Karibu Wema Sepetu, je utavumilia mikikimikiki ya Upinzani?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Ukiwa mpinzani nchini Tanzania unatakiwa ujiandae kiakili. Wema Sepetu na Mzazi wako mmejiandaa?
========================================================
Mariam, ambaye ni mama mzazi wa mrembo huyo wa Tanzania 2006 alifikishwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jana kwa madai ya kujipatia fedha hizo kutoka kwa mfanyabiashara, Alex Msama.
Habari kutoka katika kituo hicho zinadai kuwa Mariam alifunguliwa jalada la taarifa ya polisi Na. OB/RB/3358/2017 na alishikiwa kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa 12 jioni alipoandikisha maelezo na kudhaminiwa na watu wawili waliotajwa kwa majina ya Rose Moshi na Martha Mtiko.

Dar es Salaam. Mama mzazi wa msanii maarufu nchini, Wema Sepetu ametiwa mbaroni jijini hapa kwa madai ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mariam, ambaye ni mama mzazi wa mrembo huyo wa Tanzania 2006 alifikishwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jana kwa madai ya kujipatia fedha hizo kutoka kwa mfanyabiashara, Alex Msama.

Habari kutoka katika kituo hicho zinadai kuwa Mariam alifunguliwa jalada la taarifa ya polisi Na. OB/RB/3358/2017 na alishikiwa kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa 12 jioni alipoandikisha maelezo na kudhaminiwa na watu wawili waliotajwa kwa majina ya Rose Moshi na Martha Mtiko.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda alisema hana taarifa na kuahidi kuzungumzia suala hilo leo.

Inadaiwa kuwa Mariam ambaye hivi karibuni yeye na binti yake huyo waliihama CCM na kujiunga na Chadema, alikubali kumuuzia Msama nyumba iliyopo katika Kiwanja 663 Block E, maeneo ya Sinza kwa Sh125 milioni.

“Nyumba hiyo ilikuwa inatakiwa kupigwa mnada na benki ya TIB kwa sababu mama Sepetu alikuwa amemdhamini mtu aliyekuwa amekopa katika benki hiyo, yule mtu aliposhindwa kulipa, watu wa benki wakataka kuipiga mnada,” chanzo chetu kutoka Polisi Osyterbay kilisema jana jioni.

Katika maelezo ambayo yapo kituoni hapo, inadaiwa kuwa Mariam alikubali kumuuzia nyumba Msama ili apate fedha za kuilipa TIB, lakini kwa wakati huo Msama hakuwa na kiasi hicho.

Inadaiwa kuwa wakati Msama akiendelea na mchakato wa kutafuta fedha ikiwa ni pamoja na kufuatilia mkopo kwenye benki nyingine ili ainunue nyumba hiyo, Mama Wema alikuwa akipewa fedha kidogokidogo ambazo zilifika Sh14 milioni.

Hata hivyo inadaiwa kuwa baada ya mama huyo kuona mchakato huo unachelewa aliuza nyumba kwa mtu mwingine bila kumtaarifu Msama, ambaye alijulishwa na dalali.

Jana, wakati wa mahojiano na polisi inadaiwa kuwa Mariam alikiri kupewa Sh8 milioni ambazo zipo kimaandishi na hatambui kuhusu fedha nyingine.

Msama alipopigiwa simu jana usiku alikiri kumshtaki mama huyo Polisi Oysterbay na kusisitiza kuwa anachotaka ni kulipwa haki yake.

“Ni kweli suala hili lipo Polisi kama mlivyosikia, sipendi kulizungumzia sana,” alisema Msama ambaye pia ni mwandaji wa matamasha ya injili.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alithibitisha kushtakiwa kwa kada huyo mpya wa chama chake na kusema aliandika maelezo kuhusu suala hilo na kuachiwa.

Source: Mwananchi
 
Tunataka tujue wewe ni CCM au upande wa alikohamia Wema?? Maana taarifa yako imekaa kwa kuegemea kuwa kwa sababu wema kahama chama ndio atarundikiwa makesi ya ajabu ajabu. Hebu weka sawa maana ni kama taarifa tu ya Huyo msama na mama Wema hebu mnapoandika muwe mmeshabalehe tayari jamani tuna mambo ya kuangalia hasa Tanzania ya vi-wonder
 
Manyumbu na swala hili mtasema ni la kisiasa, na kwamba ccm ndio inamdai, maana hamkawii nyie.
 
Tunataka tujue wewe ni CCM au upande wa alikohamia Wema?? Maana taarifa yako imekaa kwa kuegemea kuwa kwa sababu wema kahama chama ndio atarundikiwa makesi ya ajabu ajabu. Hebu weka sawa maana ni kama taarifa tu ya Huyo msama na mama Wema hebu mnapoandika muwe mmeshabalehe tayari jamani tuna mambo ya kuangalia hasa Tanzania ya vi-wonder
Mkuu Tanzania ya vi-wonder imemshinda mkuu wa Nchi Mimi nitaiweza?
603d9d4c2ee7cc7c708cf049a8f01c19.jpg

Tunataka tujue wewe ni CCM au upande wa alikohamia Wema?? Maana taarifa yako imekaa kwa kuegemea kuwa kwa sababu wema kahama chama ndio atarundikiwa makesi ya ajabu ajabu. Hebu weka sawa maana ni kama taarifa tu ya Huyo msama na mama Wema hebu mnapoandika muwe mmeshabalehe tayari jamani tuna mambo ya kuangalia hasa Tanzania ya vi-wonder
Haya ni matokeo yangu ya kidato cha nne
 
Sijawahi ona user wa ajabu kutumia jina la kondom its shame
Unashangaa ID yangu! Endelea kushanga na ID za users wengine ndio urudi tena, ila ukweli ndio huo,machadema mnapelekwa pelekwa tu, hamuhoji kwa nini hamna ofisi mpaka Leo! Hamhoji gharama za kuendesha Kesi mbona wanaolipwa ni walewale tu! Hamhoji hata mapato na matumizi ya ruzuku, hamuhoji lini mtafanya uchaguzi mkuu wa Mwenyekiti wenu wa maisha, mko bizi kusheherekea dhamana na kufurika mahakamani kushangaa Kesi!
 
Kwa hiyo unataka mapato na matumizi yasomwe hapa jf?
Unataka uchaguzi wa chama ndani ya cdm ufanyike hapa jf?
 
Haya sema sasa mapato na matumizi mlifanyia wapi kikao na uchaguzi lini, na utuambie Makengeza ana miaka mingapi ya uenyekiti wa kudumu mpaka sasa!
 
Mkuu inaonekana wewe ni Bashite. Ngoja nikupuuze ili usije niachia ubashite wako hapa
 
Unashangaa ID yangu! Endelea kushanga na ID za users wengine ndio urudi tena, ila ukweli ndio huo,machadema mnapelekwa pelekwa tu, hamuhoji kwa nini hamna ofisi mpaka Leo! Hamhoji gharama za kuendesha Kesi mbona wanaolipwa ni walewale tu! Hamhoji hata mapato na matumizi ya ruzuku, hamuhoji lini mtafanya uchaguzi mkuu wa Mwenyekiti wenu wa maisha, mko bizi kusheherekea dhamana na kufurika mahakamani kushangaa Kesi!
CCM ndio chaka la waghushi vyeti
 
Acha maneno mengi mkuu tuleteeni vyeti vya bashite ndio tuendelee na mambo mengine kama viwanda vya kusadikika
 
Back
Top Bottom