Karibu Mara Mheshimiwa Adam Malima....

KidNinja

Member
May 26, 2017
27
15
Mh. Adam Kigoma Ali Malima kwa ukarimu wetu sisi wana MARA natumia wasaa huu na ukurasa huu kwanza kukukaribisha huku nyumbani kwetu KARIBU SANA.

Mheshimiwa mara ufikapo huku kwetu usisahau kununua PANGA, MKUKI, UPINDE NA MISHALE, RUNGU na SIME sio kwamba unaenda vitani bali ni kwasababu ndio jadi yetu pia usisahau kuchukua vikombe viwili kimoja kwa ajili ya kunywea uji na kingine cha kunywea togwa, pia ujiandae kula kichuri, nyama choma na kimoro, Mheshimiwa wala usisumbuke kuwaza kukosa zile samaki chumvi za kule kwenu pwani lahasha jiandae maana sasa unakuja kwenye samaki wenye heshima kubwa sana duniani kwani hata waizraeli na wamarekani hutuma ndege kila uchwao kuzichukua.

Mheshimiwa mshukuru mungu kwani umependelewa sana na mheshimiwa raisi kwa kukupeleka mkoa mzuri tena wenye suluhu za changamoto zake wenyewe zaidi ya yote Tanzania tena bila shaka duniani kote; Labda unaweza usilijue hilo naomba mimi nikuthibitishie kama ifuatavyo;
1. Mkoa huu una watu jasiri walio tayari muda wowote kupambana na chochote kiitwacho adui bila hata woga wowote, hivyo nakuomba uwatumie vizuri kupigana vyema na ujinga, maradhi na umaskini.

2. Mkoa huu una watu wachapakazi hatari kwani wako tayari hata kuchapa kazi katika mazingira yoyote yale iwe porini au hata majini, hivyo nakuomba utumie uchapakazi wao kutimiza kauli mbiu ya raisi ya HAPA KAZI TU.

3. Mheshimiwa mkuu wa mkoa nasema una bahati kwani umeletwa kwenye mkoa huu uliobarikiwa rasilimali na amali zinazosifika kimataifa, kumbuka mkoa huu umezungukwa na ziwa lenye upekee na utajiri adimu duniani kwa takribani halmashauri zake tano kati ya saba zimezungukwa na ziwa hili lililosheheni kila aina ya utajiri. Mkoa huu unamiliki mbuga kubwa yenye hadi ya kitaifa yenye kila aina ya wanyama na viumbe vya porini, unakuja katika mkoa ambao umejaa madini kibao karbia katika halmashauri zake lakini pia mkoa huu una chanzo cha gesi ambacho kimekosa tu uchimbaji. Mheshimiwa naendelea tu kukukumbusha kuwa unakuja katika mkoa wenye eneo kubwa na nyeti la kimpaka na majirani zetu wa kenya na uganda ambapo mipaka hiyo pia twaweza ipa hadhi ya rasilimali. Sio hapo tu unakuja katika mkoa umbao asilimia 98 ya mazingira yake yanakubali kulimika na kuzalisha kwa misimu zaidi ya mmoja kwa mwaka tena ardhi yenye rutuba. Unakuja katika mkoa ulisheheni wacha mungu kwani ndio maana wamisionari walipotia maguu 1903 hawakutaka kutoka.

4. Mh. kumbuka pia kuwa unakuja kwenye mkoa wenye uwekezaji na wenye vivutio vya utalii, ninachokuomba tumia uwezo wako wote ukimuomba na Mungu ili kwamba utumie vitu hivyo adimu duniani kuufanya mkoa uwe na uwiano na thamani ya vile vilivyopo, naamini kwa amali hizo mkoa wetu unao uwezo wa kuongoza tanzania kwa uzuri na kwa uchumi.

Tahadhari: Natambua kuwa mkoa wetu umekuwa na utambulisho hasi ambao bila shaka umejengwa na watu wenye hiana nasi kuwa ni mkoa ulijaa wakorofi lakini naomba nikwambie hilo sio la kweli bali watu hawa ni wakarimu sana,walinzi wa mali zao pia wasiopenda kuonewa na kunyaswa lakini pia hawana tabia ya kumumunya maneno, kuongelea chumbani au kwapani kwani ukiwakwaza hata ukileta vifaru vingapi hawata hofia kukupasulia ukweli wa mambo na hapo ndipo wasiojua huwachukulia kama wakorofi. Zaidi watu hawa wanapenda na kuthamini mila na desturi zao ikwa ni pamoja na kuzungumza lugha zao asili.

