Kariakoo: Gorofa inawaka moto, chanzo hakijajulikana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Habari,

Kuna gorofa inawaka moto muda huu mtaa wa Livingstone na Mkunguni, zima moto wameshafika wanaendelea kuzima.

Imewachukua saa mbili kikosi cha zima moto kufika kuzima. Moto umeanza kuwaka gorofa ya nne muda wa saa saba.

Kikosi cha zima moto na uokoaji wanaendelea kuuzima moto katika mazingira magumu

Hadi sasa maji yamewaishia huku moto ukiendelea kuwaka gorofa ya nne inayodaiwa ni Godauni. Chanzo cha moto hakijajulikana bado
IMG_20191102_160716_5.jpg
IMG_20191102_155953_8.jpg
IMG_20191102_160557_6.jpg

Stay tuned
 
Masaa mawili na kituo chao kipo karibu na hapo, na maji kuisha!!!!

Hili ni janga

I hope watu wote wameweza kutoka
 
Naona hakuna space ya kutosha kati ya jengo moja na lingine,hii inaweza kusababisha madhala kwa majengo mengine.
Na sio tu kwa majengo marefu,kuna baadhi ya mitaa fence za nyumba zimeungana kitu ambacho ni hatari kiusalama.

Watumishi wamegawa sana vibali vya majengo bila kujali, rushwa mbele.
 
Habari,

Kuna gorofa inawaka moto muda huu mtaa wa Livingstone na Mkunguni, zima moto wameshafika wanaendelea kuzima.

Imewachukua saa mbili kikosi cha zima moto kufika kuzima. Moto umeanza kuwaka gorofa ya nne muda wa saa saba.

Kikosi cha zima moto na uokoaji wanaendelea kuuzima moto katika mazingira magumu

Hadi sasa maji yamewaishia huku moto ukiendelea kuwaka gorofa ya nne inayodaiwa ni Godauni. Chanzo cha moto hakijajulikana bado
View attachment 1251975View attachment 1251978View attachment 1251979

Stay tuned
Maji kama yamewaishia watumie kubwa lao pepsi.
 
Kwa jinsi majengo yalivyo banana tuombe yasitokee madhara kwa binaadam.
 
Majengo yamebanana Kama vile hakuna maisha isipokua Dar tu?
Njoeni mikoani huku mujenge Na miji nayo iinuke
 
Back
Top Bottom