barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Karibu Kigoma Mkuu mpya wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali mstaafu Emmanuel Maganga, uliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.Dkt John Pombe Magufuli..........Mkuu mpya wa mkoa amewahi kuwa Mwambata wa jeshi nchini Afrika kusini, marekani na canada, Brigedia Genrrali Emmanuel Edward Maganga alikuwa miongoni mwa majenerali 16 walioagwa na JWTZ tarehe 03 march mwaka huu jijini Dar es salaam, amestaafu baada ya utumishi wa miaka 37 jeshini na amestaafu akiwa na wadhifa wa mkaguzi mkuu wa jeshi. Ni mwanadiplomasia , mpenda michezo na zaidi ni Mwandishi wa habari . Tutashirikiana nawe kikamilifu .
Mkoa wa Kigoma unakabiliwa na tatizo sugu la wahamiaji haramu kutoka katika nchi za Rwanda,Burundi na DRC Congo.Mapori mengi ya mkoa wa Kigoma yanavamiwa na raia wa kigeni kutoka nchi hizo na hivyo kaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa.Uhalifu wa kutumia silaha za kivita kwa Watanzania waishio katka vijiji vya pembezoni ni mkubwa sana,tuna imani kwa uzoefu wako wa kijeshi utakabiliana na tatizo hili.Tunakukumbusha tu siasa za mkoa wa Kigoma ni "ngumu" kidogo.Huku kuna watu "wabishi" sana wasio marafiki wa chama tawala.Kihistoria mkoa huu umekuwa ni mkoa wa saisa za mageuzi toka mfumo wa vyama vingi kuanza,na hii inadhihirishwa tu na uwepo wa Meya wa Mji kutoka katika chama kikuu cha upinzani Kigoma Mjini cha ACT.Tunajuwa wewe ni mtu wa kazi na si "mwanasiasa",utafanya kazi vyema na madiwani,Meya na Mbunge toka chama cha upinzani
Mkuu wa mkoa karibu Kigoma-Ujiji,Mji mkongwe usio na mawaa.Karibu "kijiwe" cha Urusi kwenye kitovu cha siasa za hoja za ujiji.Kwetu Ujiji hatuna bar wala sehemu za starehe,ni madrassa na misikiti.Ujiji ya Stanley na Dr Livingstone.Karibu tena Ujiji....kabla hujafika huku pitia kwa Mzee Yusuph Makamba,mwambie akupe "uzoefu" wa mkoa wa Kigoma na hasa eneo la "Ujiji".Mwisho tunakuandalia migebuka,mawese na dagaa wa Kigoma.Karibu Kigoma Mwisho wa Reli.....Mv Liemba ndio usafiri wetu,ATCL ni kwa nyie viongozi na gari moshi kwa wale waendao Dsm na mikoa ya Kati