Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

Status
Not open for further replies.
Padri SLAA na Padri Pengo wote lao moja wasitusitushughulishe hapawote wanafiki hawana lao wameanzisha chama wakadhani watashinda maana padri slaa alikuwa ndio chaguo lao .sasa kaanguka ndio wameanzisha USAVIMBI hata kumkemea alipoiba mke wa mtu walishindwa viongozi gani wa kiroho wanatetea ZINAA
 
Kaaaaaaaaaazi kweli kweli, chama chetu hawapendi mtu msema kweli, kama we ni magumashi utadumu, pengo udumu baba askofu.
 
Hta ule waraka wake alioutowa ulikubalika na kusimamiwa na chadema lazima aseme hayo ila CHADEMA hata ukiitetea ni chama cha fujo na kinamilikiwa na yeye huyo hata usemaje hatudanganyiki
Sasa hudanganyiki na nini au unajisemea semea tu maneno usiyojua maana yake.
 
Ndugu yangu USAVIMBI wa hawa watu upo kwa ajili ya kumtetea mtanzania wa kipito cha chini ndugu yangu, nadhani hujaelewa wanachomaanisha, maslahi ya nchi na mke wa mtu yanakujaje hapa, mwenye mke yupo kama yupo mbona hasemi kitu we ni msemaji wake?
 
Kuna jamaa mmoja kule "raia mwema" amesema, mlikuja na ukabila mkashindwa, mkaja na udini nao ikakosha mshiko sasa mnakuja na Uhaini...
 
Padri SLAA na Padri Pengo wote lao moja wasitusitushughulishe hapawote wanafiki hawana lao wameanzisha chama wakadhani watashinda maana padri slaa alikuwa ndio chaguo lao .sasa kaanguka ndio wameanzisha USAVIMBI hata kumkemea alipoiba mke wa mtu walishindwa viongozi gani wa kiroho wanatetea ZINAA

Inaonesha una jambo la kuzungumza.. Anzisha thread yake.

Pepombili una matatizo gani?? watu wakitetea kwa kusema ukweli kuhusu hali ya maisha ya mtanzania anaonekana mdini kisa tu kavaa joho..
Pengo ni mtanzania, ana haki ya kutoa maoni yake bila kujali dini yake.

Njaa,magonjwa,umaskini na ujinga havichagui dini.. kama huna mipango ya maana sio rahisi kufanikiwa

Hebu Pepombili punguza jazba na udini wako, na badala yake ujibu hoja kwa hoja
 
Ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli tu hata kama ni mchungu kiasi gani tuumeze tu ndugu zangu.

Wakati Maaskofu wakilaani wizi wa kura za CUF mwaka 1995 na mauaji ya Wanachama wa CUF wala hawakuwa na Udini lakini kwa kuwa wanatetea haki ya CHADEMA sasa Wanaudini ndugu zangu tuwe wakweli na ukweli ndio pekee utakao tuletea AMANI, UPENDO, UMOJA na MSHIKAMANO kwa sisi Watanzania na wala si Unafki wa kina J.K wa kikwere na kina Wasira ni fitina za kijinga zinazopandikizwa ili watanzania tuchukiane pasipo na sababu za msingi kabisa.

Kwani wakati CCM wakiwauwa Wapemba wakati wakiwa wanawapenda CUF unafikiri ilikuwa ni kwa faida ya Wazanzibari au WATAWALA WA CCM ambao walikuwa wanalinda ulaji wao na watoto wao kwa kumwaga damu zisizo na hatia!.

AMANI ya nchi hii italetwa na Watanzania walioshiba na wala si viongozi walafi wa CCM ambao wamekuwa wabinafsi wakiijilimbikia mali za wizi ambazo hazina maelezo yakujitosheleza jinsi walivyozipata.

UTULIVU utakuwepo tu wakati HAKI inatendeka kwa kila raia anaestahili kuipata haki hiyo. Tunata utawala BORA na wa SHERIA kila mahali ili watanzania tujivunie nchi yetu hii na Siyo nchi inayotawaliwa kwa staili ya BMW= Baba kiongozi, Mama kiongozi na Watoto nao viongozi achilia mbali Ushangazi, Ujomba, Ubabu, Ubaba mdogo/mkubwa, Ushikaji na Upenzi wa kike au wa kiume!. Nchi hii haiwezi kuongozwa kwa staili hii hata kidogo.

Tulisema, tunasema na tutaendelea kusema hadi tutakapokuwa na Serikali inayosikiliza wananchi wake na kutatua matatizo ya msingi ya Taifa hili na wala si kupeana sifa za kijinga kwenye makaratasi tu.

"NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO"
 
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema haoni tatizo katika maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana, Kardinali Pengo alisema badala yake Serikali: Ichimbue mizizi ya matatizo badala ya kukimbilia kukata matawi.

Kauli ya Pengo ni kama inaunga mkono matamshi yaliyotolewa juzi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema na badala yake ijirekebishe kwa kuwa na wepesi wa kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini.

Kadhalika, kauli hiyo ya Pengo imekuja wakati Serikali ikiendelea kulaani maandamano hayo ya Chadema na kutaka yasitishwe kwa madai kuwa yanaweza kuleta machafuko nchini.

Katika mahojiano hayo Kardinali Pengo alisema haoni kama Chadema kinafanya vurugu katika maandamano yake kama baadhi ya watu wanavyodai: Sioni point ya kusema maandamano ya Chadema yanaweza kusababisha vurugu, alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

Alisema ikiwa kuna tatizo katika maandamano hayo kama inavyoelezwa na serikali, ni bora hali hiyo ikafafanuliwa mapema na kukiambia Chadema kisitishe kuandamana.

Lakini serikali isichukulie comment (maoni) ya mtu mmoja mmoja na kusema kwamba Chadema inasababisha vurugu
, bila kusikiliza na kuchambua kwa undani, alisema.

Aliongeza kuwa endapo serikali imechunguza na kubaini ukweli kwamba maandamano hayo yanaweza kuleta vurugu za kisiasa, basi iyasitishe badala ya kutoa kauli tu kwamba yanahatarisha amani.

Pengo alisema huenda uamuzi wa Chadema kufanya maandamano unatokana na madai yao dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha, umeme na malipo kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwamba hayakusikilizwa.

Alisema Serikali haitakiwi kuyafumbia macho matatizo ya kisiasa nchini badala yake itafute kiini chake na namna ya kuyatatua.

Serikali ianze kuchimbua mizizi ya matatizo ya kisiasa yaliyopo ndani ya Taifa, badala ya kukimbilia kukata matawi. Kwa sababu kuanza kukata matawi ni kuzidi kuipeleka nchi katika machafuko ya kisisasa na matokeo yake ni kuleta madhara kwa wananchi, alisema.

Askofu huyo mkuu pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha inafuatilia matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa, ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili watu wasipate fursa ya kudai mambo hayo kwa maandamano.

Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, Serikali pia haipaswi kutoa vipaumbele kwenye masuala ya siasa na kusahau matatizo ya wananchi kwani hilo linaweza kuwa kiini cha vurugu... "Serikali iguswe kama ilivyoguswa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu."


Baadaye akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kuashiria kuanza kwa siku 40 za Mfungo wa Kwaresma ambao Wakristo hukumbuka mateso ya Bwana wao, Yesu Kristo kabla ya Pasaka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Kardinali Pengo alikemea tabia ya viongozi kung'ang'ania madaraka na kudhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo au kusonga mbele.

"Yapo matatizo katika viongozi wanaong'ang'ania madaraka wakiwa tayari hata kumwaga damu ya wengine ili wao wabaki madarakani. Hawa ni viongozi wanaofikiri uwezo unaweza kuwa ndani yao, wanajifanya wao Mungu," alisema Pengo.

Alisema viongozi hao wanatazama fadhila za kibinadamu wakiacha upungufu wao na kudhani kuwa wasipokuwa na madaraka basi nchi zao hazitakuwepo jambo ambalo si sahihi na halifai katika jamii.

"Viongozi hao wanajifanya wao ndiyo miungu, wanatazama fadhila za kibinadamu, wakiacha mapungufu yao. Hicho ni kiburi, wakumbuke kuwa Mungu aliwaumba kwa vumbi na watarudi kuwa vumbi, sasa kwa nini mnakuwa na kiburi?," Alihoji Kardinali Pengo na kuongeza;

"Mungu aliwaumba kwa vumbi kwa nini wawe na kiburi? Unadhani ukifa na nchi itakufa, kwani kabla yako nchi haikuwepo? Kumbuka wewe ni uvumbi na utarudi mavumbini."

Alisema thamani ya mtu haitokani na anavyojiona, bali nguvu ya Mungu akiwakumbusha Wakristo kutubu na kumrudia Mungu katika kipindi hiki cha Kwaresma.

