Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya Kidato cha Sita 2020

Aug 10, 2011
72
14
Mdogo wangu kapata 2 ya 11 (DDC) anataka kusoma medical,is it possible?

=====

Habari wanaJF,

Leo Baraza la mitihani la Tanzania NECTA limeyatoa matokeo ya kidato cha sita, kwa uzoefu wangu nimeona ni vyema tuanzishe uzi huu maalumu ili tushauriane, tueleweshane, tuambiane nini cha kufanya na namna ya kuchagua vyuo.

Ikumbukwe TCU wana vigezo kwa ajili ya kujiunga na elimu ya juu.

Karibuni.
 
Nimemaliza form 6 comb PCM na matokeo yang ni div 2 point 10.

Physics. (D).

Chemistry. (D).

Adv.maths. (B).

kwa wazoefu mlioko chuoni, kwenye ajira na mliojiajili naombeni mnishauli faculty nzuri ya kusomea yenye uafadhali wa maslahi, urahisi wa kuajiliwa au kujiajili kama nikifanikiwa kumaliza chuo.

N.B mliosoma PCM na mko chuo au mmemaliza nahitaji zaidi mchango wenu
 
Nimemaliza form 6 comb PCM na matokeo yang ni div 2 point 10
Physics. (D)...
Kwa ufaulu wako sijui kama utapata nafasi ya Civil Engineering, kama itawezekana kasome hiyo kozi, ukikosa degree kasomee hata diploma ya hiyo fani.

Kajaribu na Electrical. Kama ingekuwa awamu flani flani ningekushauri ukasome kozi za IT related (eg. Computer Engineering, Computer Science, Information System, ) kwa sasa hata hizo kozi mtaani kugumu kupata deal za maana labda uwe mbunifu sana.
 
Jamani msaada

Chemistry-E
Biology -C
Geography-D

Akasome nini huyu jamani?

Je? Biotechnology anaweza soma? Nursing je?

Au ipi kozi ya mifugo.
Mawazo
 
Nimemaliza form 6 comb PCM na matokeo yang ni div 2 point 10.

Physics. (D).

Chemistry. (D).

Adv.maths. (B).

kwa wazoefu mlioko chuoni, kwenye ajira na mliojiajili naombeni mnishauli faculty nzuri ya kusomea yenye uafadhali wa maslahi, urahisi wa kuajiliwa au kujiajili kama nikifanikiwa kumaliza chuo.

N.B mliosoma PCM na mko chuo au mmemaliza nahitaji zaidi mchango wenu
Kasome actuarial science hutajutia
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi nimehitimu combination ya HGE

HISTORY -D
GEOGRAPHY -E
ECONOMIC-D

O level nilipata

Mathematics-C
BIOLOGY-C
GEOGRAPHY-C
PHYSICS-D
CHEMISTRY-D

Nimeambatanisha matokeo ya O level kwasababu kuna KOZI wanazingatia hayo
Binafsi napenda kusoma COMPUTER SCIENCE , IT & ICT AU KOZI ZINAZOENDA NA HIZO
BUT KUTOKANA NA UFAULU HUO VYUO VICHACHE NAKIZI VIGEZO

Mfano SUZA, MZUMBE, NIT ila kutokana na hofu ya competition nimekuja HUMU WAKUU kuomba ushauri WA KOZI nyengine nzuri ili nikikosa hizi nisiyumbe lakini KOZI zinazotoa ujuzi na sio certificate tupu

KAMA YUPO MUHITIMU MWENGINE UZI WETU NDIO HUU TUOMBE USHAURI

Napenda kutanguliza shukrani kwa niaba ya wanafunzi wote

AHSANTENI
 
Ok, kwa ngazi ya degree huwezi kusoma kozi yoyote ya ICT kwakuwa hukusoma masomo ya sayansi.
Kama ukitaka unaweza ukaanza diploma ya CS, moja kati ya kozi bora kabisa.
 
Wote wapate UJUZI, UFUNDI STADI na umahiri katika kutumia Technologia ya Computer ili wawezeshe kujiajiri, kuajiriwa na kuongeza UFANISI na TIJA katika shughuli binafsi, Biashara, viwanda vidogo na vikubwa.
 
