Karibu JF Mgeni. Naomba nikutambulishe kwa familia yetu

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
16,310
41,217
Sijajua umetumia idea gani kuchagua ID yako, Ila tambua unatumia ID fake, lakini uwepo wako humu ni real, na yale yote utakayo sema humu, yatakuwa yanawakilisha uhalisia wako. So behave well.

Mgeni, katika Uzi wowote utakao anzisha humu, wale watu watano mpaka kumi wa kwanza kuchangia ndio wataamua Uzi wako uende vipi. Wao wakionesha kusupport ulichoandika, basi 80% ya wachangiaji watakaofuta watakusupport. Ila ukiona hao watu wamekucrash, basi mkuu watakaofata wanaweza kukunanga hadi ukahisi wanabeef na wewe, ilhali hawakujui.

Mgeni, humu JF kuna wapwa na mabinamu. Hawa watu ni nadra Sana kukuta wameanzisha Uzi. Ila ukisha anzisha Uzi wako, wao watakuja kuendesha kikao Cha familia kwenye huo Uzi. Yawezekana ulikuwa unaomba ushauri kuhusu maumivu ya jino au mshipa wa ngiri, Ila wao watakuwa wanaulizana "Mpwa umepotea sana siku hizi" au "Binamu mbona hadimu Sana?". Kipindi wewe unahitaji ushauri, kuna wengine utasikia wanasema " Ngoja waje" au " Subiria Mwongozo" Nakushauri usiwe na jazba, wazoee tu.

Mgeni, wanaume wote wa humu wanajua mapenzi na hakuna mwenye kibamia. Wakiwa kwenye 6x6 wanatumia minimum dakika 30 mpaka 45 kumuandaa mwanamke, then ndio inafata shoo ya kibabe. Sasa wewe ukija humu ukatoa maelezo chini ya hapo, jiandae kupokea kebehi na kuambiwa huna nguvu za kiume .

Mgeni, pisi za humu zote ni kali na ziko well financially na hawaendeshwi na mapenzi. Sasa wewe ukija humu, epuka kusema umempiga mpenzi wako maana utanangwa sana. Watasema ww ni masikini, maana masikini ndio wanakuwaga na hasira hasira sababu ya ugumu wa maisha. Ukisema ujitetee, watabadili mada, watakwambia unakibamia, so nenda nao taratibu .

Mgeni, tunatumia ID fake Ila be humble. Kuna member ni watu wazima Sana ila wakiingia humu wanakuwa kama watoto. Unaweza amua kutoa ushauri ukidhani unaongea na dogo wa form 2, kumbe unaongea na mtu ambae akienda kwenye kikao ambacho Mzee wako yupo, Mzee wako ataachia kiti kwa heshima .

Mgeni, bado nakusisitizia kwenye humbleness. ID tunazotumia ni fake, Ila zinawakilisha uhalisia wetu. Ili jina ulilochagua kutumia humu, utalizoea tu kiasi kwamba ikitokea mtu nje na humu amekuita, unaitika vizuri tu as if ulibatizwa nalo. So usiwe fake Sana katika uongeayo au kuandika humu, kiasi kwamba siku unatatizo serious la kuhitaji ushauri, unalazimika kufungua account nyingine, maana official account yako inakusuta. Ukikaa Sana humu utajionea, Love Connect new ID inatafuta serious life partner, lakini ukicheki ule mwandiko ni kama wa member unayemjua kitambo tu, na mmekua mkikwaruana kwaruana miaka kadhaa jukwaani, sema huwa tunakausha, na wewe nakusisitizia ukishakuwa mwenyeji ukaushe.

Mgeni, humu watu tunamood tofauti tofauti kutegemeana na siku ilivyo. So, siku ambayo wewe upo stressed usilazimishe humu watu nao wawe stressed. Siku ukiwa na hudhuni, usitake members wote tuwe na hudhuni. Relax, know how to handle your stress. Maana usipokuwa makini utaongezewa stress.

Mgeni, wewe ndio umekuja, mengi huyajui. Ila humu Kuna kitu kinaitwa JF Get Together Party. Kwasasa hii party imekuwa dormant, ila nakuhikikishia, soon huko mbeleni itarudi. Sasa kwenye ile party, utaenda wewe kama wewe, fake ID itabaki kwenye servers za JF. Hapo ndo utakumbuka kwanini nimekuwa nakusisitizia swala la kuwa humble. Humu utajichetua behind ID fake, Ila pale utakuwa smart, well dressed, ila kwavile ndo mara ya kwanza tunakuona, ID yako ndo itakuelezea. Unaweza kosa connection kizembe, au kukosa future partner. Maana ID yako ndo itasema upoje upstairs. Utabadilishana contacts, then after party watu wanakuwa busy na threads zako, hapo ndo wanakufanyia assessment .

Mgeni, ukiangalia Sana comments za humu, michango ya wadau na maelezo yetu, unaweza ukahisi JF ni forum ya diasporas tu, au ni watu kutoka sayari ya Mars au Jupiter. Ila nikutoe tu wasi wasi mkuu, ili usipate stress, wale unaopishana nao sokoni, kwenye Dala Dala, kwa mama ntilie, vibanda umiza, kwa mtogole,Buza manzese n.k ndio sisi sisi. Vyanzo vya taarifa zetu ni google, Wala hatujasoma kiviiile, tusikushtue kwa namna tunavyoichambua Hypersonic ya Mrusi.

Mgeni, kwavile umejiunga nasi naomba ujiandae kusikia baadhi ya maneno yakisemwa mara kwa mara. Mfano "JF imepoteza uhalisia,utoto mwingi", "JF ya kitambo haikuwa hivi". Nakusisitizia Sana, ukiona mtu amesema hivyo, Wala usisumbuke kuangalia profile yake amejiunga lini, na hata ukiangalia usimshangae eti anaongelea JF ya kitambo ilhali kajiunga mwaka jana. Majibu yao ni simpo tu "Nilikua guest user miaka mingi Sana, mwaka jana ndo nikaona nijiunge"

Mgeni, Nina mengi sana ya kukwambia. Ila naomba nikomee hapa, mengine watakuja kuongezea wadau. Lakini yale ya ndaani kabisa utayajua kwavile umeshaamua kujiunga nasi.


Baharia wa Nchi Kavu, kwa moyo mkunjufu naomba kukwambia,

KARIBU

Analyse
 
Juzi natoka zangu kwa biden pale whitehouse kwa mbali nikamuona putin,akiwa anakuja pale kwa. Biden,tukapeana hai pale akaniomba kama buku sita hivi anywe chai sikuwa na hiyan nikazama . mfukon nikampa teni nilichogundua kumbe putin na biden ni wana sana
 
Juzi natoka zangu kwa biden pale whitehouse kwa mbali nikamuona putin,akiwa anakuja pale kwa. Biden,tukapeana hai pale akaniomba kama buku sita hivi anywe chai sikuwa na hiyan nikazama . mfukon nikampa teni nilichogundua kumbe putin na biden ni wana sana
Hahaha na we ni diaspora mkuu au ulienda tu kushangaa shangaa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom