Karibu Kinondoni Paul Makonda kwenye Ngome ya CHADEMA

Kwahiyo ndugu yangu OCD sasa ni kumpigia salute Makonda, aisee, politiki bana!
 
Jk maliza haraka uende bhana, umepoteza matumaini yote watanzania uliyotujengea mwaka 2005 wakati ukiingia madarakani, nimeamini nyerere alikuwa nabii. Kwa kuwateua wahuni kama kina makonda kuwa wakuu wa wilaya umeidhalilisha ikulu na ukuu wa wilaya wenyewe! Tafadhalini sana wana ccm tulizeni vichwa msije mkatuletea mtu kama huyu tena!
 
Kwani kinondoni kuna majimbo ya uchaguzi mangapi? Je kati ya hayo ccm ina mangapi? Na upinzani wana mangapi? Je kule kigogo fresh uchaguzi wa serikali za mitaa ulishafanyika?
 
Kwani wewe hujui kuwa ni jamaa furani ambalo halijitambui kazi yake kushiriki mipango miovu ya kuteka watu.
 
Kukurupuka kubaya,post imewekwa saa saba usiku sijui jamaa kaota ndoto mbaya kaamua ajipoze jf
 
Nimeona taarifa ya katibu wa CHADEMA wilaya ya kinondoni.Bwana KILEWO ni ya uongo tena ni aibu kiongozi kudanganya hadharani. Kwa kumkalibisha mkuu wa mpya wa wilaya ndugu MAKONDA kwa kumwambia kuwa kinondoni ni ngome ya chadema hili sio kweli,ukweli nikwamba.kuanzia tarehe 14 desemba 2014.baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa majimbo yote ya kinondoni yapo CCM. kwa wingi wa kura JIMBO LA ubungo CCM 39,215.=52.0% CHADEMA 23,091=30.6% JIMBO LA KAWE CCM 17,209=50.4% CHADEMA 12,092=35.4% JIMBO LA KINONDONI. CCM 22,531=49,6% CHADEMA 5,156=11.3% sasa hapa ngome ya chadema ipo wapi? Au bwana kilewo hajui maana ya ngome au alikuwa uchagani moshi hana matokeo?

watu wanaongoza kwa ujinga ccm unawajua?
 
Jk maliza haraka uende bhana, umepoteza matumaini yote watanzania uliyotujengea mwaka 2005 wakati ukiingia madarakani, nimeamini nyerere alikuwa nabii. Kwa kuwateua wahuni kama kina makonda kuwa wakuu wa wilaya umeidhalilisha ikulu na ukuu wa wilaya wenyewe! Tafadhalini sana wana ccm tulizeni vichwa msije mkatuletea mtu kama huyu tena!
Nyerere aliona mbali sana yaani anachofanya Kikwete ni kama mzaha, mbali ya tabia za Makonda Kinondoni is a center for international business, diplomats and residential embassies zipo kinondoni, kumteua mtu anayejulikana kwa ukorofi kuwa mwenyekiti wa ulinzi na amani wa wilaya unatarajia kitu gani kama sio kuandaa mazingira ya vurugu.

Lakini kinachonipa matumaini ni kuwa tumebakiza muda mchache tuondokane na kadhia yote hii JK hatakuwa na executive powers tena,

tumekula ng'ombe mzima kwa uchungu kwa nini tushindwe mkia uliobaki? tuvumilie.
 
Jamani simu zetu zitapona? Kama mtu aliweza kuiba bungeni mbele ya camera basi kinondoni tujiandae
 
Daah Mamlaka ya uteuzi imejitahidi... nilitegemea wamteue yule mshindi wa Big Brother!!

Atleast wametuletea mtu aliyempiga vibao waziri mkuu wa zamani na kipenzi cha wanyonge!

Wait a minute kwa hiyo jamaa ndio atakua mkuu wa wilaya ambayo pia anaishi waziri mkuu wa zamani ambaye alimpiga vibao!

cc Chabruma
 
Last edited by a moderator:
Wewe Kijana utulie huna ubavu wa kujibizana na Makomda!

Una kaa na kujidanganya eti Kinondoni hiko chini ya CHADEMA,mbona hamfanyi uteuzi wa wakuu wa wilaya?

nani ana ubavu wa kujibishana na Makonda ?? he is not even in my league, ni wale wa kupewa cheo kutokana na namna alivyochezesha domo lake ....a reward for dissing Lowasa and humiliating Mzee Warioba
 
Molemi hiki ndicho alichowahi andika Pr.Morgan " The image of an organisation"
Ccm huu ndio utamaduni,mila,miiko na maadoli ya chama.

- Makonda alimtukana warioba,Tundu Lissu,Lowassa,na kumpiga Warioba amepata cheo Dc
* Mwigullu alimtukana Mbowe,akatupa hotuba ya bajeti ya upinzani bungeni na akatengeneza video ya ugaidi na kusema chadema wamehusika akapata uwaziri wa fedha.

* kamuhanda aliwaongoza maaskari kule Iringa kumpiga na kumlipua bomu akapanda cheo.
Tunamsubiri hata aliyewapiga Mabomu wanafunzi kule Tunduma wakiandamana kugongwa kwa wenzao wawili na yule aliyepiga bomu Soweto Arusha wakati wa Kampeni za Chadema na yule aliyempiga Lipumba.

Aidha tunasubiri na Asha Bakari aliyemtukana matusi Jussa na kumwita ni Mhindi nae kabla ya uchaguzi wataukwaa u- kiongozi mkuu

Usisahau na ile ya Juma Nkamia kutukana ndani ya bunge kuwa HAONGEI NA MBWA ghafla akatunukiwa unaibu waziri. Kwa sasa amebaki Lusinde a.k.a Kibajaji sijui naye atatunukiwa nafasi gani kama heshima kwa matusi anayovurumisha ndani ya bunge.
 
Huyo kafanya dogo la kumpiga warioba, angefanikiwa kuuwa kama waliomuuwa mwangosi angepewa ubunge! Hiyo ndo ccm bwana
 
Usisahau na ile ya Juma Nkamia kutukana ndani ya bunge kuwa HAONGEI NA MBWA ghafla akatunukiwa unaibu waziri. Kwa sasa amebaki Lusinde a.k.a Kibajaji sijui naye atatunukiwa nafasi gani kama heshima kwa matusi anayovurumisha ndani ya bunge.

Mwigulu yeye alisuka dili la ugaid na kutukana chadema akapewa uwaziri
 
Back
Top Bottom