Taamali: Mkoa huu umesheheni wasomi wa kutosha tena wazuri na watu wengi wenye karama ya uongozi.

KARIBU TUIJENGE MARA YETU.

[HASHTAG]#RoryaFm[/HASHTAG]

2a9da0a26019a2b188cdcc5eb7271cae.jpg
 
SASA UNAINGIA MKOA WA MARA.....Huko kukutana na watu wenye mkono ama mguu mmoja ni jambo la kawaida..makovu ya mapanga usoni ni kama tatoo tu hakuna anaeshangaa.
 
Tarime, Rorya na Mara kwa ujumla si watu wa kuchezea kama pwani, hakuna mnyonge kwenye mambo ya haki.
 
Hakika umenena vyema kwa utambulisho makini japo jina lake linasawili majina ya baadhi ya makabila ya mkoa wa Mara kama vile malima, mahira, na mengine mengi hivyo hatopata shida kutamka majina ya asili
 
Mkuu umesahau watu wa Mara pia wanapenda kupika majungu kwahiyo Mkuu wa Mkoa awe na tahadhari hiyo malalamiko mengi atakayoyapokea afanyie uchunguzi sana kabla hajachukua hatua.
 
Adam ni Kiburi na anadharau za pesa. Ila karibuni amekuwa mpole kidogo, ila mtu anayejiamini sana na sio muoga.

Tabia ya kujiamini karithi kwa Baba yake

Alipanga kumkabili Bwana Mkubwa live kwenye Kikao kilichopita cha NEC yeye na Msomali wa Nzega wakaishia Lupango DODOMA
 
Ukabila wenu ni ujinga sasa nyie Tarime mna ujasiri gani? Na wahehe na wangoni watasema nini? Mmewahi pigana Vita nyie Tarime kama wangoni na wahehe, Au mnaleta kelele tu
 
Tabia ya kujiamini karithi kwa Baba yake

Alipanga kumkabili Bwana Mkubwa live kwenye Kikao kilichopita cha NEC yeye na Msomali wa Nzega wakaishia Lupango DODOMA
Nilishangaa sana kwa sababu sikuwahi kusikia akizungumza lolote. Halafu kama huyu ndio haeleweki maana hasemi kwenye press wala a tweet. Siku ile anatishiwa na mtutu alikuwa cool sana. Nadhani huu ukuu wa Mkoa mpakani huko ni moja ya njia ya kudhibitiwa kisiasa au unasemaje Mkuu
 
Nilishangaa sana kwa sababu sikuwahi kusikia akizungumza lolote. Halafu kama huyu ndio haeleweki maana hasemi kwenye press wala a tweet. Siku ile anatishiwa na mtutu alikuwa cool sana. Nadhani huu ukuu wa Mkoa mpakani huko ni moja ya njia ya kudhibitiwa kisiasa au unasemaje Mkuu

achana na system

'May be' Genge lilikuwa linaundwa hapa Mjini ndo linasambaratishwa

wengine wametupwa Balozini kurudi Nchini ni mpaka kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi

Adam apunguze kujiamini kwa siasa zetu hasa za utawala huu atapotea.

Namkumbuka yule RAS wa Mwanza aliepigana Kikaoni AKATIMULIWA, kilichomgharimu nae ni over confidence
 
Mheshimiwa mara ufikapo huku kwetu usisahau kununua PANGA, MKUKI, UPINDE NA MISHALE, RUNGU na SIME sio kwamba unaenda vitani bali ni kwasababu ndio jadi yetu pia usisahau kuchukua vikombe viwili kimoja kwa ajili ya kunywea uji na kingine cha kunywea togwa,
KARIBU TUIJENGE MARA YETU.

[HASHTAG]#RoryaFm[/HASHTAG]

2a9da0a26019a2b188cdcc5eb7271cae.jpg

Unacheza wewe, hivi unajua kama jamaa atakuja na ma - SMG.

Refer alivyoibiwa Morogoro.
 
Ukabila wenu ni ujinga sasa nyie Tarime mna ujasiri gani? Na wahehe na wangoni watasema nini? Mmewahi pigana Vita nyie Tarime kama wangoni na wahehe, Au mnaleta kelele tu
Ni bora hatà wamatumbi kidogo walipambana na mkoloni kuliko hao wa Mara
 
Back
Top Bottom