Kardinali Pengo amerudishwa kwenye website ya Jimbo Kuu la D'Salaam alikokuwa ametoweka hadi jana. Hongera JF kwa kusababisha hilo

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
Heshima kwa wana JF wote,

Jana jioni katika kupekua nikaona website ya Jimbo Kuu la D'Salaam ikionyesha maaskofu wawili yaani Jude Thadaeus Ruwa'Ichi ambaye ni Askofu Mkuu Mwandamizi na Eusebius Nzigilwa, Askofu Msaidizi.

Tena thread yenyewe inaonyesha Ruwa'Ichi ameshakuwa Askofu Mkuu wa D'Salaam na Kardinali Pengo hayumo kabisa kwenye website hiyo.

Nilipotatizwa na kukosekana kwa Kardinali Pengo nikauliza mtaani nikakosa majibu nikaja humu JF nikaanzisha thread, hii hapa,

(Nini kimepelekea Kadinali Pengo kuondolewa kwenye tovuti ya Jimbo Kuu la D'Salaam? - JamiiForums).

Nimefuatilia thread yangu na hatimaye dakika 20 zilizopita nimeona ile website wameondoa picha za Askofu Jude Thadaeus za Eusebius Nzigilwa na kwenye sehemu ya maaskofu Kardinali Pengo sasa amewekwa rasmi na wenzake hao wawili.

Hii maana yake Jimbo Kuu la D'Salaam limerekebisha kosa lake.

Nani kasababisha wajirekebishe? Ni sisi wote humu Jamii Forum tuliofukunyua suala hili na wote tuliochangia kuhoji na hatimaye tumepata ukweli.

Nani alikuwa anaptosha. Waliopotosha ni wote waliojitahidi kutunga sababu za uongo wakijifanya wanaujua ukatoliki na kuutetea kumbe ni upotoshaji uchwara.

Viva JF, Viva wachangiaji wa ukweli.
 
Thread yenyewe ilisema hivi"

(Nini kimepelekea Kadinali Pengo kuondolewa kwenye tovuti ya Jimbo Kuu la D'Salaam? - JamiiForums)

SOURCE: Website ya Jimbo Kuu la D'Salaam

Nimeshtushwa kuondoloewa kwa Kardinali Polycarp Pengo kwenye website ya Jimbo Kuu la D'Salaam.

Ukiisoma inaonyesha Jude Thadaeus Ruwa'Ichi ndiye Askofu Mkuu wa Jimbo hilo na Eusebius Nzigilwa ni Askofu Msaidizi.

Jamani nikumbusheni. Je, inawezekana Kardinali Pengo ameshaondolewa jimboni ni mimi tu ndiyo sina taarifa?

Je, kuna mjadala wowote humu JF kuhusu kuondolewa Pengo labda umenipita?

Wana JF naomba ufafanuzi maana mantiki sijaielewa.

Website hii hapa:

Archdiocese of Dar-es-Salaam – Roman Catholic

Waliotupotosha wakati sisi tunatafuta ukweli walisema hivi,

"Za kuambiwa changanya na zako".. J.K WA PILI..

Sent using Jamii Forums mobile app

Tangu mwishoni mwa mwaka jana,Ruwaichi aliteuliwa na pope kua askofu mwandamizi wa jimbo kuu la dsm.

Kua askofu mwandamizi kunampa mamlaka sawa na ya askofu mkuu wa jimbo na kua askofu mwandamizi ina maanisha yeye ndiye atakayechukua nafasi ya aliepo pindi aliyepo muda wake utakapoisha kwa kuzingatia umri wa kustaafu(miaka 75) au kustaafu kutokana na kushindwa kufanya majukumu sababu ya maradhi.

Pengo anakaribia umri wa kustaafu ama amefikia pia ni mgonjwa,kwa maana hiyo askofu ni Ruwaichi hivyo ndio imepelekea ulichokiona kwenye website.

