Kardinali Pengo: Kanisa litasema kweli bila kuogopa gharama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kardinali Pengo: Kanisa litasema kweli bila kuogopa gharama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 13, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema viongozi ndani ya Serikali, wamekuwa wakitenda mambo mengi mabaya dhidi ya wananchi na kuficha uozo wao kwa gharama yoyote
  .

  Askofu Pengo alisema hayo jana alipokuwa anaongoza Ibada ya Misa kuwaombea watu waliopoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu Gongo la Mboto iliyofanika eneo la Hija Pugu, jijini Dar es Salaam.

  Kadnali Pengo alisema mambo yanayofanywa na viongozi hao ni pamoja na ufisadi dhidi ya mali za umma na matokeo yake ni serikali kulazimishwa kulipa mabilioni ya fedha kwa Kampuni ya Dowans wakati huduma zinazotolewa kwa wananchi ni hafifu.

  Alisema sakata la Dowans ni sehemu ndogo kati ya uozo mwingi unaofanywa na vigogo Serikalini na kufichwa pasipo wananchi kuufahamu.


  Kardinali Pengo alisema imefikia mahali baadhi ya watu wanatenda maovu na kufunga midomo watu na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba wako tayari kutoa uhai wa watu wanaodhani ni kikwazo kwao.


  Gongo la Mboto
  Kadnali Pengo alizungumzia milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto, kuwa ni ujumbe ambao Mungu alitaka kuutoa kwa Watanzania kuwa hali siyo nzuri na hivyo ni vyema kumrudia yeye (Mungu).

  "Kuna weza kusiwe na uhusiano wa moja kwa moja kati ya matukio kama haya na dhambi, lakini bado ujumbe unabaki pale pale, tusiyapuuzie. Kwani watu wa Gongo la Mboto wanadhambi kuliko watu wengine wote wanaoishi Dar es Salaam? La hasha! Tusipotubu nasi tutahangamia vivyo hivyo," alisema Askofu Pengo.

  Akihusisha matukio hayo na baadhi ya matukio yaliyoandikwa katika vitabu vitakatifu, Pengo alisema Nabii Yeremia alitaka kuuliwa kwa sababu tu alitoa unabii ambao siyo mzuri kwa taifa lake.

  Alisema wakati huo, watu waliangukiwa na mnara huko Yerusalemu na mfalme alipoletewa unabii juu na tafsiri ya tukio hilo la kuangukiwa na mnara huo, alitaka nabii huyo auawe.


  "Viongozi wanapenda tu habari za kuwafurahisha wao na wapambe wao. Wanapenda kusikia tu mambo mazuri hata kama ni ya kipumbavu. Yeremia alivyowaambia ukweli walifanya kila liwezekanalo kumuwa, mpaka wakaenda kumtupa kwenye kisima kilichokuwa na matope,"
  alieleza Kardinali Pengo:

  Aliongeza:
  "leo Mungu anataka kutufundisha nini Tanzania kwa matukio haya? Siyo mabomu tu, bali hata kutaka kulipa umeme ambao hata hatuupati?, Mabomu na mengine ni mambo tu ya nje. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu abadilike ili tuwe salama."

  Kiongozi huyo wa dini alisema ameamua kupasua ukweli hadharani kwa kuwa haogopi watu hao wanaowahujumu Watanzania, kwa sababu ametoa maisha yake kwa ajili ya kueneza neno la Mungu na kukemea maovu na wala haogopi kama watamuua
  .

  "Mimi nimesema haya leo, maisha yangu yapo mikononi mwenu, lakini kwa kuwa ni Mungu kanituma nitasema. Mkiniuwa leo au kesho sijali, mkisikia, msiposikia shauri yenu," alisema akionyesha kukerwa na tabia mbaya ya baadhi ya viongozi wa Serikali akifafanua:


  "Mkiniuwa damu yangu iko mikononi mwenu, kwa sababu mtakuwa mmemwaga damu isiyokuwa na hatia. Nasema hivi siyo kuwa naropoka, najua ninachokisema. Kwanini nifungwe mdomo? Nasema haya leo na nyie mkiwa hapa, kama kuna chombo kitakacho kuwa na ujasiri wa kuandika mtaona yatakayotokea."


  Hofu

  Kadnali huyo aliyekuwa akizungumza kwa hisia kali, alisema atasema lolote bila kuogopa hata kama vyombo vyote vya habari vikiwemo vya vya kanisa hilo, vitafungwa mdomo ili vifiche wananchi wasifahamu.


  Alisema katika kile kinachoonekana ni kufungwa mdomo kwa vyombo vya habari, wiki chache zilizopita wakati wa kusimka Renatus Nkwande kuwa Askofu mpya wa Jimbo jipya la Bunda alisema mambo mengi ya unabii kwa siku za usoni, lakini hayakuandikwa wala kutangazwa chombo chochote cha habari.


