Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Leo Katika kikao kilichoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na viongozi wa dini kardinal Pengo amemtetea dictator Mussolin aliyetawala Italia enzi hizo kama ifuatavyo.

Mussolin aliondoa baa au balaa la Malaria Katika mji mdogo wa Italia, Kwa mujibu wa kardinal Pengo wakati huo malaria ilitishia maisha ya watu hapo Italia.

Kuna mambo mazuri ya Mussolin na Hiltrer hayazungumzwi kwa mujibu wa kardinal Pengo.

Pengo amesisitiza darasani watu hufundishwa Hiltrer aliua wayaudi zaidi ya Milioni sita lakini hawataki Kuongelea mazuri ya Hitler.

Pengo ameiomba jamii itofautishe kati ya Dictate na neno dictator.

Akijenga hoja kuhusu watu wanaomuandika mheshimiwa Rais kuwa ni dictator,.amewaomba watafakari upya.

Je, kujenga hospital ni udikteta? Amehoji kardinal Pengo.

Je, watoto kusoma bure wao na wajukuu zao ni udikteta? Amehoji kardinal Pengo.

Amepongeza uongozi wa Makonda kama moja ya watu vijana wanamsaidia Rais.

Aidha Kardinal Pengo amesema alikuwa na hofu Rais wa sasa akimaliza muda wake nani atafaa na kufanya kama Rais wa sasa, Hofu imepungua kuona kuna vijana kama Makonda wanachapa kazi.
.
Kardinal Pengo amesisitiza uwepo wa vijana wachapa kazi kama Makonda na wakijitokeza wengi hana shaka kabisa kazi za Rais zitaendelezwa vizuri.

Kwa mujibu wa kardinal Pengo na Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es Salaam amesema haya mambo ya kumuita Rais dikteta anayasoma mitandaoni lakini pia kwa Uzee wake kuna watu wema wanampa taarifa nini kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Mwana Jamii Forum aitwaye "Barafu" ameelezea sana kwenye uzi mmoja jinsi Mussolin alivyoliteka kanisa wakati huo na kukandamiza Raia huko Italia.

Hili la Hiltrer na Mussolin Nadhani ni elimu mpya kuwa kuna mambo mazuri walifanya.

Tunaruhusu povu kwa wale wanaowalaumu viongozi wa kikatoliki, Kikubwa Wakatoliki kila jumapili kabla ya kuanza misa hutubu dhambi zao tofauti na wale wanaoanza kukusanya sadaka.

====

Kardinali Pengo amewashangaa watu wanaomuita Rais wa Tanzania, John Magufuli dikteta na kueleza kuwa wanakosea.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 18, 2019 wakati wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini na Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda, Kardinali Pengo amesema kumekuwa na watu wanaozungumza maneno ya kupotosha kuhusu rais Magufuli.

“Katika mitandao kumezuka maneno kwamba Rais wetu ni dikteta. Hivyo yale anayoyafanya anashughulikia kuendeleza vitu kuliko kuendeleza watu.”

“Wanaongelea juu ya kushughulikia vitu kuliko watu, ni watu gani hao hawajashughulikiwa wakati mambo mengi yanafanyika kwa ajili ya watu,” amesema Kardinali Pengo

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, “Ni lugha ambayo kwa akili zangu za kizee siwezi kuelewa, utakuwa unamshughulikia mtu kiasi gani kama unamfanya mtoto wake na mjukuu wake waende shule.”

Kardinali Pengo ambaye ni Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam amempongeza Makonda na kumtaja kuwa ni miongoni mwa wasaidizi bora wa Rais Magufuli.

“Nimefurahi, imenidhihirishia wewe ni kiongozi wa aina gani na tunamuomba Mungu atujalie viongozi wa aina yako wengi. Wewe (Makonda) ni mmoja kati ya wasaidizi bora wa Rais Magufuli.”

“Tunajiuliza baada ya Magufuli atakuwa nani ila mkiwepo wengi wa aina yako nisingekuwa na shaka ya kuwaza nani atafuata baada yake,” amesema


Chanzo: Mwananchi
 
Amepongeza uongozi wa Makonda kama moja ya watu vijana wanamsaidia Rais

Aidha Kardinal Pengo amesema alikuwa na hofu Rais wa sasa akimaliza muda wake nani atafaa na kufanya kama Rais wa sasa, Hofu imepungua kuona kuna vijana kama Makonda wanachapa kazi
Naunga mkono hoja

P
 
Naunga mkono hoja

P
Naona unajipiga promo za unabii

Na wewe kama unapenda Sana unabii fungua kanisa basi

Uitwe mtume na nabii pascal mayala
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom