MAGALEMWA
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 6,413
- 4,882
Kwenye mjadala wa wasomi wa chuo kikuu DSM kuhusu tathmini ya uchauzi 2015 kuliibuka maswali kadhaa na tuhuma dhidi ya Tume ya Uchaguzi. Prof Chaligha alitoa maelezo na majibu manne kuhusu hilo kadhia. Kilichonigusa na kunikera toka wakati huo hadi sasa ni kama ifuatavyo.
1. Eti tume hutangaza matokeo yaliyowekwa sahihi za mawakala. Kwa bahati mbaya kama ni kweli ushahidi hautakiwa kuhojiwa po pote na kwa kweli hakuna ushahidi wa kuhoji hicho.
2. Karatasi za kupigia kura zina namba kwenye vishina SIYO KWENYE KARATASI INAYOTIWA TIKI NA KUWEKWA KWENYE SANDUKU LA KURA.
Hii ni kero ya aina yake na imefanywa hivi kwa sababu nilizoshindwa kubaini; inashangaza vyama havihoji.
Changamoto zilizopo
1. Unapiga kura kwa Imani kuwa utaratibu utaiheshimu kura yako. Kura zinakusanywa na vyombo vya dola kwenda kwa Mkurugenzi kujumuishwa. Inatokea tofauti. Tofauti hii inalazimu kuhesabu upya kura ambazo hazina namba kama iliyopo kwenye kishina.
2. Kwenye taarifa zinazoibuliwa kuna masanduku yenye kura zilizopigwa tayari hasa yakiwa kwenye magari ya vyombo dola.
3. Kila kwenye vituo vinavyolalamikiwa huwa kunatokea tofauti ya idadi ya kura (Kawe). Kuna hata mgombea alitutamkia kuwa wataiba asilimia 10 kwa hiyo tumpe kura nyingi hata wakiiba zibakie za kutosha.
4. Pamoja na hayo yote, mimi kama mpiga kura ni kama naweka kura yangu kwenye rehani ya kutoheshimiwa kwa mwanya huu wa uchakachuaji.
Kama mpiga kura nawaomba wanaothibitisha uhalali wa karatasi hizi waliangalie upya ikiwezekana namba iliyopo kwenye kishina iwepo kwenye karatasi ya kutumbukiza kwenye sanduku la kura. Hii itasaidia mawakala kubaini kura zinazotoka nje ya kituo wakati wa majumuisho.
Hili suala ni zito kwenye mazingira ya uadilifu uliokufa. Haya ni maoni na kero yangu kuhusu kura yangu kukosa usalama miaka yote.
Ninawaomba wanajamvi tushauriane kwenye suala hili maana linatia doa kwenye sanduku letu la kura. Kama kuna wenye vyama humu watuthibitishie kuwa wanaliafiki na usalama wa kura ukoje?
KIONGOZI AKICHAGULIWA KIHALI BARAKA ZA MUNGU ZINAKUWA JUU YAKE NA NCHI YAKE