  Hata hivyo, Kardinali Pengo, hakuweka hadharani mambo hayo ya kinabii aliyoyasema hadharani siku hiyo na kuelezwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Thadeus Ruwaichi kuwa ni maneno ya kinabii.


  Alieleza kwaba kesho yake hakuna chombo cha habari kilichoandika habari hizo kutokana na kile alichosema ni kunyamazishwa.

  "Kesho yake baada ya Askofu kusema mambo hayo ambayo ni unabii wa taifa hili, hakuna chombo kilichoandika," alisema Pengo.Alisema kutokana na viongozi hao kuendelea kuziba watu midomo, sasa Mungu anatumia njia nyinge kufikisha ujumbe ili watu wake waweze kumrudia na kutubu kuokoa taifa lisiangamie.


  Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili kuhusiana na alichosema kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini wakati akimsimika Askofu mpya wa jimbo la Bunda, aliwataka viongozi wa kanisa hilo kusimama daima katika ukweli hata kama ukweli huo utagharimu maisha yao.Alisema litakuwa kosa kubwa kwa viongozi hao kukubalia kila jambo lililo kinyume na ukweli bila kulitolea neno lolote.


  "Simameni daima katika ukweli; liwalo na liwe. Ukiogopa kufa leo utakufa kesho. Ukiogopa kusema ukweli leo eti kwa kuogopa kufa utakufa kesho," alisema Kadinali Pengo.

  Kwa mujibu wa Pengo shinikizo linalolisababisha kanisa hilo kutoa wito wa kuwataka watumishi wake wasimame katika ukweli linatokana na hali ilivyo sasa katika jamii ya mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa madhehebu ya kidini na watendaji wa serikali.


  Kwa mujibu wa Kadinali Pengo, mgawanyiko huo umewafanya watu wanaoitakia nchi mema kushindwa kutimiza jukumu lao ipasavyo wakihofia kukosolewa na kundi jingine lililojijengea tabia ya kuona mapungufu tu hali inayowaumiza wananchi wa kawaida wanaobakia kuteseka kwakushindwa kupata huduma wanazostahili.


  "Katika hali hii ni vigumu kwa mtu kutenda mema wala kunuia mazuri, huzuka hali ya kuona mapungufu;hatuoni mema yanayotendwa au kunuiwa na kutendwa na sehemu nyingine,"alisema Pengo kwenye ibada hiyo ya kumsimika Askofu mpya ambayo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali.


  Kardinali Pengo aliwageukia viongozi wa serikali na kuwataka kushirikiana na wananchi na kusoma alama za nyakati ili waweze kukabiliana na changamoto zilizomo ndani ya kanisa na jamii kwa ujumla kabla ya kuamua chochote.

  Kauli ya kadinali Pengo iliungwa mkono na Askofu Thadeus Ruwaichi akisema kamwe Kanisa haliwezi kunyamaza bila kuwaambia waamini na watanzania kwa ujumla ukweli juu hali ya mambo ilivyo nchini.


  Alitolea mfano suala la umasikini uliokithiri miongoni mwa Watanzania ilihali nchi imejaliwa utajiri wa rasilimali nyingi na kwamba hilo ndilo jambo linalopaswa kuwekwa wazi na Kanisa hilo kwa waaminio na watanzania kwa ujumla ili wazitambue na kuzifanyia kazi kwa maslahi ya wote.


  Askofu Ruwaichi alienda mbali zaidi akisema kwamba Kanisa lipo tayari kushirikiana na watu wote ambao wanaitakia mema Tanzania bila kujali imani zao za kidini, itikadi zao za kisiasa, rangi zao wala maeneo wanakotoka ilimradi tu wanaweka maslahi ya taifa mbele.


  Source: Mwananchi Publications
   
 2. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nae kumbe ni pipoz pawa
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa watu shupavu kama hawa wanaoweza kupakua ukweli na uozo unaotokana na uvundo ndani ya serikali yetu.
  Kama uozo huo haupo kwa nini Kikwete hajatamka lo lote kuhusu siri zilizofichuliwa na week-leaks?
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  viongozi wa ukweli ndio hawa
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Ukweli una gharama yake bwana na wale wote walioufuata na kuusimamia kwa maisha yao yote walilipia gharama kubwa! Kwangu mimi Kardinali Pengo aanze kwanza yeye na wenzake ndani ya kanisa katoliki kwa kuusimamia na kuufuata ukweli kisha aende na nje pia kufanya hivyo hivyo.
   
 6. Mcmamo

  Mcmamo Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :hatari: MI BINAFSI kardinali namchukulia km mwana harakati kwani ni zaidi ya askofu wala astishwe na wahafidhina wa ccm ambao hawataki kukosolewa badala yake wanakimbilia matusi na kejeli asimamie ukweli bila kuogopa wa kumuogopa ni Mungu tu
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Angalia vyombo vya habari vinavyoshikishwa adabu siku hizi, vinachuja habari, vinachakachua habari ha vyombo vya habari vilivyokuwa kifua mbele kuleta bayana
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pia ni vizuri wanakuwa wakweli katika kuongoza waumini wao kwani hata hawa Makadrinali ni wananchi na raia wa Tanzania. Ni vizuri waongee kama kuna jambo zuri lijulikane kama kuna jambo baya tunakatiwa kujirekebisha waongee pia. Kanisa linaongoza waumini wengi na wote wanapitia maisha magumu sana kiuchumi kutokana na uozo wa uongozi wa Kikwete. Kukaa kimya kama hivi vitu havipo ni usaliti wa hali ya juu na Neno la Mungu siku zote linazungumzia "Ukweli na Haki" Today, we don't none of these.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Slaa, Mwakyembe watishiwa kuuawa

  • Membe, Mengi, Mwandosya nao wamo
  • IJP: Tuna taarifa hizo, tunachunguza
  • Sheikh Yahaya Hussein naye ahusishwa
  KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini, Dk. Willibrod Slaa ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotishiwa kuuawa. Mwingine aliye kwenye orodha hiyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, MwanaHALISI linaweza kuripoti.

  Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IJP), Said Mwema amethibitisha kuwa ana taarifa kuhusiana na tishio hilo na kwamba ofisi yake inazifanyia kazi. "Ni kweli, jeshi la polisi linazo taarifa hizo za kuwapo kwa tishio la mauaji. Lakini nafikiri hilo ni jambo la kiupelelezi zaidi," alisema IJP Mwema katika mahojiano yake na gazeti hili juzi Jumatatu.

  Hata hivyo, Mwema alikataa kulizungumzia suala hilo kwa undani, badala yake alielekeza gazeti hili kumtafuta Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishina wa Polisi, Robert Manumba. Naye Manumba alipoulizwa alikiri kuwapo kwa tishio hilo lakini aliishia kusema, "Bado tunafanya uchunguzi." Alipoulizwa hatua walizofikia katika uchunguzi huo, Manumba alisema, "Unapofanya uchunguzi kuna mambo mengi ya kuzingatia. Kuna kukusanya ushahidi. Kwa jumla, bado tunafanya uchunguzi," alisisitiza na kusema muda ukifika taarifa kamili itatolewa.

  Kufichuka kwa tishio la mauaji ya watu hao mashuhuri, kumeibuka kufuatia barua ya kurasa saba iliyoandikwa na Dk. Mwakyembe ambaye sasa ni naibu waziri wa ujenzi kwa IJP Mwema. Katika barua hiyo ya 9 Februari 2011, iliyobebwa na kichwa kisemacho, "Taarifa ya njama za kuondoa maisha yangu na ombi kwa jeshi la polisi kulinda haki yangu ya kikatiba ya kuishi," Dk. Mwakyembe anataja watu wengine mashuhuri wanaotishiwa kuuawa. Hao ni mfanyabiashara mashuhuri nchini, Reginald Mengi, waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Melecela.

   
 10. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Hii ni ishara wazi kabisa kuwa ukombozi Tanzania umewadia.
  Ukiona haki inapiganiwa kwa gharama yeyote ujue vilio vya
  watanzania vimesikika.

  Watu wanaumia, wamama wajawazito wanapata tabu, watu
  wanaishi kwa mlo mmoja, maji/umeme tabu, bei ya vyakula
  imepanda yaani ni chaos tupu.

  Mungu ibariki Afrika
  Wabariki Viongozi wake
  Hekima Umoja na Amani
  Hizi ni ngao zetu
  Afrika na watu wake.

  Ibariki Afrika
  Tubariki watoto wa Afrika.

  Mungu ibariki Tanzania

  Dumisha uhuru na Umoja
  Wake kwa Waume na Watoto
  Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.

  Ibariki Tanzania
  Tubariki watoto wa Tanzania.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tanzania na watu wake
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mroojr

  Mroojr Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kumbe je! Hali ngumu ya maisha ya watanzania ilikuwepo toka awamu ya kwanza na pengo alikuwepo lakini hakuwa na ukweli wa kupasua.Waliokuwepo,sukari mikate sabuni nguo hupati mpaka kwa foleni RTC na ukipata kwingineko jela kwa ulanguzi.Ilikuwa hali nzuri hajazungumzia leo mbaya anazungumza.Hebu acheni siasa makanisani na misikitini mtaipeleka nchi pabaya.Shauri yenu.
   
