Kariakoo na Dar es Salaam: Wanahistoria tendeeni haki Historia za majina hayo

Mkwawa, Kinjikitile, Isike, Mangungo, Mamangi wa kichaga, na wengine wengi katika sehemu kubwa iliyokuja kuwa Tanganyika hawakuwahi kuguswa na dini iliyoletwa na majahazi kutoka uarabuni.
Tanganyika na kabla ya hapo ilikuwa ni utawala wa Waislam ndio maana leo unaabudu kwa uhuru, upendacho. Jiulize ungeanza kwa utawala usio wa Kiislam ungekuawaje.-?

Hivi Hamuelewi kuwa Wazungu ndio walioleta Ukristo? Walipokuja walikuta tayari tawala zipo na zilikuwa za Waislam na wakakaribishwa.

Ni kipi kigumu kukifahamu hapo? Au historia unayosomesshwa uliambiwa Tanganyika na kabla ya kuitwa Tanganyika utawala ulikuwa wa nani? Msome Ibn Batuta aliekuja hapa kabla ya wengi na aliandika alichokikuta alikuta, alikuta nini na ilikuwa ni mwaka upi?
 
Naona mjadala huu umewaacha vinywa wazi wengi.

Hakuna ubishi kwenye niliyowaletea. Eti Kariakoo ni "carrier corps"! Khaaa! hata haileti maana yoyote.

Kariakoo ni Kiarabu. Mji au Kijiji cha wote (Karia kuulu).
 
Tafiti ndogo tu, yangu binafsi na isiyo na shaka kabisa niliyoifanya kuhusu jina la jiji letu kuu "Dar Es Salaam" na jina la soko letu kuu "Kariakoo" ninaihitimisha kwa ufupi (summary) hapa chini kwa kusema wanahistoria hususan wa hapa Tanzania hawayatendei haki hayo majina kwa kutuaminisha maana ya majina hayo isiyo halisi na isyo ya kweli.

Dar Es Salaam

Kila ninapokutana na maan ya jina Dar Es Salaam naona makosa ya wazi kabisa au ya wanaotoa maana kutokufanya tafiti japo kidogo au kuwaamini sana wanahistoria ambao au wao kuwaamini waliowafundisha au waliyoyasoma bila kuyanyia tafiti na kuiamini tu maana inayotolewa. Au ni makusudi inafanyika ili kuifuta maana hali ya jina hilo na lilipoanzia kihistoria.

Mara nyingi, kama si zote, tumeaminishwa kuwa maana ya neno Dar Es Salaa ni "bandari ya Salama", na wanatuaminisha kuwa historia yake ni Waarabu waliotoa jina hilo kutokana na kuwepo bandari hapo Dar Es Salaam. Huo tunaoaminishwa sio ukweli.

Ukweli ni kuwa neno Bandari halimaanishi bandari kwa Kiarabu bali neno Bandar ni neno la Kiajemi (Persia) linalomaanisha bandari. Na ipo miji maarufu ya Kiajemi (Persia) yenye jina hilo.

Jina Dar Es Salaam halina neno "Bandar" la Persia au Kiarabu hata maana yake iwe ni "Bandari". Jina hilo lina neno la Kiarabu"Dar" linalomaanisha Nyumba au "dari" kwa maana "haven". Kwa akirefu chake ni Dar Es Salaam ni Nyumba ya Amani au vile vile Dar Es Salaam ni "haven of Peace". Ambayo ni maana halisi ya jina la lililokuja kuwa jiji letu pendwa.

Neno Dar Es Salaam linatokana na neno la Kiarabu fasaha "Dar Us Salaam" linalopatikana ndani ya Qur'an Tukufu, utalipata katika sura ya 10 aya ya 25 na sura ya 6 aya ya 127 likimaanisha jina la pepo (Abode or Haven of Peace).

Kwa maana hizo, jina la jiji letu la Dar Es Salaam lilianzia kilipojengwa chuo cha kwanza cha Kiislam (Madrassa) hapo ilipo sasa Ikulu ya Dar na jengo hilo la la chuo hicho ndio likaitwa Dar Us Salaam (Nyumba ya amani) na ilipo Hospitali ya Ocean Road ndipo palikuwa mabweni ya chuo hicho.


Mjerumani ndiye akja kukifanya chuo hicho kuwa nyumba ya gavana baada ya kukitengeneza upya lakini aliacha mjengo ule ule wa asili kwa kiwango kikubwa. Athari za majengo ya Kiarabu na Kiislaam kwenye Ikulu yetu ipo mpaka leo. Haipingiki kwa aijuae Ikulu hiyo.:-
Unanifurahisha sana, kweli una akili za kimadrassa..eti "athari za majengo ya kiarabu na kiislamu kwenye ikulu yetu ipo mpaka leo" Uarabu na uislamu unahusiana vipi? Kwani hakuna nchi za kiarabu lakin sio za kiislamu?Uarabu mi utaifa na uislamu ni dini, inakuaje uvioanishe? Ni kitu gani unaweza kutuonyesha Cha kiislamu ambacho kipo ikulu kuthibitisha madai yako?
 
Usijaribu kulazimisha kuinasibisha historia adhimu ya nchi hii na dini yako kilo mara.
Hilo hutoweza kuliepuka hata chembe. Unataka uinasibishe na dini ipi? Ukipenda usipande ndio unalo hilo.

Nini maana ya neno na jina Dar Es Salaam, na linatokea wapi?

Usije kwa kuhororoja, uje na ushahidi kama niliouweka mimi hapo post # 1.
 