Wakati huohuo; Festo Polea anaripoti kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao wapo katika taasisi isiyo ya kiserikali ya Truya wamesema ili kuondokana na machafuko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, viongozi wanaokiuka matakwa ya uongozi, uvunjaji wa Katiba na sheria za nchi wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Helman Sheluleta alisema Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi inatambua haki ya mtu kutoa maoni, kusikilizwa na kuandamana kwa amani na kwa mujibu wa sheria lakini sheria inapovunjwa kwa ajili ya kupata haki ndiko kuhatarisha amani ya nchi.

Source: Mwananchi March 10, 2011
=================================================================
Hatukutarajii uone tatizo ndani ya Chadema!
Ila unadhihirisha kile ambacho wengi humu wanakificha kwamba Mkulu unashabikia na ulishawishi watu washabikie Chama chetu kileeee!
Kwa heshima zote zinazosmstahikia kiongozi mkubwa wa jamii kama Muadham Pengo nahisi hakuwa mkweli wa nafsi yake juu ya mambo yaliyo katika bold (ikiwa kauli hizi ni zake kweli).
Kama kiongozi wa diniangekuwa mkweli kueleza kuwa hakuna uwezekano wa kuondowa kauli ya viongozi wa CHADEMA aliowaita yeye kuwa kauli za mtu mmoja mmoja.

Angekuwa makini kujuwa watu mmoja hao hao ndio walikuwa chanzo cha mauwaji ya Arusha. Isitoshe JK alisema wazi kuwa Maandamano si tatizo bali matamshi ya viongozi ndio tatizo.

Mhasham Pengo angekuwa mkweli kama kiongozi wa jamii kutowa wasia kwa hao anaowaita mtu mmoja mmoja kuacha hiyo tabia ya kuharibu Amani.

Asiwe ni kiongozi wa kuishauri serikali tu bali wanajamii wote hata hao mtu mmoja mmoja (akimaanisha wale wanaopata nafasi ya kutowa matamshi ambao ni viongozi wa vyama)
 
Nafikiri wengi we2 ha2jaelewa bt CDM wanahitaji ku2elimisha zaidi wananchi kuhusu kutohusika na udini
 
Ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli tu hata kama ni mchungu kiasi gani tuumeze tu ndugu zangu.

Wakati Maaskofu wakilaani wizi wa kura za CUF mwaka 1995 na mauaji ya Wanachama wa CUF wala hawakuwa na Udini lakini kwa kuwa wanatetea haki ya CHADEMA sasa Wanaudini ndugu zangu tuwe wakweli na ukweli ndio pekee utakao tuletea AMANI, UPENDO, UMOJA na MSHIKAMANO kwa sisi Watanzania na wala si Unafki wa kina J.K wa kikwere na kina Wasira ni fitina za kijinga zinazopandikizwa ili watanzania tuchukiane pasipo na sababu za msingi kabisa.

Kwani wakati CCM wakiwauwa Wapemba wakati wakiwa wanawapenda CUF unafikiri ilikuwa ni kwa faida ya Wazanzibari au WATAWALA WA CCM ambao walikuwa wanalinda ulaji wao na watoto wao kwa kumwaga damu zisizo na hatia!.

AMANI ya nchi hii italetwa na Watanzania walioshiba na wala si viongozi walafi wa CCM ambao wamekuwa wabinafsi wakiijilimbikia mali za wizi ambazo hazina maelezo yakujitosheleza jinsi walivyozipata.

UTULIVU utakuwepo tu wakati HAKI inatendeka kwa kila raia anaestahili kuipata haki hiyo. Tunata utawala BORA na wa SHERIA kila mahali ili watanzania tujivunie nchi yetu hii na Siyo nchi inayotawaliwa kwa staili ya BMW= Baba kiongozi, Mama kiongozi na Watoto nao viongozi achilia mbali Ushangazi, Ujomba, Ubabu, Ubaba mdogo/mkubwa, Ushikaji na Upenzi wa kike au wa kiume!. Nchi hii haiwezi kuongozwa kwa staili hii hata kidogo.

Tulisema, tunasema na tutaendelea kusema hadi tutakapokuwa na Serikali inayosikiliza wananchi wake na kutatua matatizo ya msingi ya Taifa hili na wala si kupeana sifa za kijinga kwenye makaratasi tu.

"NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO"
Naona kama huna kumbukumbu nzuri juu ya maoni ya viongozi hao akiwamo Pengo wakati wa mauwaji ya Pemba. Rudi katika historia na utambue nini kauli ya Pengo ilikuwa!

Kuhusu karipio ni haki yake lakini si ameshaelewa kuwa kuna kauli alizoziita za watu wachache ambazo ndio zinazohubiria uchafuzi wa Amani basi angegeuza upande wa pili wa upanga wake kuwashughulikia hao.