Olevel umesoma sayansi,A level umesoma madudu mengine,history,!!!HV huwa mmelogwa au?unapokuwa kidato cha pili,unatakiwa uwe unajua,utasoma masomo gani,kidato cha tatu,na unataka uwe nani huku duniani, dakitari, Muhandisi, Mtaalamu wa kilimo, ICT, Mwanasiasa, Mwalimu, Mwanasheria, nk, sasa ukipelekwa na upepo wa matokeo,inakuwa umepoteza muda,sasa wewe unataka kusoma IT,wakati kidato cha sita hukusoma sayansi!kwahiyo inabidi ukatumie cheti cha form four,sasa miaka miwili ya A level,siimepotea bure,,baada ya kumaliza form four, ungeenda DIT, ungepiga, diploma, miaka miwili, then unaunganisha mitatu tena sasa HV, ama ungekuwa unasoma bachelor In Engineering,au ungekuwa kazini,unalipwa mshahara.

Sie Anko zenu,tumemaliza form four 99,kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii,no mobile phones,no smart phones,lakini tulijitaidi kupata taarifa,za kutosha ni nini tunataka maishani na nini tusome,sasa Leo kila kitu kipo,information on ur fingertips,!!!mnafeli wapi?!!!inakuwa kama mnasoma kama vipofu,mkigonga ukuta ndio mnajua mmefika,
Mimi niliamua kuwa nataka kuwa engineer nikiwa kidato cha pili.

Na niliihapa lazima nisome UD nikiwa darasa la saba,nilivutiwa na matamasha,ya siku ya mtoto was afrika yaliyokuwa yakifanyika UD ukumbi wa nkuruma.
 
Ndugu, ndo ulifanya nini..?

Yaan mtiti wa kusoma physics, chemistry, math, bios na akatoboa japo si kwa kiwango kikubwa then A level ukaenda kupiga huo utopolo sijui wa HGE.. Duuh umezingua sana, wenzio hzo pass za sayansi wanazitafuta kwa tochi wasome kozi za sayansi e.g Afya..

Ungeanza hata cheti CO,nursing,engineering, ICT ingekuwa poa sana na wala usingekuja Julia hapa.

Binafsi Physics nilizingua Olevel ila sikukubaki kwenda kupiga Art A level.

Yaan nina Average zangu nzuri za Bios,Chem, math,geog naendaje Art...!!
 
Tafuta guidebook ya 2020/2021,isome vzr kwa vyuo vyote vinavyotoa hiyo course unayoitaka nadhani utapata chuo kinanacho endana na sifa ulizonazo.
 
Olevel umesoma sayansi,A level umesoma madudu mengine,history,!!!HV huwa mmelogwa au?unapokuwa kidato cha pili,unatakiwa uwe unajua,utasoma masomo gani,kidato cha tatu,na unataka uwe nani huku duniani,dakitari,Muhandisi,Mtaalamu wa kilimo,ICT,Mwanasiasa,Mwalimu,Mwanasheria,nk,sasa ukipelekwa na upepo wa matokeo,inakuwa umepoteza muda,sasa wewe unataka kusoma IT,wakati kidato cha sita hukusoma sayansi!kwahiyo inabidi ukatumie cheti cha form four,sasa miaka miwili ya A level,siimepotea bure,,baada ya kumaliza form four,ungeenda DIT,ungepiga,diploma,miaka miwili,then unaunganisha mitatu tena sasa HV,ama ungekuwa unasoma bachelor In Engineering,au ungekuwa kazini,unalipwa mshahara.
Sie Anko zenu,tumemaliza form four 99,kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii,no mobile phones,no smart phones,lakini tulijitaidi kupata taarifa,za kutosha ni nini tunataka maishani na nini tusome,sasa Leo kila kitu kipo,information on ur fingertips,!!!mnafeli wapi?!!!inakuwa kama mnasoma kama vipofu,mkigonga ukuta ndio mnajua mmefika,
Mimi niliamua kuwa nataka kuwa engineer nikiwa kidato cha pili.
Na niliihapa lazima nisome UD nikiwa darasa la saba,nilivutiwa na matamasha,ya siku ya mtoto was afrika yaliyokuwa yakifanyika UD ukumbi wa nkuruma.
hapo ndipo nilipokudharau
 
Back
Top Bottom