 13. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  "Human being is a political animal" kwa maana kwamba binadamu anaathiriwa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya kisiasa. Siasa inagusa nyanja zote za maisha hivyo viongozi wa dini kama sehemu ya jamii wana wajibu mkubw wa kuishauri serikali kuweka mambo sawa. Hali ya maisha inavyozidi kuwa ngumu ndivyo na maovu yanavyoongezeka kwenye jamii viongozi wa dini nao watazidi kuwa kwenye wakati mgumu kuwarudisha watu kwenye msitari ulionyooka..
   
 14. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Hebu tujikumbushe historia kidogo. Kipindi kile kulikuwa na:

  1. Oil Crisis
  2. Famine
  3. Cold War

  Haya mambo yalileta hali mbaya ya uchumi katika
  ukanda wetu, mfano kutokana na ukame akiba ya
  chakula ilipungua ndiyo sababu ya nyerere
  kuomba msaada wa chakula Marekani (mahindi ya yanga).

  Vile vile kutokana na oil embargo ya OAPEC
  iliyosababishwa na msaada wa marekani dhidi ya
  jeshi la israeli hali yetu ya uchumi ikadidimia. Kama
  unavyojua mafuta yakiadimika kila kitu kinapanda.

  Wakati mambo hayajakaa vizuri ikaja vita ya
  Kagera ambapo tulitumia zaidi ya dolari za
  kimarekani milioni 500 kupigana ($500,000,000).

  kumbuka ile vita tuliigharamia wenyewe kwasababu
  OAU walikataa kushiriki.

  Kuhusu athari za cold war nitaliacha kwa leo (kiporo).

  Hata hivyo watu walikuwa wanasoma bure (viongozi
  wetu wengi wa sasa walikuwa wanafunzi wa vyuo
  kipindi hicho), matibabu bure, umeme ulikuwa haukatiki
  hovyo na nchi ilikuwa na msimamo.

  Inabidi uisone historia ya inchi yako na dunia ili uelewe
  kwanini mambo yalikuwa hivyo.

  Hivi sasa mambo ni tofauti kabisa hakuna vita baridi,
  ukame, wala vita na nchi yeyote lakini wengi wanakiona
  sasa huoni kama kuna tatizo ndugu?
   
 15. M

  Mindi JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Baada ya watawala kupumua kutokana na vichwa vya habari kuhamia Loliondo, Pengo amerejesha tena maumivu kwa kushusha kombora hili. na amelishusha kwa hisia kali na nguvu zote. hii ni aina ya ngumi ambayo huwezi kuwa na majibu. inatoa elimu nzuri sana kuangalia ni magazeti yapi yameripoti habari hii. Hapo tena huwezi kuishangaa serikali pale ilipochukua hatua za kutoa onyo kali kwa gazeti la Mwananchi, kwamba linatoa upendeleo kwa habari zinazoikera serikali! Bravo Mwananchi! endelea kuonesha njia! tenda za kutangaza matangazo ya serikali zinaweza kupungua, lakini kazi yako tunaiona na Mungu akuwezeshe.

  Bravo pengo! tunahitaji watu wengi zaidi wa calibre yako watoe kauli kama hizi, ili watawala wasipate nafasi ya kuwakandamiza akina Dr. Slaa kwamba ni wachochezi. Suala la Amani ya Tanzania sio la CCM na serikali kuachiwa kufanya wanavyoona wao, bali ni la wananchi wote. wananchi wanayo haki na wajibu kutoa tafsiri sahihi ya nini hasa kinachovuruga amani yetu. kusema bila kuuma maneno kwamba HATUWEZI KUWA NA AMANI BILA HAKI
   
 16. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  viongozi wa dini wazidi paza sauti kulaani yote maovu yanayofanywa na viongozi wetu hapa nchini
  japo ni busara itumike kwan kuna hatari ya kuchanganya dini na siasa
   
 17. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,172
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 280
  Mwanangu hata mmbwa akikutangazia msiba ukimdharau kwa kuwa ni mnyama utakuta weshazika! ima mla kalaleo mla jana kala nini.
  Msikiti/Kanisa ni wadau wa siasa wote kwa nafasi zao ni waTg walio pewa haki hiyo na katiba ya nchi.
  Acha kuwa kipaza sauti cha mafisadi mwana angalia alama za nyakati.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kauli nzito.
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kama hakuna aliyepaza sauti kipindi kile haimaanishi sauti zisipazwe sasa kwa hali ilivyo...
   
 20. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HApo Hakuna Siasa KAnisani ila amesema kweli, viongozi wanatakiwa kufuata, kama kuna unaloona ni baya basi muhukumu kwa hilo, usilete propaganda.
   
Loading...