Karibu shujaa Tundu Lissu; Umemaliza ngwe ya kwanza, umeona mwenyewe Tanzania ilivyokupokea. Hii iwe ngwe ya pili...

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,224
26,039
Karibu Shujaa Tundu Antipas Lissu!

Tanzania imekuona, Tanzania imeamka. Tanzania imeshtuka kutoka usingizini.

Umemaliza ngwe ya kwanza, umeona mwenyewe Tanzania ilivyokupokea. Ni dhahiri kuwa watanzania wanakupenda ni dhahiri pia kuwa watanzania wameamka. Hawababaishwi tena na pambio za kusifu na kuabudu. Hawababaishwi tena na propaganga

Nirudi kwenye mada!

Kwenu Chadema, Watanzania wanawapenda, watanzania wanawaamini, watanzania wanataka mbadala wa utawala ambae wanaamini atawafanya wapate maendeleo ya kweli na si kama ilivyo sasa wanaona maneno kwenye makaratasi huku hali zao za kimaisha sikuwa zinadhoofu kila kukicha.

Ni dhahiri shahiri kuwa CCM hawawezi kupambana na Lissu, walijaribu kumfungulia kesi wakashindwa, wakajaribu kumpiga risasi wakashindwa sasa hawajaamini kama kamanda katua na yuko tayari kupambana nao. Lissu kajipanga, vyovyote vile kwa uhalisia amewatega CCM na viongozi wake pabaya sana. Kwa ufuatiliaji huu wa hali yake na usalama wake kimataifa Nina uhakika sasa wa asilimia 100 hakuna anayetaka kutolewa arrest warrant na ICC kwa sababu ya Lissu.

Sasa Chadema katika haya yote nendeni hatua ya pili kwa kufanya haya!

1. Andaeni ilani kabambe inayoenda kuibadilisha hii nchi completely kutoka uchumi wa kijamaa kwenda kwenye uchumi wa kibepari. Uchumi unaondoa control ya serikali kwa asilimia 100 kwenye biashara, uwekezaji na uchumi. Kwenye ilani hii muelewe na kuweka kila kitu ni kwa jinsi gani mnaenda kutumia sekta binafsi katika kuibadilisha Tanzania kiuchumi na kimaendeleo.

2.kwa muda uliobaki fanyeni mawasiliano na urafiki na Kagame, Museveni na Kenyata. Fanyeni vikao na vyema vyao na kufanya nao makubaliano. Msiishie hapo, nendeni na Malawi na Zambia Pia. Mnaitaji support na ushirikiano na hawa watu. Najua mnajua kwa nini nimesema hivi. Aliyepo hakubaliwi na hawa watu. Itumieni hii nafasi vizuri. Support yao ina umuhimu mkubwa

3. Andaeni Mpango mkakati wa kuiendesha Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa October mwaka huu. Kuanzia mtafanya nini kwa kipindi gani.

4. Najua mtampitisha Lissu, ila kwa msisitizo mpitisheni. Huyu mtu Mungu yupo nae. Nimeona Safari zake. Sijaona akishindwa. Muwekeeni wasaidizi wazuri watakaomsaidia kazi zake kipindi chote cha kampeni. Wawe watu waaminifu.

5. Kuanzia sasa fanyeni kazi kubwa kuweka mipango kabambe ya kufufua suala la ajira kwa watanzania, kukifanya kilimo kiwe cha kisasa na kibiashara na kuifanikisha nchi hii kwenye sekta zote ambazo zitaipandisha hii nchi kiuchumi haraka kama mafuta/ gesi na utalii

Mwisho wekeni mikakati kabambe ya jinsi gani mtahamasisha wananchi kupiga kura mwaka huu na pia wasiishie tu kupiga kura bali wazilinde kura zao. Wekeni mipango kabambe ya kukusanya matokeo yenu yote ya ngazi zote hasa uraisi na ubunge. Kura zipigwe kwa vingi, zilindwe, zihesabiwe kwa uwazi na kulindwa na mwisho matokeo yatangazwe kama yalivyohesabiwa.

Chadema lazima muamini kuwa Mungu yupo pamoja nanyi mwaka huu. Hawa jamaa (CCM ) wamejisahau sana na hawana nguvu saivi zaidi ya kutegemea vyombo vya dola.

Jiandaeni kuongoza nchi, Jiandaeni kuwa Chama tawala. Jipangeni.

Asanteni na usiku mwema!
 
Yani hayo uliyoyandika ndio ya kuitoa CCM madarakani mwaka huu?

Hujui kama chadema wanapolalia ndio CCM ilipoamkia?
 
Mitandao ya kijamii Ina nguvu Sana.Figisu zote zinazotaka kufanywa na CCM&Co dhidi ya upinzani zikiibuliwa kwenye Twitter& facebook na hata JF,MiCCM inaghairi.Kinachoendelea Pemba &Unguja sasa hivi wakaona bora kabisa wazime internet ili yasijulikane!
 
Back
Top Bottom