Karibu kwa fursa hii ya Pilipili Kichaa

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
Ni kuhusu kilimo biashara. Unapoamua kulima lazima akili ilenge faida. Hukuna tena kulima kwa kubahatisha au kufuata mkumbo. Kwa msingi huo, ndiyo maana Kampuni yetu ya Kinasoru East Africa (T) Ltd kwa kushirikiana na wadau wetu tukaja na kilimo cha mkataba kilimo ambacho mkulima unalima ukiwa na uhakika wa soko.

Dunia inahitaji chakula. Na sisi tukiwa sehemu ya Dunia tunawajibu wa kuchangia sehemu yetu katika kuilisha dunia. Na kwa bahati nzuri sana Tanzania tumejaliwa ardhi nzuri yenye rutuba tele, kuna mabonde na mito inayotiririsha maji kwa muda wa mwaka mzima inayoruhusu kuendesha shughuli za kilimo kwa kipindi chote cha mwaka. Pia kwa maeneo mengi ya nchi yetu yanapata mvua za kutosha zinazotoa fursa za uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa gharama nafuu. Ni muhimu tukaitumia fursa hii ambayo wenzetu kwenye nchi zao hawana.

Ni lazima tuamue kutengeneza pesa kupitia kilimo chenye soko la uhakika. Kilimo cha Mkataba. Ni kama ambavyo siku zote tumekuwa tukikinadi kwa wakulima, lengo letu hasa ni kuona mkulima ananufaika na kilimo chake.

Hatutaki kilimo cha kufukuza upepo. Tunataka tukutafutie kwanza soko kisha tukuambie ulime. Hadi sasa bado tuna fursa za Kilimo cha Mapapai, Viazi Lishe, Maboga Vibuyu, Maboga ya kawaida na Pilipili kichaa.

Na kwa muda mrefu tumekuwa tukiandika sana kuhusiana na fursa za viazi lishe, leo kwa mara nyingine , nimeona niwaletee maelezo ya fursa ya kilimo cha Pilipili. Na pilipili ninayoizungumzia hapa siyo pilipili nyingine, bali, ni pilipili kichaa, ni zile Pilipili ndogo ndogo zenye ukali kupita pilipili zote.

Piilipili kichaa zinatumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo viungo kwenye mboga, kutengenezea chachandu, dawa mahospitalini, Viuatilifu kwa ajili ya kuzuia wadudu mashambani na pia zinatumika kwa ajili ya kutengenezea gesi ya machozi kwa ajili ya kutawanya watu wakati wa maandamano au vurugu mbalimbali zinapojitokeza. Pilipili kichaa ni biashara kubwa Duniani ingawa watu wengi bado hawajalijui hili.

Kuna aina nyingi za Pilipili kichaa lakini small red ndiyo inayohitajika zaidi kwenye soko letu.

Zao hili hustawi zaidi kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kuanzia ukanda wa mwambao wa pwani, mashariki, kanda ya ziwa, kati na Nyunda za Kuu Kisuni. Pia hustawi zaidi kwenye eneo lenye mwinuko kuanzia Mita 1500 na kuendelea kutoka usawa wa bahari na huitaji mvua za wastani kati ya 600 - 1200mm. Mvua zikiwa nyingi husababisha mmea kupukutisha majani yake lakini mvua zikiwa chache sana husababisha udumavu katika ukuaji wa mmea husika. Aidha, ukosefu wa maji halikadhalika husababisha mmea uliyoanza kuweka maua kupukitisha maua yake na kufanya pilipili zishindwe kujitengeneza.

Uoteshaji wa pilipili huanzia kwenye kitalu kabla ya kuhamishia miche shambani. Na kwenye kitalu hutumia muda wa wiki tano hadi sita.

Miche itatakiwa ihamishwa kutoka kitaluni na kupelekwa shambani ikiwa na urefu wa sm 8 hadi 10 huku ikiwa imetengeneza majani angalau manne.

