Karibu wapinzani wote tuunganishe nguvu kuleta mfumo wa vyama vingi halisia

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Historia inafundisha mengi na watanzania mkifuatilia historia ya imani unaweza kuifananisha na historia ya mfumo wa siasa kama unataka kutafuta matokeo chanya.

Nikirejea katika historia ya imani za dini unaweza kuona wazi jinsi ambavyo wanadamu mwanzoni walikuwa kila jamii ilikuwa imeshikilia imani moja na wanajamii hawa waliwekeza nguvu zao zote katika kulinda imani yao hiyo. Viongozi waliamini waliwekwa madarakani "enzi hizo wafalme" na miungu na hivyo wafalme hawa ni kama walikuwa wakiapa kuilinda miungu hiyo kwa nguvu zao zote. Haikuwa rahisi kwa mwanajamii kuibuka na kupinga imani hizo.

Haikuwa kazi nyepesi kwa wale wanadamu wa kwanza waliokuja kuvunja mifumo hii ya imani moja katika jamii kama huamini futalia historia mbali mbali za imani.

lakini leo hii imani hizi hizi zimekuwa huria, mtu yeyote analala anaota na kesho yake anaanzisha imani yake, hakuna anayejali na anapata wafuasi.

Lipo somo kubwa ambalo tunaweza kujifunza kutoka katika mfumo wa imani kuwa kubadili mfumo wa kitu si kazi rahisi na akili ya mpumbavu atakwambia unahitaji watu wa "kujitoa" lakini kwa watu makini watakwambia kinachohitajika ni akili ya ziada kubaini njia nyepesi ya kutuharakisha kuleta mabadiliko.

Ukifuatilia historia za siasa unaweza kuona wanasiasa wengi waliojaribu kupambana na mfumo wa chama kimoja kokote duniani walikutana na ukinzani uleule waliokutana nao wana imani waliojaribu kupambana na mfumo wa imani moja kwa jamii tofauti ni wakati kuwa wanadamu wa kizazi hiki wamestaarabika na hivyo matendo yao ni yakistaarabu na wanadamu wa enzi hizo ustaarabu ulikuwa chini na matendo yao yaliendana na wakati huo.

SASA TUNATOKAJE HAPA TULIPO WAPINZANI WENZANGU

Itakuwa ni upofu kwa mpinzani yeyote kuwaza kuchukua madaraka katika hii "transition period" ya kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda mfumo wa vyama vingi.

target ya wapinzani wote kwa sasa inatakiwa kuleta mageuzi ya mfumo wa siasa kutoka mfumo wa chama kimoja na kuwa na mfumo kamili wa vyama vingi.

Tunaweza kufika huko kwa haraka ikiwa wapinzani wote tutaungana ili kutafuta hili hivyo basi napendekeza muungano ufuatao

1. wapinzani wote tuungane tuunde chama kimoja kinachoitwa CHAMA CHA WANANCHI (CCW)
2. Rangi za bendera yetu ni kijani na nyeusi na mavazi ya wanachama wetu yatakuwa hivyo
3. Sera zetu sisi ni wananchi wanashida zipi na sera zetu ni kutoa ahadi za nini tutakifanya ikiwa wananchi watatupa ridhaa.

Katika swala la sera naomba kufanunua kidogo kuwa tatizo lililopo la wapinzani wenzangu wengi ni kufanya "uanaharakati" badala ya siasa.

mfano 1. serikali ya sasa ninapoandika haijapandisha mishahara sasa kwa chama mbadala sera zetu sisi ni kuwaahidi wananchi kuwa sisi tukipewa madaraka tunaamini mtumishi kupandishwa mshahara kila mwaka ni hitaji la kisheria na kiuchumi hivyo sisi lazima tupandishe mishahara kila mwaka ili kukidhi mahitaji ya kisheria na kujenga uchumi wetu. Wananchi watuelewe hivyo na watawala walioko wasipopandisha watawaeleza wananchi kwa nini hawapandishi na ukifika uchaguzi wananchi watapima tunachokisema na wanachokisema.

Uana harakati ni pale chama cha siasa kisipotamka kinasimamia nini katika hili kama sera zake na kugangania kulazimisha watawala kufanya tofauti na sera zao wanazotekeleza.

Mfano wa 2. Mifuko ya hifadhi ya jamii ni kizungumkuti, watu kupata mafao yao ni shida kwa sasa, kama chama cha siasa sisi tunasema hizo ni sera za watawala na sisi kama chama cha siasa tutaweka wazi msimamo wetu wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa mifuko hii sio mifuko ya kutunza wazee au mifuko ya kutafutia fedha za serikali kufanyia miradi au fedha za kuweka tu ili watumishi serikali inaowaajiri wazitumbue watakavyo.

Sisi tutaweka bayana kuwa malengo ya mifuko ya hifadhi ya kuhahakisha watanzania wote wanapata ustawi, ustawi huu tutausoma kwa kila kuangalia kila kundi lina uhitaji upi na tunaweka mifumo ya kila mwananchi mwenye uhitaji aliyeweka akiba yake mifuko ya hifadhi ya jamii anapata msaada.

kwa kifupi Siasa za chama chetu zitakuwa "maslahi ya wananchi ndio sera zetu"

hivyo hatutajiingiza katika siasa za kupinga mambo ambayo yanamaslahi kwa wananchi kwa dhana ya wapinzani wanatakiwa kupinga serikali na kujifarakanisha na wananchi bali kwa yale ambayo watawala watayafanya na ya maslahi mapana kwa wananchi tutayaunga mkono lakini tutawaeleza wananchi ni kwa jinsi gani wakitupa sisi nafasi tutayafanya mambo hayo kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Makosa wanayofanya watawala kwetu sisi itakuwa ni fursa za kuwapa wananchi mtizamo mbadala ni nini tutakifanya kama wakitupatia nafasi.

MWISHO

Mabadiliko ya mfumo yatatoka kwa wananchi wenyewe. Tukijenga imani kwa watanzania, wakatuamini wakasawazisha tofauti zetu zile za idadi katika vyombo vya maamuzi ya sheria, tukawa na uwiano ambao watawala na sisi ili tupitishe jambo lazima tukubaliane ndio njia pekee ya kubadili mfumo.

Kwa wananchi wakitambua umuhimu wa hilo na sisi wenyewe tukawajengea imani kwa kuonekana tunatambua shida zao na tuna mawazo sahihi yanayowapa matumaini.

Uchaguzi wa jina la chama na rangi za bendera ya chama ni wa kimkakati katika kuhakikisha tunafanikiwa katika malengo yetu.

Nawakaribisha wapinzani wenye nguvu wote tuunganishe nguvu za hoja pamoja.

tukishafanikiwa kuleta sera za vyama vingi kamili huko mbeleni sasa vyama vya siasa vitakuwa kama dini kwamba ukilala ukaota baba wa taifa anakutuma kuanzisha chama basi ukiamka unaanzisha chama na unapata wafuasi kama zilivyo imani leo
 
Back
Top Bottom