KARIBU KOROMIJE KWA UTALII WA NDANI KUINUA MAPATO YA KIJIJI

Lukusi

Member
Dec 23, 2016
13
55
Mh Rais Umefanikiwa kukamilisha mradi wa Hosteli UDSM sasa weka msukumo kwa mbinu zilezile za kubana matumizi kukamilisha miradi ya ujenzi wa hospitali za rufaa za Mikoa....

Mh Rais Magufuli maamuzi yako magumu na ya busara yanahitajika kusaidia ukamilishaji wa Miradi ya Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Mara, Shinyanga, Singida na Manyara. Ujenzi wa Hospitali hizo mpya umeanza takribani miaka 9 iliyopita isipokuwa ya mkoa wa mara inazaidi ya Miaka 20. Ujenzi wa Majengo ya Hospitali hizo umesimama kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na kukosekana kwa fedha za miradi ya maendeleo hivyo kuyafanya majengo yaliyokuwa yanajengwa kuwa magofu na hivyo kuanza kuchakaa.

Naamini Serikali yako Mh Rais haishindwi kutenga Bajeti ya Bilioni 15 kwa kila Hospitali za Mikoa nilizozitaja ili ziweze kukamilika na kuanza kutumika na Mikoa husika. Wananchi wanashangaa sana kwanini miradi hii haikamiliki iliwaweze kupata huduma za kisasa katika hospitali hizo.

Nawashangaa viongozi wanaokuzunguka Mawaziri wa TAMISEMI na Wizara ya Afya kwanini wameshindwa kuandika andiko maalumu kwa ajili ya kukamilisha Hospitali hizo nakuleta kwako kwa ajili ya kuomba fedha ya kukamilisha miondombinu ya majengo na vifaa katika hospitali hizo, Mh Rais waulize Mawaziri wa OR TAMISEMI, Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha kama wana Action Plan yeyote ya kukamilisha majengo ya Hospitali hizo HOPE hawana na ndio maana wameshindwa kusaidia uwekezaji ulioanzishwa na Rais Mstaafu ndugu Kikwete.


Mh Rais naomba uwaite Ikulu Wakuu wa Mikoa ya Mara, Shinyanga, Singida na Manyara kwa ajili ya kujadili Ukamilishaji wa Miradi hiyo Mikubwa ya ujenzi wa Hospitali za Rufaa ya Mkoa ambao tayari ulishaanza zaidi ya miaka 9 ilikuweza kutoa maamuzi magumu na ya Busara kwa Afya za Watanzania

TAMISEMI, WIZARA YA AFYA NA WIZARA YA FEDHA AMKENI Majengo ya Hospitali Mpya yanageuka magofu Mpo tu mnamsuburi Mpaka Rais aseme


Mwisho Mh Rais unda Kikosi kazi kikiongozwa na TBA,TAMISEMI, WIZARA YA AFYA NA WIZARA YA FEDHA Kufanya Tathimini ya kina ya kukamilisha ujenzi wa hospitali hizo then fedha itolewe huu ni ushauri tu
 
Back
Top Bottom