Karate ndio mchezo unaoweza kukuhakikishia safe self defense kwa zaidi ya 90%

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,120
Karate ni mchezo mtamu sana, na hautumii nguvu nyingi sana kama ndondi.

Ndondi haiwezi kukupa uhakika wa zaidi ya 50% katika suala zima la self defense.

Karate inakufundisha kila kitu even magic kama utabahatika kufikia level ya kuanzia mkanda wa blue.

Sema tu Bongo karate hailipi sana kwakuwa haina competition nyingi na watu hawaijui licha ya kuipenda sana.

Mcheza karate mwogope sana hata Kama yuko level za chini anaweza kukuvunja mgongo huku amerelax.

Mcheza karate mwenye mkanda wa njano (mwanafunzi mwandamizi) anaweza kumpiga star wa ndondi ambaye anashiriki ngumi za kulipwa.

Karate ni pana na ina matawi au mapigo tofauti kulingana na mvumbuzi au muasisi.

Vijana chezeni karate mtakuja kunishukuru.
 
Ucheze karate akati mtu ana bisibisi au kisu
Asa kisu na bisi bisi ni kitu gani mbele ya mcheza karate kuanzia yellow belt .??....labda Kama ulikua hujui ni kua...hivo visilaha watu wanafanyia mazoez kiukweli ukweli ..kwahyo mpumbavu mmoja au wawili wakija na kisu Yani ni Kama wamefata kufanyiwa mafunzo kwa vitendo kwa mcheza karate aliyeiva
 
Nawajua wacheza karate wawili walishambuliwa na watu wenye silaha, visu na nk.

Mmoja kasharest in peace baada ya kushambuliwa na wahun wenye silaha mwingine yupo nje kwa matibabu zaidi ya miez mitatu sasa kwa kushambuliwa pia.

So karate sio suluhisho kwamba ndio utaweza kujedefend kwa 100% msibeze wanaosema watu wanakushambulia na silaha km visu bisibisi. Timing nayo inamata.
 
Nawajua wacheza karate wawili walishambuliwa na watu wenye silaha, visu na nk.
Kwahiyo kisa wanacheza karate hata wakishambuliwa na watu 1000 wenye mavisu washinde
So karate sio suluhisho kwamba ndio utaweza kujedefend kwa 100%
Jamaa hajasema 100%
msibeze wanaosema watu wanakushambulia na silaha km visu bisibisi.Timing nayo inamata.
Bado karate itabaki kuwa Defense, defense hainamaana 100% unaweza kuwa na Ma Ak47 na ukashambuliwa na kuuwawa.
 
Nchi ina jeshi,askari polisi japo wanapenda sana dhulma wapo,ina migambo siku hizi kuna hawa SUMA-JKT wameachiwa mitaani wapo baadhi ya sehemu wakilinda halafu tena nikahangaike kukunja kunja viungo?

Kama ni mgomvi sawa ila kama unaishi kwa kufuata kanuni za kawaida sana za maisha hauhitaji vurugu zote hizi,usimdharau mwenzako ishi kwa kuheshimu watu unaweza kuingia kwenye kumi na nane za mtu mwenye silaha na mateke teke yako akakuvunja kiuno.
 
Back
Top Bottom