Lakini kwa vile hao wachache ni ndio viongozi wa CHADEMA anashindwa kuwakaripia. Huu upendeleo ndio unaofanya tulaumu kitendo cha Kardinali.
 
Kwani Pengo ni nani vile? Dr Padre Slaa ni wale wale.

Ukweli utadhihiri Chadema acheni hayo. hata Arusha ni dini na watu hawa hawa walimkataa meya.

Ni hatari sana, maana hawa ndo wapiga kura.. itachukuwa muda kiasi wa watu kutofautisha hali halisi na udini. Ninapata wasi wasi sana kwamba dini zetu hizi ni kikwazo kwa maendeleo yetu kama nchi.

Mtu kama huyu hawezi tena kufikiri zaidi ya aliyofundishwa kwenye nyumba ya ibada.

Wanasiasa wetu msikatishwe tamaa na watu wenye mawazo finyu kama hawa.
 

Kasikilize REDIO IMANI jamvini hakukufahi, kwenye mshiko kubali na kama pumba ponda, mpaka magazeti yameandika hujue hiyo habari ina tija na hutasikia viongozi wenu wa CCM wanakejeli kauli ya Kadinali Pengo maana yeye hakurupuki kama maaskofu sadaka.

Hawa wachache wenye kauli za uchochezi ni wepi hao? Sifikiri kuwa hao ni Mkwele na Ngekewa bali ni Viongozi wa CHADEMA, ndio wenye uwezo wa kupata viriri vya kuwahamasisha vijana (kama Arusha)

Halafu ndugu yanguMkwele huyu baba mtakatifu kwanini asiwape neno la Amani hawa?

Hakuna anaeridhika na matatizo lakini nafikiri namna ya kuyatatuwa ndio tatizo! The same to CHADEMA.
 
Natamani sana Tendwa,Sokwe,Makambale,Tambwe Hiza ,Sophia Kungwi aka mtaalam wa ngono,Uvccm wote wajitokeze kujibu kauli za huyu Philosopher....halafu usikie muziki wa Jemadali Pengo!

Hawa wote uliowataja IQ zao ni sawa na zero.jana nimemsikiliza mama simba BBC anaongea siasa badala ya kuongea hali halisi na ilikuwa kama pumba tupu kazidiwa kete na wenzake wa Rwanda na Uganda.

Cardinal Pengo yuko sahihimda sii mrefu utasikia kaongea kwa vile dr slaa hakushinda.Sokwe hapo ndio umeniacha hoi sijaelewa ni nani labda ni yule ambae anakisiwa alikuwa anapita mbuga za wanyama polisi kasimamisha gari na kummuliza dreva anapeleka wapi huyo Sokwe jamani makubwa.
 
Wana JF,
Salaam toka Monrovia Liberia, ambako mimi na Mhe Freeman Mbowe tunahudhuria Mkutano wa DUA( Democratic Union of Africa). Tutakuwa hapa hadi 14 March ambapo tutarejea nyumbani.

Nadhani mjadala unavyoendelea hapa "one can easily tell between 'small minds' ambao kazi yao ni kuzungumzia "watu" badala ya "Issues". Ukiish kujua tatizo huhitaji kugombana nao. Waache wapoteze muda wao na kujifurahisha kwa kuwa hawana mchango kwa Taifa.

Hakuna ashabu kubwa unayoweza kumpa mtu kuliko kum "ignore" Let us ignore them and move forward. The nation needs "our precious time on critical issues. Udini is no longer an issue, wanaochochea wanajulikana, Dr Slaa kumpora mke wa mtu is not an issue wamejaribu njia za kisheria wamebaki na nonsensical propaganda.

Mwenye Busara ni yule anayeuliza kama hajui facts, asiyetaka kujua usihangaika naye. There are more pressing issues for the nation, wale "serious minds" let us focus on those issues. Historia haitatuhukumu kwa kuzungumzia propaganda bali kwa kukuacha kuchukua "serious action on fundamental issues". Nawatakia heri sana nyumbani


Padri SLAA na Padri Pengo wote lao moja wasitusitushughulishe hapawote wanafiki hawana lao wameanzisha chama wakadhani watashinda maana padri slaa alikuwa ndio chaguo lao .sasa kaanguka ndio wameanzisha USAVIMBI hata kumkemea alipoiba mke wa mtu walishindwa viongozi gani wa kiroho wanatetea ZINAA
 
Kwani hamjui kama viongozi committed wa kikikristo wanaita kijiko kijiko na si koleo. Ukristo haujajengwa juu ya unafiki na husuda kama hao wengine tunaowaona na kushuhudia matamko yao ambao uongo wake unawakera hata watoto wadogo wasiojua chochote
Sifikiri kuwa neno la Mungu linaupendeleo! Kukiri kuwa wapo watu wachache wabaya na ukashindwa kuwahukumu, nao huu ndio ukiristo?
 
