Karibu JamiiForums Mhe. Rachel Mashishanga

Kama mtu kajiunga leo jf
tena na id yake ya kweli

tunapaswa kumkaribisha na kusubiri michango yake
sio kuanza leo leo 'kumponda'
wakati ndo kwanza anajiunga
Nilijua hiki kitatokea!wacha wapumue kaka,I guess humu ndo mahala pake! Kiongozi usiposemwa uongozi wako utakuwa wa mashaka
sasa tutafanya wengine waogope kujiunga

Waache wapumue kwani wanatambua uwepo wangu!Nililijua hili hivyo inawezekana ndo pa kupimulia humu!Kiongozi usiposemwa uongozi wako una mashaka!
 
Waache wapumue kwani wanatambua uwepo wangu!Nililijua hili hivyo inawezekana ndo pa kupimulia humu!Kiongozi usiposemwa uongozi wako una mashaka!
Safi sana Kamanda, kusifiwa kuna pumbaza, kunalewesha na kuna ondoa uwajibikaji maana msifiwa kila anachofanya atataka asifiwe, asiposifiwa hana la kufanya. Karibu sana, huu si muda wa kusifiwa ama kutafuta sifa bali kuwajibika zaidi kuelekea ukombozi wa kweli wa Mtanzania. Pamoja tutaweza, unaposemwa ma kukosolewa jua unatakiwa mema na kuelekezwa kwenye mafanikio!
 
Niwashukuru walionikaribisha sebuleni, great thinkers itakuwa nyumbani tu,niwe fyekeo,jembe,panga nitabaki kuwa Rachel Mashishanga,na nitaendelea kusimamia ninachokiamini,na kuwasimamia wanaoniamini!
Ukiwa Kiongozi tegemea kupuuzwa,kudharauliwa,Kukejeliwa na kupongezwa,ukijatambua maisha yatasonga mbele!

Kuna mtu kakupuuza mama? Karibu jamvini angalia hoja na mambo ya maana tu ukitaka kufuatilia kila kitu hapa mama utakasirika kuliona jukwaa chungu. skip nonesense na majungu kwa sababu lazima utakutana nayo
 
Safi sana Kamanda, kusifiwa kuna pumbaza, kunalewesha na kuna ondoa uwajibikaji maana msifiwa kila anachofanya atataka asifiwe, asiposifiwa hana la kufanya. Karibu sana, huu si muda wa kusifiwa ama kutafuta sifa bali kuwajibika zaidi kuelekea ukombozi wa kweli wa Mtanzania. Pamoja tutaweza, unaposemwa ma kukosolewa jua unatakiwa mema na kuelekezwa kwenye mafanikio!

Nimekaribia kamanda,niko tayari kwa yote,mwenye matusi haya,mwenye kinibeza haya,mwenye kunitia moyo Kama wewe hay a,nawakaribisha wote kwa ujumla wao
 
Karibu sana mbunge wetu hapa JF. Mimi nina swali au angalizo kidogo. Hivi ni kweli ndani ya Chadema kuna makundi? Kama ni kweli ninyi kama viongozi hamuoni kuwa kuwa na makundi kuna hatari ya kututumbukiza katika matatizo yanayoikumba CCM sasa hivi? Na kama kweli kuna makundi, ni kwa nini tuwe na makundi? Kwa nini tusiangalie na kujikita zaidi katika lengo la kile wazungu wanaita "the big prize" ambao ni ukombozi wa Mtanzania kutoka ufisadi wa CCM badala ya kuangalia zaidi personalities? Mimi naunga mkono Chadema, lakini nisingependa kuona tunatumbukia kwenye siasa za UCCM ndani ya chama chetu. Ni hayo tu mheshimiwa.
 
Kuna mtu kakupuuza mama? Karibu jamvini angalia hoja na mambo ya maana tu ukitaka kufuatilia kila kitu hapa mama utakasirika kuliona jukwaa chungu. skip nonesense na majungu kwa sababu lazima utakutana nayo
Mimi ndio nimempuuza kama ana akili kuanzia leo asimame kwa miguu yake miwili na sio ule usaliti alioufanya kwa kushikwa masikio na Zitto Kabwe wakati wa Walk out Move Bungeni. were watching this Guys very serious.
 
Mama Karibu jf ila hapa unatakiwa kuficha mapungufu yako kwa kujilinda kwa kutoropoka Kama wengine....kumbuka kujenga jina unaweza kuku cost century ila kuharibu jina una ku cost minute. Take care
 
Karibu sana kamanda. Kwa keeling tunahotaji viongozi wenye uthubutu Kama wewe!
 
Karibu sana dada ,jisikie uko nyumbani,
sipati picha 2015,magamba watatafutana
 
Karibu Rachel, wengine wetu si wanachama wa Chadema lakini, kama kwa kuupinga ufisadi tunajikuta tunapingana na CCM, basi tuhuma za kuwa manazi wa Chadema tunazipokea kwa mikono miwili. Wasichokijua hao vipofu wanaotuita hivyo ni kuwa kwa kuamini hivyo ndivyo wanavyozidi kuipaka matope CCM na kuihusisha na ufisadi...kwamba ukiuchukia ufisadi basi wewe moja kwa moja ni Chadema! Matokeo yake ni kwamba hata hili jamvi la JF wakati mwingi wanajaribu kulihusisha na Chadema kwa sababu tu wengi wetu hatupendi CCM inakolipeleka taifa letu! Karibu Rachel, tuungane pamoja katika kulikomboa taifa kutoka mikononi mwa hili genge la walafi, waongo, wezi na wauaji, CCM.
 
Nimekaribia kamanda,niko tayari kwa yote,mwenye matusi haya,mwenye kinibeza haya,mwenye kunitia moyo Kama wewe hay a,nawakaribisha wote kwa ujumla wao

karibu sana sister katika jamvi letu ambalo tunategemea mabadiliko makubwa kwa maisha ya baadae ya mtanzania wakati ni huu kumukomboa mtanzania tunaitaji uwepo wako ndani ya Jf kuna mambo mengi magumu na mepesi cha msingi tu ni uvumilivu wa hali ya juu vumilia katika yote ili mwisho wa siku tuseme tumeshinda pamoja.
 
Mimi ndio nimempuuza kama ana akili kuanzia leo asimame kwa miguu yake miwili na sio ule usaliti alioufanya kwa kushikwa masikio na Zitto Kabwe wakati wa Walk out Move Bungeni. were watching this Guys very serious.

Mmh basi ngoja nipite maana @by the way ni maoni yako.
 
Back
Top Bottom