Elections 2010 Karatasi za Kura Zabadilishwa!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza mabadiliko katika karatasi ya kupigia kura .

Wananchi watakaopiga kura watapaswa kuweka alama ya vema kulia kwa mgombea wa chama anachokusudia kukichagua badala ya chini ya picha ya mgombea.

Kwa habari zaidi soma HabariLeo.

My take: Kwa nini kuingia gharama za kubadilisha karatasi za kupigia kura kwa kubadili tu sehemu ya kuweka alama ya vema kulia badala ya chini ya picha ya mgombea? Au mnielimishe wandugu hii itasaidia au kupunguza au kuongeza nini kwenye upigaji kura?
 
Sisomi habari leo la mafisadi....je, naweza kupata source nyingine
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza mabadiliko katika karatasi ya kupigia kura .

Wananchi watakaopiga kura watapaswa kuweka alama ya vema kulia kwa mgombea wa chama anachokusudia kukichagua badala ya chini ya picha ya mgombea.

Kwa habari zaidi soma HabariLeo.

My take: Kwa nini kuingia gharama za kubadilisha karatasi za kupigia kura kwa kubadili tu sehemu ya kuweka alama ya vema kulia badala ya chini ya picha ya mgombea? Au mnielimishe wandugu hii itasaidia au kupunguza au kuongeza nini kwenye upigaji kura?

Si ili zipatikane nyingi zilizoharibika? (Hasa zile zitakazokuwa zinaashiria ushindi kwa chama pinzani)
 
Kwa kweli huko ni kuwachanganya wapigakura na kuleta mparaganyiko usio kuwa wa lazima kabisa
 
hata waseme tupige kwa kuweka alama kichwani kwa mgombea bado mwaka huu JK kura hazitatoshaaa
 
Labda uchakachuaji ndiyo ushaanza kiaina ili kura zinazoharibika ziwenyingi na baadaye ziwekwe upande wa CCM!!
 
Back
Top Bottom