Kardinali Laurence Sengo wa kanisa katoliki Congo amtaka kabila aondoke madarakani.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,198
6,416
Habari wadau.

Leo jijini Kinshasa kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki nchini Congo DRC ameitisha mkutano na waandishi habari na kumtaka Rais kabila aondoke madarakani ili kuheshimu mkataba wake na kanisa hilo lenye wafuasi wengi nchini humo.

Kardinali Laurence Sengo pia amelaumu waumini wa kanisa hilo kuuawawa juzi na maelfu kunyimwa haki yao ya kuabudu.

Serikali ya Congo imempinga kardinali huyo na kusema waliouawawa ni majambazi na vibaka waliokuwa wakipora ngawira kwenye maandamano.

Kardinali pia amesema serikali imeshindwa kuwaletea raia na taifa maendeleo na badala yake kabila na viongozi wenzie wanajilimbikizia Mali.
 
Kanisa hili ni kikundi cha siasa dhamira zao kuu ni kuitawala Dunia katika:
. Uchumi
. Dila
Akishika uongozi wa juu mtu wao niwavumilivu sana! Wanafumbia macho mambo mengi, akishika mwingine weee
 
Kanisa hili ni kikundi cha siasa dhamira zao kuu ni kuitawala Dunia katika:
. Uchumi
. Dila
Akishika uongozi wa juu mtu wao niwavumilivu sana! Wanafumbia macho mambo mengi, akishika mwingine weee
 
Kabila siyo rahisi kihivyo maana amepandikizwa hapo anapewa order .
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom