Kariakoo: Polisi wafanikiwa kuwaua majambazi wanne baada ya majibizano ya risasi

kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,694
2,131
Nimeona kuna taarifa zinasambaa huko Instagram kwamba kuna majambazi yalitaka kupora ktk mtaa wa Livingston Kariakoo bahati mzuri polisi wamewahi ktk eneo la tukio. Taarifa zinasema kulikuwa na majibizano ya risasi. Na kunaonekana picha za watu wakiwa wamepigwa risasi wapo chini kama watatu hivi.

Je, Kuna mtu anayejua lolote aje atutosheleze hapa?

---Updates---
Maeneo ya kwa Bakhresa Kariakoo usiku huu wameuawa majambazi wanne mtaa wa Livingstone na Aggrey karibu na mtaa wa Lumumba Mnazi Mmoja. Kuna mama mwenye mimba ambaye alienda kununua mikate kapigwa risasi mbili.

Tukio limetokea mida ya saa nne kasoro usiku huu.


57c93a63373eb12ceeabfeef83cd7071.jpg
2793a0407e589ed17c11754c542bf547.jpg
c3850957c8bf3f0353fe109986d9be0a.jpg
 
Kweli kuna tukio la ujambazi ambalo halikufanikiwa na majambazi watatu wa kiume na mwanamke mmoja wameuwawa katika majibizano ya kurushiana risasi na Polisi. Tukio hilo limetokea Mtaa wa livingstone na Aggrey kwenye duka maarufu kwa Bakhresa usiku huu wa leo majira ya saa mbili plus. Picha zitafuata baadae zilizopo si nzuri kuziweka hapa.
 
Wa ndg nimeona kunataarifa zinasambaa huko Instagram kwamba kuna majambazi yalitaka kupora ktk mtaa wa Livingston kariakoo bahati mzuri polisi wamewahi ktk eneo la tukio, na taarifa zinasema kulikua na majibizano ya risasi. Na kunaonekana picha za watu wakiwa wamepigwa risasi wapo chini km watatu, hivi. Je Kuna mtu anaejua lolote aje atutosheleze hapa?

Kama wameshaanza hadi kuvamia ' Kariakoo ' basi bila shaka hawapo mbali sana ' kuvamia ' Magogoni kwa ' Taita ' mwenyewe.
 
Asee hata mimi nimeziona hizo picha.
Wenye taarifa zaidi waje hapa kutuhakikishia.
 
Kweli kuna tukio la ujambazi ambalo halikufanikiwa na majambazi watatu wa kiume na mwanamke mmoja wameuwawa katika majibizano ya kurushiana risasi na Polisi. Tukio hilo limetokea Mtaa wa livingstone na Aggrey kwenye duka maarufu kwa Bakhresa usiku huu wa leo majira ya saa mbili plus. Picha zitafuata baadae zilizopo si nzuri kuziweka hapa.

Weka tu Mkuu ili tuweze kuwatambua Ndugu zetu ' Majambazi '.
 
Kadri ugumu wa maisha unavyoongezeka,watu nao wanazidi kuwa majasiri kukabiliana na ugumu huo wa maisha uliopo.
 
Back
Top Bottom