Kwa ufahamu wangu mdogo,ndio hivyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tangu mwaka jana mwishoni walitangaza kua Rwaichi ni askofu mwandamizi wa jimbo la dsm,maana yake mda wowote anatepewa mamlaka kamili,.labda kama haukusikia hiyo ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikweli ulichoandika Pengo anatoka madarakani huo niutaratibu unafanyika kwaajili ya kumuidhinisha Ruwaichi kushika madaraka ya juu ktk Kanisa Katoliki Tanzania, wanaanza kumwondoa kwenye maamuzi ya kikanisa taratibu mpaka muda walioupanga ukifika basi atapumzika kazi nyingi za kikanisa na atabiakia nancheo cha Kadinali mstaafu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wataalamu wengine wa upotoshaji ni hawa,
Ndugu ilishatangazwa Pengo atapumzika na Rwaichi atachukuwa mahali pake, ila kuna baadhi ya mambo yanafanyika niyandani na yakiutawala/uongozi ambayo hayatangazwi. Yanafanyika kiutawala zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali la nini wakati unajua wazi Mwadhama Ruwaichi alishateuliwa? Kwani aliacha Mwanza kuja Dar kufanya nini kama si kuchukua nafasi ya Pengo? Na wewe bila shaka unajua afya ya Mwadhama Pengo nayo haiko vizuri saàana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
The archdiocese’s motherchurch and thus seat of its archbishop is St. Joseph’s Cathedral. The current Archbishop of Dar-es-Salaam is His Grace Jude Thaddaeus Ruwa’ichi. Maana yake yeye ndiye askofu mkuu wa Dar kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
SWALi HILI SIJATARAJIÀ LITATOKÀ KWA MUUMINI WA KIROMA

HATA TULIO NJE TUNAJUA ASKOFU JUDE NDIE MRITHI WA ASKOFU PENGO

NA KUTOKANA NA AFYA YAKE HATOWEZA KUENDELEA TENÀ NA MAJUKUMU YAKE......
MPWA HUYU ALIEULIZA SWALI ATAKUWA DINI YA ...KWA MROMAN WANAELEWA FIKA KINACHOENDELEA ..

Wapotoshaji wengine ni hawa,
Kumbe mkuu una majibu yako tayari ,maana umesema hujui,eumejulishwa hutaki kukubali.
Jibu alilokuoa jamaa ndo sahihi.

Sent using Brain
Alipowekwa kwnye website waumini hatukuambiwanalaf ni minor issuea hizi mkuu,
As long tunajua mda tu majukum yake yanapunguzwa taratibu na mrithi wake ypo tayari kitambo,No problem.

Sent using Brain
Kwa mujibu wa kanuni za Kanisa Katoliki Askofu wa Jimbo akitimiza umri wa miaka 75 anapaswa kumwandikia Askofu wa Roma (Pope) kumwomba kustaafu uongozi wa jimbo na hivyo kumpa nafasi kumteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo.
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo atatimiza miaka 75 mwezi August 2019 lakini kwa maoni yangu Vatican wameishateua mrithi wake ambaye ni Mkapuchini Askofu Mkuu Yuda Thadei Ruwaichi (Ofcap).
Kwa wafuatiliaji wa ukatoliki Tanzania hili lilitarajiwa. Haya ni maoni yangu. Niishie hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mk
Mkuu kumbe unamajibu unayo yataka na hutaki kueleweshwa,Wakatoliki wa jimbo la Dar asilimia kubwa tulikua tunajua Baba kadinali akifikisha miaka 75 atastaafu na anafikisha miaka hiyo August2019 na hata mwenyewe alishaongea huko nyumba,hata alivyokuja Luwaichi tulijua ndio atakua askofu mkuu wa jimbo ni taratibu tu zinazosubiriwa na mwezi wa august ufike kadinali astaafu
 
Nawashukuru Domaradzka na wenzako mliosaidia kuumbua mambumbumbu waliodandia ile thread kwa kukurupuka.


Wakati uzi huu unaandikwa alikuwa ameondolewa kwenye website

Umeangalia picha ya pili toka kushoto kona ya kushoto kwako? Ni nani huyo? kama kweli upo serious!
An

Dogo ingia kwenye list ya current bishops ndio uprove kama ameondolewa au lah? Mamlaka hayupo uwepo wa picha kwenye website kuna kipindi kwenye picha waliwekwa askofu nzigilwa na libena.. Hata kabla huyo ruwaichi hajaja, tusiwe na hisia hasi na kuleta vijimaneno tujiridhishe kabla ya taarifa.
Mbona kwenye list yupo nyie kuondolewa mnaangalia nini!?? Picha?
Kwa Mtazamo wangu naona hauko siliaz na Unachokisema.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom