Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shinto, Mar 10, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema haoni tatizo katika maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana, Kardinali Pengo alisema badala yake Serikali: “Ichimbue mizizi ya matatizo badala ya kukimbilia kukata matawi.”

  Kauli ya Pengo ni kama inaunga mkono matamshi yaliyotolewa juzi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema na badala yake ijirekebishe kwa kuwa na wepesi wa kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini.

  Kadhalika, kauli hiyo ya Pengo imekuja wakati Serikali ikiendelea kulaani maandamano hayo ya Chadema na kutaka yasitishwe kwa madai kuwa yanaweza kuleta machafuko nchini.

  Katika mahojiano hayo Kardinali Pengo alisema haoni kama Chadema kinafanya vurugu katika maandamano yake kama baadhi ya watu wanavyodai: “Sioni ‘point’ ya kusema maandamano ya Chadema yanaweza kusababisha vurugu,” alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

  Alisema ikiwa kuna tatizo katika maandamano hayo kama inavyoelezwa na serikali, ni bora hali hiyo ikafafanuliwa mapema na kukiambia Chadema kisitishe kuandamana.

  “Lakini serikali isichukulie ‘comment’ (maoni) ya mtu mmoja mmoja na kusema kwamba Chadema inasababisha vurugu, bila kusikiliza na kuchambua kwa undani,” alisema.

  Aliongeza kuwa endapo serikali imechunguza na kubaini ukweli kwamba maandamano hayo yanaweza kuleta vurugu za kisiasa, basi iyasitishe badala ya kutoa kauli tu kwamba yanahatarisha amani.

  Pengo alisema huenda uamuzi wa Chadema kufanya maandamano unatokana na madai yao dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha, umeme na malipo kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwamba hayakusikilizwa.

  Alisema Serikali haitakiwi kuyafumbia macho matatizo ya kisiasa nchini badala yake itafute kiini chake na namna ya kuyatatua.

  “Serikali ianze kuchimbua mizizi ya matatizo ya kisiasa yaliyopo ndani ya Taifa, badala ya kukimbilia kukata matawi. Kwa sababu kuanza kukata matawi ni kuzidi kuipeleka nchi katika machafuko ya kisisasa na matokeo yake ni kuleta madhara kwa wananchi,” alisema.

  Askofu huyo mkuu pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha inafuatilia matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa, ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili watu wasipate fursa ya kudai mambo hayo kwa maandamano.

  Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, Serikali pia haipaswi kutoa vipaumbele kwenye masuala ya siasa na kusahau matatizo ya wananchi kwani hilo linaweza kuwa kiini cha vurugu... "Serikali iguswe kama ilivyoguswa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu."


  Baadaye akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kuashiria kuanza kwa siku 40 za Mfungo wa Kwaresma ambao Wakristo hukumbuka mateso ya Bwana wao, Yesu Kristo kabla ya Pasaka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Kardinali Pengo alikemea tabia ya viongozi kung'ang'ania madaraka na kudhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo au kusonga mbele.

  "Yapo matatizo katika viongozi wanaong'ang'ania madaraka wakiwa tayari hata kumwaga damu ya wengine ili wao wabaki madarakani. Hawa ni viongozi wanaofikiri uwezo unaweza kuwa ndani yao, wanajifanya wao Mungu," alisema Pengo.

  Alisema viongozi hao wanatazama fadhila za kibinadamu wakiacha upungufu wao na kudhani kuwa wasipokuwa na madaraka basi nchi zao hazitakuwepo jambo ambalo si sahihi na halifai katika jamii.

  "Viongozi hao wanajifanya wao ndiyo miungu, wanatazama fadhila za kibinadamu, wakiacha mapungufu yao. Hicho ni kiburi, wakumbuke kuwa Mungu aliwaumba kwa vumbi na watarudi kuwa vumbi, sasa kwa nini mnakuwa na kiburi?," Alihoji Kardinali Pengo na kuongeza;

  "Mungu aliwaumba kwa vumbi kwa nini wawe na kiburi? Unadhani ukifa na nchi itakufa, kwani kabla yako nchi haikuwepo? Kumbuka wewe ni uvumbi na utarudi mavumbini."

  Alisema thamani ya mtu haitokani na anavyojiona, bali nguvu ya Mungu akiwakumbusha Wakristo kutubu na kumrudia Mungu katika kipindi hiki cha Kwaresma.

  Wakati huohuo; Festo Polea anaripoti kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao wapo katika taasisi isiyo ya kiserikali ya Truya wamesema ili kuondokana na machafuko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, viongozi wanaokiuka matakwa ya uongozi, uvunjaji wa Katiba na sheria za nchi wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

  Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Helman Sheluleta alisema Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi inatambua haki ya mtu kutoa maoni, kusikilizwa na kuandamana kwa amani na kwa mujibu wa sheria lakini sheria inapovunjwa kwa ajili ya kupata haki ndiko kuhatarisha amani ya nchi.