Tafsiri yako ya "Kariakoo" sio tafsiri rasmi hivyo haiwezi kuwa sahihi kwa namna yeyote

Aidha umeshindwa kuweka vyanzo vya tafsiri yako ili uthibitishe usahihi ulichoandika na pia uthibitishe kuwa tafsiri ya sasa siyo sahihi


Inaweza kuwa sahihi kwa wale wanaoamini hivyo ili kuwafurahisha tu
Ni sahihi kwa Waislam na wengine wasio na elimu na waliozoea kuburuzwa tu na wao wanaburuzika.

Huyu ni MWONGO na MZUSHI kama tu alivyo Mohamed Said anavyoletaga uzushi kuhusu historia ya Tanzania

Ikulu ilijengwa na Wajerumani.

Kariakoo asili yake ni kiingereza kama inavyofahamika wala si kiarabu

Wanatapatapa ili nao waonekane

Kunguni wahed
 
Dar es salaam hujulikana kama "Heaven of Peace" hiyo inajulikana sana na imeandikwa sehemu nyingi mno.

Bandar means port, port city or city by the sea kwa kiarabu; Hata mji ulio pembeni ya bahari huitwa Bandar lexchangeably kwa sababu miji mingi iliyo pembeni mwa bahari hutokana na bandari. Kwa hiyo siyo kosa kuita huu mji bandari ya salama.

"Carrier Corps" ni kikosi maalum cha wabeba mizigo wa KAR na hata Nairobi kuna kariakor, Dar es salaam pia kutokana na makaazi au kambi za vikosi hivyo. Babu yangu mzaa upande wa baba yangu alikuwa KAR na alipewa space mtaa wa Muheza waliporudi kutoka Sri Lanka (mwenyewe alipaita Ceylon) na alikuwa karibu na kea wenzake wengi.
Kikosi hiki kilikuwepo hata kenya. Kariakoo jina limetokana na waingereza.
Umeandika UKWELI Mkuu, hii mada iliyoletwa imejaa uongo na uzushi mtupu, yaani haina chanzo rasmi cha utafiti wala Mantiki

Wallah Wabillah
 
Huo mji kiasili ni MZIZIMA nadhani ungepambana jina hilo lirudi sio kufafanu majina ya kikoloni
 
Ni sahihi kwa Waislam na wengine wasio na elimu na waliozoea kuburuzwa tu na wao wanaburuzika.

Huyu ni MWONGO na MZUSHI kama tu alivyo Mohamed Said anavyoletaga uzushi kuhusu historia ya Tanzania

Ikulu ilijengwa na Wajerumani.

Kariakoo asili yake ni kiingereza kama inavyofahamika wala si kiarabu

Wanatapatapa ili nao waonekane

Kunguni wahed
Utafiti hupingwa na utafiti sio kuhororoja na kubwabwaja kama ufanyavyo.

Ulisomeshwa na kujazwa ujinga kuwa Kariakoo ilianza na Mwingereza. Licha ya Mwingereza, hata Mjerumani kaikuta Karia kuu.

Kwenu wapi wewe, au ndio katika wale wasio na asili?
 
Huo mji kiasili ni MZIZIMA nadhani ungepambana jina hilo lirudi sio kufafanu majina ya kikoloni
Hapana. Mzizima ni ilipo sasa Kisutu (Wakuja sikuhizi mnapaita Posta) mpaka bandarini na Ikulu na Upanga Mashariki yote mpaka Ikulu. Ukifika Salendaar Bridge kiasili, unapopita mto Msimbazi wote, pakiitwa Maji Mshindo.

Karia kuu kulikuwa na kijiji kikubwa au / mji mkubwa tayari hata Mjerumani kapakuta mpaka anakuja Muingereza kapakuta, Kikiitwa Karia Kuu, jina ambalo limebaki hadi leo hii. Matamshi tu yamebadilika, Karia Koo.
 
Kumbe hata Biden anaweza kuwa mwarabu!
Ikiwa Malkia wa Uingereza ana asili ya Uarabu itakuwa Biden? Tena jina Biden lina "sound" Kiarabu zaidi.

Ushahidi:

Kulingana na matokeo yao, ukoo wa damu wa Elizabeth II hupitia Earl ya Cambridge katika karne ya 14, kuvuka Uhispania Waislamu wa zamani, hadi Fatima, binti ya Nabii.

Ingawa ilibishaniwa na wanahistoria wengine, rekodi za nasaba za Uhispania za zamani za kati pia zinaunga mkono madai hayo na pia imethibitishwa na Ali Gomaa, mufti mkuu wa zamani wa Misri.

Mkurugenzi wa uchapishaji wa Burke aliandikia Waziri Mkuu wa wakati huo Margaret Thatcher mnamo 1986 akitaka kuongezwa usalama kwa familia ya kifalme.


Chanzo: Historians believe Queen is related to Prophet Muhammad
 
Mkwawa, Kinjikitile, Isike, Mangungo, Mamangi wa kichaga, na wengine wengi katika sehemu kubwa iliyokuja kuwa Tanganyika hawakuwahi kuguswa na dini iliyoletwa na majahazi kutoka uarabuni.
Hapo ndipo usipopaelwa.

Hao wote walijuwa Uislam kabla ya Ukristo.

Uislam haujaletwa bara hili na majahazi. Yesu mwenyewe alikuwa Mwafrika, nae ni Muislam.

Turudi kwenye mada, jina "Kariako" halikutokana na maneno ya Kiingereza kama tunavyodanganywa na kuuona ndio ukweli na sasa tunajidanganya wewnyewe. Neno Kariakoo ni neno la Kiarabu "Qariah" na neno la Kibantu "kuu", likimaanisha, kwa tafsiri nyepesi, kijiji kikuu. Neno "Qariah" kwa Kiarabu hutumika kama, mji au kijiji, inategemea na sentensi. Neno "kuu" nalo unataka tafsiri yake?

Qariah kuu = Kariakoo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom