Karibu kundini mwana mpotevu ila umekatwa mkia

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Umetumia uamuzi wa busara kurudi nyumbani. Kabla ya hapo umetusaidia kuwarejesha wabunge na madiwani wa upinzani tuliowapoteza kwa sababu yako.

Umetusaidia kudhoofisha washindani wetu kisiasa na hadi sasa hwajui nini cha kufanya baada ya kurejea kwako.

Kazi tuliyokutuma uliifanya kwa ufanisi mkubwa na waliobaki kule ulikotoka kimkakati wanaendelea kutupa ushirikiano mzuri.

Katika siasa kuna gharama zake. Ulienda kule kwa bahati mbaya sana umekatwa mkia. Kurudi kwako kundini kila mtu anakuona hata kama utakuwa mbali.

Nikushauri tu kuwa ile kiu yako ya kuwa Namba Moja Tanzania ipotezee. Kwansasa hakuna uwezekano tena. Imeshindikana 1995 na 2015 haitakuja kuwezekana milele

Karibu kundini japo umekatwa mkia
 
Karudi kupiga pesa na RA bila wao ccm haina fedha ya kampeni.KAGODA RICHMOND
Ccm kimejidhirisha kuwa bila ufisadi hakipo bila vyombo vya dola hakipo.
EL alikua kikwazo katika maamuzi magumu juu ya dhulma inayofanywa na ccm sasa hayupo tegemea mafanikio zaidi ya ukawa.

Huyu mzee ana TAMAA MBELE MAUTI NYUMA
 
Attachments

  • IMG_20190227_183644.jpeg
    IMG_20190227_183644.jpeg
    19.1 KB · Views: 52
Amekatwa mkia!! Ng’ombe karudi zizini lakini hana mkia! Duh kumbe kabla ya kurejea aliwatuma akina Millya, Dr Mollel, et al kumwandalia mapito!
 
Huyo kada wenu hakwenda kimkakati huko cdm. Tuseme tu ukweli, alikwenda huko baada ya kuahidiwa kupewa nafasi yake ya kugombea urais ambayo alinyimwa ktk hali ya kutatanisha kwenye ule mkutano wenu wa mchujo. Baada ya kugombea na kushindwa, akawa hana namna isipokua kurudi nyumbani kama mwana mpotevu.

Ukijumlisha na hali ya upepo wa urais 2020 kugeukia kwa Tundu Lissu, ndiyo kabisaa atabaki cdm kufanya nini?
 
Umetumia uamuzi wa busara kurudi nyumbani. Kabla ya hapo umetusaidia kuwarejesha wabunge na madiwani wa upinzani tuliowapoteza kwa sababu yako.

Umetusaidia kudhoofisha washindani wetu kisiasa na hadi sasa hwajui nini cha kufanya baada ya kurejea kwako.

Kazi tuliyokutuma uliifanya kwa ufanisi mkubwa na waliobaki kule ulikotoka kimkakati wanaendelea kutupa ushirikiano mzuri.

Katika siasa kuna gharama zake. Ulienda kule kwa bahati mbaya sana umekatwa mkia. Kurudi kwako kundini kila mtu anakuona hata kama utakuwa mbali.

Nikushauri tu kuwa ile kiu yako ya kuwa Namba Moja Tanzania ipotezee. Kwansasa hakuna uwezekano tena. Imeshindikana 1995 na 2015 haitakuja kuwezekana milele

Karibu kundini japo umekatwa mkia
WAKULIMA WA KOROSHO BADO HAWAJALIPWA NDIO KUSEMA WAMEPORWA? MCHANA KWEUPEE
 
Usijifanye hujui kilicho mkimbiza Chadema! Chama kinakuja na dhoruba mpya kabisa ambayo haijapata kuikumba ccm toka kuumbwa kwake. Ukiona mpaka haya mabadiliko ya leo barazani ujue ni mkakati wa kupambana na dhoruba hiyo.
Siasa itakapo rudishwa kuwa ya wazi ndio hapo ccm itakapojua imewakifu watu kiasi gani, mfano kule kusini ndio usiseme kabisa ccm itachakazwa kama mbwa mwizi.
 
Siasa za Tanzania zilikuwa zinamkosa mtu kama Lissu. He is reasonably aggressive kwa kutumia sheria. Alikuwa anamiss kitu kimoja tu ambacho sasa amekipata, international arena and recognition. I can't wait for 2020 election, Lissu hasiti kuwaambia watu waingie barabarani kudai haki zao. Na nina imani kubwa atachota 90% ya kura za Zanzibar kutokana na siasa zake za.Muungano. Na ndio maana tumeanza kuona team nyengine ishaanza kupanga safu yake mapeema starting from today!
 
Back
Top Bottom