  Source: Mwananchi March 10, 2011
  =================================================================
  Hatukutarajii uone tatizo ndani ya Chadema!
  Ila unadhihirisha kile ambacho wengi humu wanakificha kwamba Mkulu unashabikia na ulishawishi watu washabikie Chama chetu kileeee!
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  credible comments
   
 3. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sasa hivi watasema udini ile hali ndio ukweli wa mambo.......hongera Pengo misimamo siku zote ukweli utabaki kuwa ukweli na ni dhambi kuwa mnafiki kama baadhi ya mashekhe ubwabwa na maaskofu sadaka
   
 4. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Pengo alishawahi kuwa CUF ?maana mwaka 2000 aliwaonya Mkapa+Karume(CCM) wasiibe kura za CUF huko Wilayani Zanzibar,na alilaani sana mauaji ya WanaCUF 2001.Pengo huwa si Mnafiki husimamia ukweli daima.Ni mwanaharakati wa enzi hizo kabla hata ya CHADEMA,he stands on reality.Go go go Pengo!!!!
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa viongozi wa nchi hii walivyoshindwa kuelewa tatizo la watanzania, ili tuendelee tunahitaji "machafuko" zaidi kuliko "amani"

  Wanatumia nguvu nyingi kutuhubiria amani na kupambana dhidi ya maandamano ambayo ni ya amani lakini hawatumii nguvu yoyote kutatua matatizo yanayopelekea maandamano
   
 6. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Truth is objective. Haitegemei ni nani amesema. Pengo amesema ukweli. Hakuna dini hapo. "ukweli ni ukweli hata kama amesema mwendawazimu"
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kweli wewe un kumbukumbu sana....I salute ..ni kweli aliyasema maneno haya wazi wazi
   
 8. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  GOOD!!!!

  Maaskofu uchwara na Mashehe njaa kali huwa ni vigumu kukwepa noti(misimbazi) za JK,Lowasa na Rostam.Lazima wauze utu,wajifedheheshe kwa kutoa Matamko wasiyoyaamini.Huu ni unafiki mkubwa sana na mnalo la kujibu mbele za Subuana W.Waamini wenu ambao wanataabika na maisha magum nyie mnatafuta pesa chafu tu! Tumuigeni Arch Bishop Pengo,Desmund Tutu etc...
   
 9. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baba ukweli ndio huo. CHADEMA haija sema neno lolote la uongo= MAISHA KUPANDA, MALIPO YA DOWANS, MIKATABA MIBOVU INAYOLETA ATHARI KWA WANACHI= uongo uko wapi?? CCM jibu hoja wacha kuwadanganya wananchi
   
 10. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hta ule waraka wake alioutowa ulikubalika na kusimamiwa na chadema lazima aseme hayo ila CHADEMA hata ukiitetea ni chama cha fujo na kinamilikiwa na yeye huyo hata usemaje hatudanganyiki
   
 11. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Rudisha kwanza pesa za MOU kisha ndio usemme hayo maneno yake mumezitafuna sasa zimezuiliwa ndio munaanza kuchonga
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hilo ndio tatizo la msingi. Maisha kupanda hayakuanza leo, umesahau UKAPA wakati wa mkatoliki Mkapa? Mikataba mibovu wizi pia havijaanza leo, IPTL, Loliondo na scandal nyingine zilikuwepo kwenye awamu zilizopita mbona "BABA" alikaa kimya? Kwa nini sasa, kwanini abadilishe political affiliation ?

  Mmesahau huyu "BABA" alikuwa anawakejeli waandamanaji wa Pemba wasichezee mamlaka halali?
   
 13. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Well said Cardinal Pengo
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani Pengo ni nani vile? Dr Padre Slaa ni wale wale.

  Ukweli utadhihiri Chadema acheni hayo. hata Arusha ni dini na watu hawa hawa walimkataa meya.
   
 15. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kasikilize REDIO IMANI jamvini hakukufahi, kwenye mshiko kubali na kama pumba ponda, mpaka magazeti yameandika hujue hiyo habari ina tija na hutasikia viongozi wenu wa CCM wanakejeli kauli ya Kadinali Pengo maana yeye hakurupuki kama maaskofu sadaka.
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pengo yupo sawa kabisa, na nimefurah kwa kiongozi wa dini kutoa msimamo. Yote aliyoyasema Kadlinali yanaukweli, viongozi wengine wafuate nyayo zake!
   
 17. M

  Mwanaume Senior Member

  #17
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwani hamjui kama viongozi committed wa kikikristo wanaita kijiko kijiko na si koleo. Ukristo haujajengwa juu ya unafiki na husuda kama hao wengine tunaowaona na kushuhudia matamko yao ambao uongo wake unawakera hata watoto wadogo wasiojua chochote
   
 18. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa vile serikali imeshindwa kushughulikia kero za wananchi, kila wananchi wakipiga kelele kwa namna yeyote ile, serikali inasema eti wanataka kuvuruga amani! Sasa wananchi wafanyeje?

  Maana kunyamaza haiwezekani tena, kama serikali inataka watu wanyamaze, itatue na ishushe bei za umeme, sukari, mafuta, usafiri nk. Itangaze haimlipi Rost Am na inataifisha mitambo yake! Ihakikishe reli ya kati inafanya kazi kama enzi za Mwalimu.Inapandisha kiwango cha elimu. Inatengeneza ajira mpya kwa kujenga viwanda nk.
   
 19. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Yani hapo tatizo litakuwa kwamba maoni katoa Pengo, vilaza wa kuchambua wataleta isu zao za udini, lakini ukweli ni kwamba maoni ya Pengo ni halisi na yana maana kwa taifa hili kinyume cha makada wa ccm kama Tendwa, Wasira na wengine wanavyotaka tuamini.
   
 20. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Natamani sana Tendwa,Sokwe,Makambale,Tambwe Hiza ,Sophia Kungwi aka mtaalam wa ngono,Uvccm wote wajitokeze kujibu kauli za huyu Philosopher....halafu usikie muziki wa Jemadali Pengo!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...