Karatasi za Uchaguzi Kuchapwa nje,Vigezo vya Kugawanya Majimbo Vyatajwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karatasi za Uchaguzi Kuchapwa nje,Vigezo vya Kugawanya Majimbo Vyatajwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Regia Mtema, Jan 23, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Karatasi za uchaguzi kuchapwa nje
  • Serikali haina uwezo wa kuzichapa

  na Shehe Semtawa


  [​IMG]
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutangaza zabuni kwa kampuni ya kimataifa kuchapa karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
  Taarifa za ndani ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka katika kikao walichoketi jana jijini Dar es Salaam viongozi wa vyama vya siasa na Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu zinadai kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika kuwa hapa nchini haiwezi kufanyika kazi hiyo.
  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Kiravu aliwaambia viongozi wa siasa kuwa si kweli kuwa mpiga chapa mkuu wa serikali ndiye atakayezichapisha karatasi hizo kama ambavyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo alivyoliambia Bunge mwaka jana.
  Marmo aliliambia Bunge kuwa kazi ya kuchapa karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu amepewa mpiga chapa mkuu wa serikali.
  Chanzo hicho kilisema kuwa Kiravu amekanusha taarifa hizo za karatasi za kura kuchapwa hapa nchini kwa kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kuteua kampuni ya kuchapisha karatasi hizo na mpaka sasa hawajatoa zabuni kwa kampuni ya kuzichapisha lakini wanatarajia kuitangaza kimataifa.
  “Alituambia nia ya NEC ni kutangaza zabuni ya uchapaji karatasi hizo ili waweze kupata kampuni ya kimataifa yenye uwezo wa kufanya kazi hiyo kwani mpiga chapa mkuu wa serikali hawezi kuifanya,” kilisema chanzo hicho.
  Wakati huo huo, NEC imekamilisha mchakato wa kuweka vigezo vitakavyotumika katika kuangalia upya mipaka na kugawa majimbo ya uchaguzi kwa madhumuni ya kutekeleza matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
  Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Omar Makungu alibainisha hayo jana kwenye mkutano huo wa tume na viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya taifa uliofanyika kwenye ofisi za tume hiyo.
  Alisema NEC imepewa mamlaka chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Ibara ya 75(4) ya kuchunguza mipaka ya majimbo ya uchaguzi kila mara na angalau kila baada ya miaka kumi.
  Aidha, Jaji Makungu alisema suala hilo ni moja kati ya mambo ambayo tume inakusudia kuwashirikisha viongozi wa kisiasa kupatikana maoni yatakayosaidia kuondoa manung’uniko ya mara kwa mara.
  “Mtakumbuka kuwa tume mara ya mwisho kufanya zoezi kubwa la kuchunguza mipaka ya majimbo na kugawa mapya ilikuwa wakati wa uchaguzi wa rais na wabunge mwaka 2005,” alisema.
  Alisema kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 na uchaguzi wa mwaka 2005, tume iliweza kufanya uchunguzi kwa kuangalia upya mipaka ya majimbo na kufanya mabadiliko machache katika majimbo husika kutokana na kuanzishwa kwa halmashauri mpya kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini.
  Akifafanua zaidi alisema vigezo ambavyo vitatumika katika zoezi la ugawaji wa majimbo ya uchaguzi ni pamoja na vilivyotajwa katika Katiba ya Jamhuri na vingine ambavyo vimeainishwa baada ya kufanya utafiti katika baadhi ya nchi za kusini mwa Afrika zikiwemo Msumbiji, Zambia, Botswana na Afrika Kusini.
  Jaji Makungu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni upatikanaji wa mawasiliano, hali ya kijiografia, idadi ya watu, mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu na hali ya uchumi.
  Vigezo vingine ni pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kugawanywa, mipaka ya utawala, jimbo moja lisiwe ndani ya halmashauri au wilaya mbili, kata moja isiwe ndani ya majimbo mawili na vingine. Jaji Makungu alisema NEC imeweka utaratibu ambao utafuatwa katika kukamilisha maombi, maoni au mapendekezo husika. Alisema maombi yote yatapaswa kuwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambapo yatajadiliwa katika vikao rasmi kisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa na mwisho wa kuwasilisha maombi au mapendekezo hayo itakuwa Februari 28.

  SOURCE:TANZANIA DAIMA

  Haya Wakuu,habari ndio hiyo. Hivi ni kweli hatuwezi kuchapa hizi katarasi za uchaguzi?ugumu uko wapi?what is the secret behind the scene?
   
Loading...