia itatambua Uwepo WA MwenyeziMungu, Itasaidia kupata viongozi waadilifu, wachamungu hivyo kupunguza matendo yote maovu ie: Ufisadi, Wizi WA Mali za Umma, Udikteka etc.
5. Walemavu wasipungue asilimia TANO (5%) katika ngazi zote za Uongozi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna zaidi ya walemavu millioni NNE (4mil.) NCHINI Tanzania.
6. Asilimia hamsini ya wanawake katika ngazi zote za Uongozi.
Vp kuna eneo tumewaingilia mpaka hapo? Tazama kwenye blue utajua tumejipanga kwa KIASI gani. Punguza kuropoka pia.
KARIBUNI ADC - DIRA ya mabadiliko.