Karibu na uchaguzi tutasikia mengi wadanyika sisi, naibu waziri afufuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karibu na uchaguzi tutasikia mengi wadanyika sisi, naibu waziri afufuka

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kipa, Mar 26, 2009.

 1. k

  kipa Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Habel Chidawali,Dodoma ( MWANANCHI )
  NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Omari Yusufu Mzee amewajia juu watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kudai kuwa, baadhi yao ni wezi wakubwa, jambo linalolifanya taifa likose usingizi kwa ajili yao.

  Mzee alisema hayo jana katika ofisi za TRA, wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya fedha mjini hapa.

  Tofauti na alivyozoeleka Naibu waziri huyo kwa upole, jana alikuwa mkali mithili ya mbogo aliyejeruhiwa na kusisitiza kwamba dawa ya wazembe wa taasisi hiyo nyeti imekwishachemka, kinachosubiriwa kwa sasa ni kuipua na kuanza kutoa dozi.

  “Ndugu zangu michezo yenu hii michafu, mtatuua kabisa, acheni ,kama

  tunatoa mishahara mikubwa kuwapeni mnadhani kuwa tunawapeni kwa ajili ya kuangalia sura zenu, sivyo bali ni kutaka mfanye kazi kwa uaminifu na kufuata maadili, lakini sasa huu ni wizi mtupu mnaoufanya watu wa TRA," alisema na kuhoji "kwa nini msibadilike,”.

  Alisema kuwa umefika wakati kila mfanyakazi katika taasisi hiyo atapimwa uwezo wake mwenyewe na atakayebainika kuwa anashirikiana na wafanya biashara kuiibia serikali atatolewa kafara na kuwa mfano kwa wenzake.

  Aliwataka watumishi hao mkoani humu kukaa chonjo, na kuahidi kufika kuwakagua wafanyakazi hao sikuya Julai Mosi na kuwapatia mikakati mipya.

  Naibu waziri huyo alisema hakubaliani kabisa na watu wanaofanya kazi kwa mazoea na akawataka kubuni mbinu mpya za kazi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya walipa kodi kwa kila mtanzania mahali popote hata maeneo ya barabarani na vijiweni.

  Jambo lingine alilosisitiza Naibu Waziri huyo ni pamoja na watumishi hao kujenga mahusiano mazuri yasiyo ya kinafiki na walipa kodi ili waweze kulipa kodi kwa

  hiari yao wenyewe bila ya kusukumwa au kufuatwa na mtu mwingine .

  "Nimeambiwa hapa Dodoma hakuna uhusiano mzuri baina ya watumishi wa TRA na wafanyabiashara", alisema.  Awali, akitoa taarifa yake kwa Naibu Waziri huyo, Meneja wa mkoa wa TRA Lazaro Njarabi alisema katika lengo walilopewa kwa mkoa wa Dodoma

  hadi sasa wamekusanya kwa asilimia 97 na kwamba wanatarajia kuvuka lengo katika kipindi kilichobaki kumaliza mwaka.

  Njarabi alitaja lengo la makusanyo walilopewa na serikali kuwa ni Sh11.5 bilioni na hadi kufikia Februari mwaka huu walishakusanya Sh7.4 bilioni na kwamba wanaamini watavuka lengo kwa kukusanya sh. 200 milioni zaidi ya malengo.

  MWISHO.


  Bwana Mzee,
  unataka tuamini haya ndio umegundua sasa hivi, na hio dawa itaiva lini au ndio mapishi ya mawe? tusubiri yaive.
  kweli njii hiii imejaa wasaniii
   
 2. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani si anatoka visiwani huyu? Hivyo anafanya kampeni Dodoma badala ya KiembeSamaki waliko wapiga kura wake. Pengine anataka nafasi za upendeleo 2010.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nadhani alipata kifungua kinywa cha chai na pilipili ili kupandisha mzuka. hajasema madai ya msingi ya kiini cha uzembe wa wanaTRA. naona anafanya siasa za ushabiki wala hamna kitu nguvu za povu tu pale.
  angesema wanavyobambikiza watu kodi hasa ktk kuclear mizigo pamoja na mengine. Masikini waziri ameshindwa ktk rehearsal stages,
  Wizi mtupu
   
Loading...