Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Ni katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Karibu!
Kardinali Pengo na Sheikh wa mkoa kwa niaba ya Mufti wanauombea mkutano huo.

Sasa viongozi wa dini wanaangalia mkanda wa video unaomuonyesha RC Makonda akitolea ufafanuzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

======

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kasi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo inayofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli inazidi maelekezo ya ilani ya CCM.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 18, 2019 katika mkutano wake na viongozi wa dini unaofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) ambako anawaeleza mambo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka minne.

Amesema kasi ya kiongozi mkuu huyo wa nchi ni kubwa kuliko ilani hiyo, kwamba amefanikiwa kwa kuwa amemtanguliza Mungu mbele.

Amesema uchapakazi huo ndio umewafanya watendaji wengine kumuiga.

“Kawafanya hata viongozi wa Serikali wanaotumia hirizi kumtaja Mungu kwanza. Mara nyingi ameweka wazi kuwa mambo yanavyokwenda kasi hata yeye mwenyewe anamshangaa Mungu,” amesema Makonda.

Amesema ameamua kukutana na viongozi wa dini ili kuwaeleza miradi inayotekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi
 
God Is Not Stupid

God will burn this people for their mockery over him....

Wait and see!!
Dr Malasusa wa KKKT, askofu Sosthenes wa Anglican, Kardinali Pengo wa Katotiki na shehe mkuu wa waislamu wote wa mkoa wa Dsm wamehudhuria mkutano huu wa kipekee!
 
Kuna wakati unaangalia Mapito inayopitia nchi kwa sasa unajiuliza yaani tumegeuka kuwa nchi ya kishamba namna hii kwa speed ya ajabu kwa nini?

Kweli Rais wa nchi ndio dira akiwa mchangamfu basi nchi inachangamka, mshirikina basi mwelekeo wa nchi unakuwa hivyo au MTU mwenye utu pia mnaenda mkondo huo.

Sasa awe mshamba! Lahaula! Hivyo ndiyo inakuwa njia yenu ya kufuata.
 
Kukutana na viongozi lazima iwe live! Awamu hii kutafuta sifa za kijinga kumezidi. Unakutana na watu live, wamekuwa bidhaa unataka kuzitangaza?

Hakuna mjadala wowote wa maana huwa unafanyika live.
Kinachokuuma tunakijua kamanda
 
Ni katika ukumbi wa Kimataifa wa mwalimu Nyerere.

Karibu!

Kardinali Pengo na shehe wa mkoa kwa niaba ya mufti wanauombea mkutano huo.

Mkoa wa Dar es Salaam hauhitaji Maombi dhidi ya Wanafiki, Watekaji na Wauwaji badala yake unahitaji Mikakati madhubuti ya Kuuendeleza na pia Kupambana na Changamoto mbalimbali za Kijamii. Nawaheshimu Viongozi wa Dini nchini Tanzania, ila naona kwa miaka ya hivi karibuni wanaanza ' Kutepeta ' Kimaadili, Kiimani na Kiutumishi ndani ya Taasisi zao huku wakianza taratibu ' Kutekwa / Kurubuniwa ' na Wanasiasa.
 
Lipi la maana unadhani tunaweza kulipata kutoka kwenye huo mkutano!!

Si bora huo muda wa coverage TBC wangeutumia kuwaweka wataalamu kutoka wizara ya kilimo au mifugo watufundishe namna ya kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo au ufugaji hata wa kuku kwa ubora ili kupunguza tatizo la ajira huenda wangepata hata watu 100 ambao wangethubutu sasa kila siku coverage zisizo na impact za nini

Wasteful of resources
 
Wahenga walisema usikatae wito, kataa neno. Kama hao watumishi wa Mungu bado wanaojitambua kuwa wao ni chumvi ya Ulimwengu basi wakatumie mkutano huo kutekeleza wajibu wao wa kitume. Mungu anawaona.
 
Kuna wakati unaangalia Mapito inayopitia nchi kwa sasa unajiuliza yaani tumegeuka kuwa nchi ya kishamba namna hii kwa speed ya ajabu kwa nini?
Kweli Rais wa nchi ndio dira akiwa mchangamfu basi nchi inachangamka, mshirikina basi mwelekeo wa nchi unakuwa hivyo au MTU mwenye utu pia mnaenda mkondo huo.
Sasa awe mshamba! Lahaula! Hivyo ndiyo inakuwa njia yenu ya kufuata.
Tunajua unaumia kamanda! Wewe endelea kumsifu Mbowe hapo ufipa
 
Back
Top Bottom