Upandaji kati ya shina na shina ni sm 45 na kati ya tuta na tuta ni sm 60. Ekari moja inapanda miche 10,000.

Kwa ajili ya kuongeza uzakishaji, mkulima unaweza kutumia samadi au DAP wakati wa kupanda na CAN kwa ajili ya kukuzia. Ingawa kwa kilimo chetu tunashauri zaidi itumike samadi badala ya mbolea ya madukani.

Toka kupandwa hadi kuanza kuvunwa, pilipili kichaa hutumia muda wa miezi 2½ hadi 3. Na kwa wiki unaweza kuvuna mara mbili hadi tatu.

Kwa kawaida Pilipili inayovunwa ni ile tu iliyoiva ambayo inakuwa imebadirika rangi yake kutoka kijani na kuwa nyekundu. Na shughuli ya uvunaji huendelea kwa muda miezi 3 hadi 4 kama unatumia kilimo cha mvua lakini kama unatumia kilimo cha umwagiliaji zao hili linakwenda miaka miwili hadi mitatu huku ukiendelea tu kuvuna. Kazi yako kubwa inakuwa ni kumwagilia tu.

Kwa matunzo mazuri, ekari moja inaweza kukupatia hadi tani sita za pilipili mbichi ambazo zikakaushwa zitakupa tani 3.5 hadi 4. Mvuno mmoja kwenye mche mmoja hutoa gram 150. Na ukizidisha kwa miche yote 10,000 ya shamba la ekari moja, kwa awamu moja utaweza kupata tani 1.5. Kwa wastani utakuwa na mivuno mikubwa minne kama utatumia kilimo cha mvua na kwa ekari moja utaweza kupata kiasi cha tani 6 za Pilipili mbichi ambazo zikikaushwa utapata tani 3.5 hadi 4.

Kimahesabu, unapozunguzia tani 4, maana yake unazungumzia kilogramu 4000 na kila Kilogramu moja ya Pilipili kichaa iliyokaushwa inanunuliwa kwa TZS 4000/=. Hapa kuna biashara ambayo ni hai.

Karibu kwa fursa hii ya Pilipili Kichaa.

Aman Ng'oma
Kinasoru East Africa (T) Ltd
Instagram: #kinasueatzltd
Facebook page: Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
+255767989713 au 0655038210
Msalato
Dodoma
 
Mpo Tayari nije na mwanasheria wangu Wakati wa kuingia mkataba na nyinyi
 
Amani tuambie MKATABA TUNAINGIA NA NANI,TULIME NA TUMUUUZIE? KUWA WAZI MASHAMBA TUNAYO
 
Nikifikiria kuhusu Matikiti, Mayai ya kware, mkojo wa sungura napata mashaka kidogo..

Ila bado mleta uzi unaweza kunitoa mashaka, ukanishawishi tukaingia mkataba wa kimaandishi kuhusu Soko lake yasije yakatokea ya kware
 
Shida bwana hizi fursa watu huwa wanageuzwa fursa wao! Huwa wanajazwa wakiingia biashara inaishia hapo. Tumeona kwenye mapapai, mara mayai ya kwale mara mitiki

Lakini sisemi na ya kwako ni hivyo!
Tuchangamkie fursa
 
Fursa ni sawa na miluzi ya wapiga debe, kila mmoja anakupigia kama hauna msimamo unaweza ukawa unazunguka kama feni.
 
sijui ni hali mbya?lakini watz tupo wepesi mno mno kuamini haya mambo.. haua makampuni ya kulima pilipili yapo kibao na hakuna alowah faidika nao.. unaishia kulia tu..lilikuepo jingine dodoma acha watu tulime zile eye bird..tuliwaona basi!
 
Kinasoru naomba utudadavulie Gharama kwa mwaka kwa ekari... na uzalishari kwa mwaka kwa ekari... Je tukioingia mktataba niko hapa songea je hiyo bei ni ya shambani au ya wapi(delivery point)
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom