Kardinali Pengo: Watu wasisambaze chuki, Kanisa Katoliki haliendeshwi kwa ruzuku ya Serikali

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,863
image.jpeg

*Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameonya dhidi ya uzushi wa baadhi ya watu kuwa ruzuku toka serikalini ndizo kichocheo cha maendeleo ya Kanisa hilo.

*Awataka Watanzania kumuunga mkono Rais JPM,kwani magumu ya sasa ni dalili ya maisha ya neema ya kesho.Watanzania wazoee kupitia magumu ili kufikia maisha mazuri.

Akizungumza na gazeti Kiongozi Kardinali Pengo amesema kuwa, hizo ni chokochoko za wasiolitakia mema Kanisa na kwamba zisipokemewa kwa dhati zinaweza kusababisha chuki za kidini jambo ambalo ni hatari katika jamii.

“Mimi sina kubwa la kusema ila ninawaambia watu hawa kuwa, wachunguze kwanza kabla ya kusema, hakuna ukweli wowote juu ya Kanisa Katoliki eti linasaidiwa na Serikali na haya ndiyo yanayoleta chokochoko na chuki za kidini baadaye,” amesema Kardinali Pengo.

Ameongeza kuwa, kuna vitu vingi ambavyo vinazungumzwa mtaani juu ya Kanisa Katoliki na kuanza kuamsha chuki, baina ya wale wenye uelewa mdogo kuwa Kanisa Katoliki linapewa fedha na Serikali kitu ambacho si kweli.

Kardinali Pengo ameendelea kusema kuwa Kanisa Katoliki lina vyanzo vyake vingi vya kupata fedha ikiwemo sadaka za waamini, ambazo ndizo zimekuwa chachu ya kuendelea kwake na kuwa kila nchi hapa duniani Kanisa limekuwa likijiendesha lenyewe pasipo kutegemeana.

“Kanisa lina miradi chungu nzima zikiwemo shule na hospitali, ambazo zimekuwa zikiingiza fedha na kulisaidia Kanisa kukua na kujitegemea pasipo kutegemea chochote, wanaodai kuwa tunapewa ruzuku na Serikali si wakweli wachunguze, sio kukaa na kuzungumza vitu vya uongo”amesema Kardinali Pengo.

Ameendelea kusema kuwa Kanisa Katoliki halijawahi kupata fedha wala kwenda kuomba msaada serikalini ili kuendesha shughuli zake za uinjilishaji ila watu wasiokuwa na mapenzi mema na Kanisa hilo wamezusha taarifa hizo hewa ndiyo chanzo cha kusambaa kwa chuki ambapo baadhi ya watu wa madhehebu mengine wataamini kitu ambacho si cha kweli.

Aidha Kardinali Pengo amewataka waamini wa kanisa hilo kuendelea kusali na kuwaombea kwa Mungu watu wanaozusha taarifa za uongo ili wawe na ufahamu wa mambo wajue na kulitambua kanisa katoliki na kuwa wajinze jinsi kanisa hilo linavyojiendesha ili nao wapeleke neema hiyo katika madhehebu yao waweze kuendelea kama kanisa katoliki lilivyoendelea.

Mbali na hilo Kardinali Pengo ametumia fursa hiyo kuendelea kuwatia moyo watu kuvumilia hali ngumu ya maisha yaliyopo sasa kwa kuwa ugumu huo wa maisha ndiyo njia ya kufikia mafanikio.

Amewataka kuacha kulalamikia kitendo cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kununua ndege na kuanza kwa mchakato wake wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa huko Chato Mkoani Geita kwa kuwa nalo ni jambo jema.

Amesema ili kufikia mafanikio ni lazima kupitia magumu kwa kuwa kila safari ina changamoto zake na kwa changamoto hizo ni lazima wananchi wafunge mikanda ili kuimaliza amewataka kumuombea rais Magufuli ili kumaliza changamoto hizo na si kumlaumu.

Chanzo: Kiongozi(Gazeti)

=======

My take: Ukipata Kitabu kinachoitwa "HOW THE CHURCH AND GOVERNMENT GOT THE SAME BED" hutashangazwa na kauli ya Mwadhama Polycalp Cardinal Pengo kumsifia JPM kujenga uwanja mkubwa wa ndege CHATO.

Wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.Alifanikiwa...

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa. Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clabu zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" kama "Public Crime" ..Yaani mwananchi ukiwa mtaani umnabishana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu... Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu". Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu. Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako". (Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii(kidding)).

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoana hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church". Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa, na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani; japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Rail station. Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu? Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio "rasharasha" waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya "serikali ya kifashisti" ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.

Baadae aliwaingiza mapadre na maaskofu wote wa Italia kwenye "payroll" ya serikali,wakawa wanalipwa mshahara na serikali usiokatwa kodi.Mpaka leo Padre wa Kanisa Katoliki Italia analipwa mshahara na serikali.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini. Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema "hewalaaa", huu ni utawala mzuri tu, maana "umerudisha" heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu, pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika. Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda, lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU".

Kama hali hii ni kwa sababu mianya yote ya wapiga dili imefunikwa basi na tusema, na sio kusema kinyume chake.Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika, ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka.Kwamba kauli hii inakuja siku kadhaa baada ya mtu kutembelewa nyumbani kwake,inaweza kuwatia watu woga.Kanisa libaki kuwa mali ya waumini wanyonge,liachane na "urafiki" wa mashaka kama ule wa "Mussolini" na "Vatican" enzi hizo za zama za giza za Ulaya.

Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya "ufashisti" wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya "Ugumu wa maisha na hali mbaya ya Uchumi" kwa waumini wake.Kutoa kauli za aina hii hadharani,mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatupa mashaka na tutaamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed".

Tukizifunua kurasa hizi; Tutahitimisha kwa kusema "Pengo ameongea lile alilotumwa kuongea na sio alilojituma kulitumikia".

Tutamkumbusha Pengo kuwa kuutumikia mwili ni gharama zaidi ya kuitumikia roho. Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body).

Tusiwe Watumwa wa miili yetu ili tuwe huru,tukubali kuwa watumwa wa roho,zinazoishi milele... Haya ya duniani yanakuja na kupita.
 
Ni aibu mtu anayejiita kiongozi mkubwa kuwa muongo na mnafiki.

Mkuu wala usishangae,ukipata Kitabu kinachoitwa "HOW THE CHURCH AND GOVERNMENT GOT THE SAME BED" hutashangazwa na kauli ya Mwadhama Polycalp Cardinal Pengo kumsifia JPM kujenga uwanja mkubwa wa ndege CHATO.

Wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.Alifanikiwa...

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clabu zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" kama "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani umnabishana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"(Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii(kidding))

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoana hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Rail station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu?Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio "rasharasha" waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya "serikali ya kifashisti" ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.

Baadae aliwaingiza mapadre na maaskofu wote wa Italia kwenye "payroll" ya serikali,wakawa wanalipwa mshahara na serikali usiokatwa kodi.Mpaka leo Padre wa Kanisa Katoliki Italia analipwa mshahara na serikali.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema "hewalaaa",huu ni utawala mzuri tu,maana "umerudisha" heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu,pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika.Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda,lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU"

Kama hali hii ni kwa sababu mianya yote ya wapiga dili imefunikwa basi na tusema,na sio kusema kinyume chake.Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika,ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka.Kwamba kauli hii inakuja siku kadhaa baada ya mtu kutembelewa nyumbani kwake,inaweza kuwatia watu woga.Kanisa libaki kuwa mali ya waumini wanyonge,liachane na "urafiki" wa mashaka kama ule wa "Mussolini" na "Vatican" enzi hizo za zama za giza za Ulaya.

Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya "ufashisti" wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya "Ugumu wa maisha na hali mbaya ya Uchumi" kwa waumini wake.Kutoa kauli za aina hii hadharani,mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatupa mashaka na tutaamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Tukizifunua kurasa hizi;Tutahitimisha kwa kusema "Pengo ameongea lile alilotumwa kuongea na sio alilojituma kulitumikia"

Tutamkumbusha Pengo kuwa kuutumikia mwili ni gharama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tusiwe Watumwa wa miili yetu ili tuwe huru,tukubali kuwa watumwa wa roho,zinazoishi milele...Haya ya duniani yanakuja na kupita
 
Nimemuuelewa Baba Askofu, ila kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato, BIG NO!

Huko Chato kuna nini cha kufanya uwanja wa ndege ujengwe, tena kwa siri bila fedha kuidhinishwa na bunge?

Kuna biashara gani, kuna utalii gani chato... huko ni kufuja hela za walalahoi. Kwann fedha hizo zisingetumika kukarabati uwanja wa Mtwara, au Kigoma?

Chato kuna nini, au ndio mawazo ya kutawala milele. Au ndio mawazo ya yeye kuwa mfalme. Si alisem atakuwa anatumia usafiri wa barabara akiwa Tz, sasa fedha za kujenga uwanja za nini... Au ma VX yanatua airport siku hizi..!?
 
Mkuu wala usishangae,ukipata Kitabu kinachoitwa "HOW THE CHURCH AND GOVERNMENT GOT THE SAME BED" hutashangazwa na kauli ya Mwadhama Polycalp Cardinal Pengo kumsifia JPM kujenga uwanja mkubwa wa ndege CHATO.

Wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.Alifanikiwa...

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clabu zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" kama "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani umnabishana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"(Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii(kidding))

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoana hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Rail station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu?Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio "rasharasha" waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya "serikali ya kifashisti" ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.

Baadae aliwaingiza mapadre na maaskofu wote wa Italia kwenye "payroll" ya serikali,wakawa wanalipwa mshahara na serikali usiokatwa kodi.Mpaka leo Padre wa Kanisa Katoliki analipwa mshahara na serikali.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema "hewalaaa",huu ni utawala mzuri tu,maana "umerudisha" heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu,pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika.Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda,lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU"

Kama hali hii ni kwa sababu mianya yote ya wapiga dili imefunikwa basi na tusema,na sio kusema kinyume chake.Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika,ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka.Kwamba kauli hii inakuja siku kadhaa baada ya mtu kutembelewa nyumbani kwake,inaweza kuwatia watu woga.Kanisa libaki kuwa mali ya waumini wanyonge,liachane na "urafiki" wa mashaka kama ule wa "Mussolini" na "Vatican" enzi hizo za zama za giza za Ulaya.

Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya "ufashisti" wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya "Ugumu wa maisha na hali mbaya ya Uchumi" kwa waumini wake.Kutoa kauli za aina hii hadharani,mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatupa mashaka na tutaamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Tukizifunua kurasa hizi;Tutahitimisha kwa kusema "Pengo ameongea lile alilotumwa kuongea na sio alilojituma kulitumikia"

Tutamkumbusha Pengo kuwa kuutumikia mwili ni ghalama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tusiwe Watumwa wa miili yetu ili tuwe huru,tukubali kuwa watumwa wa roho,zinazoishi milele...Haya ya duniani yanakuja na kupita
Kwanza Sizonje alilihasi kanisa na kutengwa kwa migogoro ya ndoa.... Sizonje alipohamia kwa yule mama wa kebbys akahamia kwa makanisa ya kiroho...

Leo wanamwona mtamu.... Wacha pesa itawale dunia.... Kama hadharani BAKWATA ilipewa briefcase ile je huko sirini akina Pengo wanapewa nini?
 
Back
Top Bottom