Arch Bishop P.Pengo Just like Desmund Tutu etc...........fanya kazi ya kuelimisha Viongozi wajue nini maana ya Haki na si kuhubiri Amani.
 
Wana JF,
Salaam toka Monrovia Liberia, ambako mimi na Mhe Freeman Mbowe tunahudhuria Mkutano wa DUA( Democratic Union of Africa). Tutakuwa hapa hadi 14 March ambapo tutarejea nyumbani.
Nadhani mjadala unavyoendelea hapa "one can easily tell between 'small minds' ambao kazi yao ni kuzungumzia "watu" badala ya "Issues". Ukiish kujua tatizo huhitaji kugombana nao. Waache wapoteze muda wao na kujifurahisha kwa kuwa hawana mchango kwa Taifa. Hakuna ashabu kubwa unayoweza kumpa mtu kuliko kum "ignore" Let us ignore them and move forward. The nation needs "our precious time on critical issues. Udini is no longer an issue, wanaochochea wanajulikana, Dr Slaa kumpora mke wa mtu is not an issue wamejaribu njia za kisheria wamebaki na nonsensical propaganda. Mwenye Busara ni yule anayeuliza kama hajui facts, asiyetaka kujua usihangaika naye. There are more pressing issues for the nation, wale "serious minds" let us focus on those issues.Historia haitatuhukumu kwa kuzungumzia propaganda bali kwa kukuacha kuchukua "serious action on fundamental issues". Nawatakia heri sana nyumbani

Mkuu Dr W. Slaa, nakubaliana na hoja yako uliyotoa kama hitimisho la huu mjadala. Ni kweli kuwa huwezi kumfundisha mtu aliyekwisha kuchagua njia yake, msimamo wake na mtazamo wake, akaelewa.

Mimi huwa nashindwa kuelewa watu wengine tunasimama upande wa maslahi yepi? Ya dini? au ya Jamii? Kwasababu ukimchukia Dr W Slaa kwa vile ni Padre, je huyo padre si Mtanzania mwenziyo? Je kwakuwa ni padre hana jambo lolote lililo jema atakalosema na linalogusa maslahi ya taifa ukamuunga mkono?

Inashangaza kuona kuna watu kila Cardinal akisema jambo lenye hekima ya kiwango wanaanza kumpinga kwa mashambulizi kuwa anatetea CDM! Ni mkatholic huyo..!!! Watu hawa, mimi sioni hekima yao yoyote yenye neema na mapenzi mema kwa taifa letu. Watu hawa, nadhani waliokuwa na lengo lao ovu dhidi ya jamii yetu, lkn wanaona uwezekano wa kutimia kwa uovu wao unatiwa kiza, sasa wanaanzisha matukano dhidi ya wanaharakati wetu. Haitasaidia chochote na wakati wowote...

Mimi naona kuwa, kauli zetu hizi za hovyohovyo, tunazotamka hapa, haziendi na upepo na kupotea, bali zinakaa katika mioyo ya watu. Watu hao wanaosikia kauli hizi, wanakwenda kurithisha watoto na wajukuu zao, baada ya muda tutachukiana upeo na kuuana. Katika hatua hiyo pevu, usitegemee kuna atakayeshinda, na kubaki kwa amani peke yake, na kula matunda ya ushindi huo kwa amani tele na raha mstarehe. Hiyo ni ndoto ya mchana kweupe. Njia nzuri ni ile ya kuacha imani zetu hukooo misikitini, hekaluni na makanisani, na kuishi Tanzania kama M-Tz wa kawaida bila kubaguana. Tumwachie Mungu kufanya ubaguzi siku ile ya kiyama, wengine watakwenda peponi na wengine ahera kwa vigezo Vyake na si vyetu.

Kama kuna mtu anadhani anaweza kutetea dini yake kupitia siasa, basi dini yake haina Mungu, na kama aliwahi kuwepo huyo Mungu wake alikufa na hajafufuka na bahati mbaya hatafufuka milele.
 
Natamani sana Tendwa,Sokwe,Makambale,Tambwe Hiza ,Sophia Kungwi aka mtaalam wa ngono,Uvccm wote wajitokeze kujibu kauli za huyu Philosopher....halafu usikie muziki wa Jemadali Pengo!

umenikumbusha mbali sana kuhusu makambale(makufuli) thanks
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom