Karibu 47% ya wabunge kuwa si wawakilishi wa wananchi!

Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
71,255
105,368
Bunge la Tanzania limegawanyika hivi

From http://www.parliament.go.tz/bunge/aboutus.php?cat=2&subcat=4

1. Members elected from the same number of constituencies. 232
2. Special seats women members. 75
3. Members elected by the Zanzibar House of Representatives. 5
4. Attorney General. 1
5. Members appointed by the President. 10
Grand Total . 323

Mpaka hapo wawakilishi wa wananchi moja kwa moja ni 232, wengine ni 91.

Tukichukulia baraza la mawaziri kama la sasa lenye wabunge takriban 60 wanaoenda kuwa mawaziri na naibu mawaziri, tutakuta namba ya wabunge wasiowakilisha wananchi inashuka kutoka 232 kwenda mpaka 232- 60 = 172 wakati ile ya wasiowakilisha wananchi inapanda kutoka 91 mpaka 91 + 60 =151

151/323 ~ 47%

Habari ndiyo hiyo.
 
Ni kweli kwa sababu kuna wabunge ambao kimsingi wankuwa wawakilishi wa mafisadi kwani kama mtu kwenye hoja za msingi hachangii anasubiri muda wa kupitisha ndo anasema NDIYO ya kuunga mkono.

Ila safari hii tumewapunguza kwakiasi kikubwa sana tuzidi kuwapunguza na tuzidi kuiunga chadema mkono.
 
mimi nitarudia kusema kuwa viti maalum kwa wanawake ni ubadhirifu wa fedha za umma.

wanawake hao hatujawachagua, na hatuoni faida ya wanawake hao kuwepo bungeni kwa kisingizio cha jinsia tu..
 
mimi nitarudia kusema kuwa viti maalum kwa wanawake ni ubadhirifu wa fedha za umma.

wanawake hao hatujawachagua, na hatuoni faida ya wanawake hao kuwepo bungeni kwa kisingizio cha jinsia tu..

Mimi nitaongeza kusema viti maalum vyote viondolewe, halafu mawaziri wasiwe wabunge.

Wananchi wakimchagua mbunge maana yake wanataka mbunge huyu awatetee bungeni, serikali ikimteua mbunge huyu huyu awe waziri au naibu waziri maana yake wanamtoa mbunge huyu katika kutetea wananchi na kumuweka katika timu ya serikali. Mbunge akiwa waziri hawezi kusimamia interests za wananchi inavyotakiwa kwani anafungwa na principles za "collective responsibility" za serikali.

Tuondoe viti maalum vyote, wabunge wawe ni wale wa kuchaguliwa na wananchi tu. Kisha kati ya hao wasiteuliwe mawaziri, mawaziri watoke nje ya bunge, hususan miongoni mwa watendaji waandamizi wa serikali.
 
na asilimia kubwa ya hawa wadada wanateuliwa kutokana na interest za mteuaji belive mo or not
 
na asilimia kubwa ya hawa wadada wanateuliwa kutokana na interest za mteuaji belive mo or not
hivi haiwezekani wakawa wanachaguana wanawake wenyewe kwa kila mkoa muwakilishi mmoja???? au sielewi jamani hv viti vya wanawake!????
 
mimi nitarudia kusema kuwa viti maalum kwa wanawake ni ubadhirifu wa fedha za umma.

wanawake hao hatujawachagua, na hatuoni faida ya wanawake hao kuwepo bungeni kwa kisingizio cha jinsia tu..

Tuko pamoja Gaijin mkuu viti maalum yafaa vifutwe mara moja vimechomekwa kwaajili ya kuwafurahisha nchi wahisani havina faida kwa mlipa kodi.

Hivi viti kumi vya rais wa JMT ni ugandamizaji wa hali ya juu wa demokrasia,fikiria watu zaidi ya laki moja wanamchagua mbunge mmoja iweje mtu mmoja achague wabunge kumi?.
 
umesahau kundi lingine la wabunge hao ni wale wabunge wa makame, kiravu, wasimamizi wa uchaguzi na polisi
 
Ubunge bongo ni sawa na kuula..hata useme sense kiasi gani hamna atakayekusikiza..ndio maana wabunge wanapongezwa, hii ni kuashiria kwamba sasa wameuaga umaskini.

IMO, concept yenyewe tu ya ubunge kichwani mwangu haimeki sense..yes ni wawakilishi wa wananchi kinadharia, lakini huwa wanapata inputs based on what? how do they collect voice of their masses kuhusu topics mbalimbali? je,kuna mwakilishi bora kuliko aliyesomea fani husika aliyepo kule jimboni (au halmashauri) full time ? anawezaje kuwa mwakilishi wa wananchi wakati yupo loyal kwa chama chake zaidi na akileta mbinde tu anaweza kufutwa uanachama na kuishia kutemeshwa mkate wake? etc etc
 
Wabunge Wa majimboni walau unaweza kusema watafungua ofisi zao majimboni kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi, hawa wa viti maalum wapatap Mia moja wanafanya kazi zao vipi?

Suala hili hata vyama vya upinzani haviwezi kuzungumzia kwa kuwa linahusu ruzuku ya chama na kurudisha fadhila kwa wafadhili na vigogo wa chama
 
mimi nitaongeza kusema viti maalum vyote viondolewe, halafu mawaziri wasiwe wabunge.

Wananchi wakimchagua mbunge maana yake wanataka mbunge huyu awatetee bungeni, serikali ikimteua mbunge huyu huyu awe waziri au naibu waziri maana yake wanamtoa mbunge huyu katika kutetea wananchi na kumuweka katika timu ya serikali. Mbunge akiwa waziri hawezi kusimamia interests za wananchi inavyotakiwa kwani anafungwa na principles za "collective responsibility" za serikali.

Tuondoe viti maalum vyote, wabunge wawe ni wale wa kuchaguliwa na wananchi tu. Kisha kati ya hao wasiteuliwe mawaziri, mawaziri watoke nje ya bunge, hususan miongoni mwa watendaji waandamizi wa serikali.

viti maalum visingekuwepo huyo mdee angeanzia wapi?
 
viti maalum visingekuwepo huyo mdee angeanzia wapi?

Viti maalum visingekuwepo chances are huyo goigoi Kikwete asingekuwepo alipo, maana kaingia bungeni mara ya kwanza kwa viti maalum.

Hapendwi mtu hapa, ni maswala tu yanaongewa. Kwa nini unafikiri mtu anayekataa viti maalum ni CHADEMA na mfurukutwa wa Mdee ?
 
Bunge la Tanzania limegawanyika hivi

From Parliament of Tanzania

1. Members elected from the same number of constituencies. 232
2. Special seats women members. 75
3. Members elected by the Zanzibar House of Representatives. 5
4. Attorney General. 1
5. Members appointed by the President. 10
Grand Total . 323

Mpaka hapo wawakilishi wa wananchi moja kwa moja ni 232, wengine ni 91.

Tukichukulia baraza la mawaziri kama la sasa lenye wabunge takriban 60 wanaoenda kuwa mawaziri na naibu mawaziri, tutakuta namba ya wabunge wasiowakilisha wananchi inashuka kutoka 232 kwenda mpaka 232- 60 = 172 wakati ile ya wasiowakilisha wananchi inapanda kutoka 91 mpaka 91 + 60 =151

151/323 ~ 47%

Habari ndiyo hiyo.
kuna kajiukweli kidogo, lakini siyo lazima mawaziri watokane na wabunge wa kuchaguliwa tu, can come from anywhere, viti maalum, presdential apointees etc. so umenifehemu
 
Ugali bila mboga hauwezi kunoga. Sasa lazima ugali ukipikwa na mboga iwepo pembeni japo samaki mkavu.
 
sawa kabisa mkuu kiranga!!!
lakini kumbuka kati ya hao 172 wengine ni wastaafu wa utumishi wa umma wanaosubiri kuzikwa kwa fedha za walipa kodi ambao aghalabu hulala wakati wa vikao ( kwa maslahi yao binafsi) na wakati wa kupitisha (mfano bajeti) unapofika ndio hao wanaosikika, ndioooooo!

kiukweli hiyo 151 huongezeka kwa mtindo huo na kuwa zaidi ya 47%
 
huu ni ubadhirifu wa rasilimali usio na sababu , hamna cha viti maalum wala viti vya wageni waalikwa . siku hizi si mambo ya haki sawa ? na wao waende juani wakaombe kura kama wenzao wanavyofanya . wanatunyonya hawa wanawake kwanza wengi wao wanapata hizo nafasi katika mazingira ya gizani ( hayaeleweki).
 
Back
Top Bottom