Karata ya Urusi itaiimarisha kuwa Super power na kuidhoofisha USA na EU kiuchumi

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,562
15,906
Habari za Eid natumaini wazima wote.

Kama ilivyo ada katika jukwaa hili tunachambua masuala mbalimbali ya kimataifa kuhusiana hasa na suala la vita ya Ukraine na Urusi. Binafsi naona kama mpaka sasa na kama itaendelea hivi Urusi itakamilisha mpango wake wa kuwa na nguvu zaidi Duniani kiuchumi ,kijeshi n.k . Nasema haya kwa sababu zifuatazo.

1.Mpaka sasa Urusi amefanikiwa kuimarisha sarafu yake (Rubles) kwa kulazimisha nchi zote "unfriendly " kufanya biashara kwa pesa yake ( USD imepotezwa)

2. Hivi sasa Marekani na nchi za ulaya baadhi wanatuma fedha na silaha nzito nzito huko Ukraine. Kinachoendelea huko Ukraine Urusi anapambana kuteka depot za silaha kutoka Western na kuzichukua na nyengine anazilipua. Hapa faida anaepata ni mrusi na hasara kwa upande wa pili.

3. Soko la nishati kwa ujumla kuanzia mafuta , gesi na coal limeongezeka maradufu kwa nchi za India na China ambazo mahitaji yake ni makubwa hivyo kuzidi kuimarisha biashara ya urusi kwa nchi hizo.

Kwa uchache nikiweka katika mzani wa faida na hasara naiona Urusi ikinufaika zaidi na hii vita na nina predict kuna uwezekano wa vita hii kuchukua muda mrefu kutokana na faida inayopatikana though pia makampuni ya silaha kule marekani yameongeza faida maradufu baada ya kuuza kwa serikali silaha zinazopelekwa Ukraine.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Ninakupinga kwasababu mshirika mkubwa wa kukuza uchumi wa Urusi ni mchi za Eu na NATO.
Iwapo leo hii wanajadili kuacha kununua mafuta ya Urusi hadi kufikia June huoni kuwa ni hasara na anguko kubwa kibiashara?
Hao China na India anao kila siku.
 
Ninakupinga kwasababu mshirika mkubwa wa kukuza uchumi wa Urusi ni mchi za Eu na NATO.
Iwapo leo hii wanajadili kuacha kununua mafuta ya Urusi hadi kufikia June huoni kuwa ni hasara na anguko kubwa kibiashara?
Hao China na India anao kila siku.
India na China wameongeza asilimia ya manunuzi. Kuna punguzo la 2% mpaka 3% ya mafuta kwa pipa. Ukiwa mnunuzi biashara inawekwa mezani mna jadili bei ktk asilimia tajwa. EU WATAENDELEA KUNUNUA GAS KWA SALAFU YA URUSI, JAWANA UJANJA, HATA HAYO MAFUTA WAMEGAWANYIKA.
 
Ninakupinga kwasababu mshirika mkubwa wa kukuza uchumi wa Urusi ni mchi za Eu na NATO.
Iwapo leo hii wanajadili kuacha kununua mafuta ya Urusi hadi kufikia June huoni kuwa ni hasara na anguko kubwa kibiashara?
Hao China na India anao kila siku.
Watanunua kupitia kwa third party ambapo bei inategemewa kuwa ya juu zaidi na kuzidi kuziumiza nchi za Ulaya.
 
Ninakupinga kwasababu mshirika mkubwa wa kukuza uchumi wa Urusi ni mchi za Eu na NATO.
Iwapo leo hii wanajadili kuacha kununua mafuta ya Urusi hadi kufikia June huoni kuwa ni hasara na anguko kubwa kibiashara?
Hao China na India anao kila siku.
Inawezekana lakin kwa %ndogo sana za uwezekano. Kwasababu lazima pia tujiulize!

1. Kwann thaman ya dollar imeshuka?

2. Kwann mfumuko wa bei umeongezeka sana kwa nchi kama USA na UK? Kwasababu tunaambiwa mfumuko wa bei wa sasa nchini UK wa sasa, haujawah kutokea since 1982.

So kwa mantiki hii ni dhahiri kabisa urusi wanaongoza ushindi wa kiuchumi kwa sasa.

Sasa kama hao UK na USA ndo main contributor wa kukuza uchumi wa RUSSIA mbona wao ndo wanaporomoka kiuchumi badala ya RUSSIA.

Tuwekane sawa hapo kidogo.
 
Nitakujibu kwa Maneno Machache.

Endapo kweli Uchumi wa Marekani na Ulaya utaanguka kabisa na Kusambaratika,Basi Ujue pia Uchumi wa Dunia ndio utazikwa rasmi mpaka pale Uchumi wa Marekani na Ulaya utakapofufuka. Angalia Mifano;

1.Mwaka 1929,Kulitokea Mpasuko kwenye Mahitaji ya Bidhaa za Viwandani barani Ulaya na Marekani. Bidhaa za Viwandani vilikosa thamani kutokana na Uzalishaji kuwa Mkubwa Sana kuliko Mahitaji Nchini Marekani na Ulaya. Uchumi wa Marekani na Ulaya Uliyumba Sana Mpaka Bidhaa za Viwandani zikaanza kutupwa Baharini kwa kukosa wanunuzi. Matokeo yake,Kulitokea Mpasuko wa Uchumi Duniani Maarufu Kama THE GREAT ECONOMIC DEPRESSION(GED).

2.Mwaka 2008,Dollar ya Marekani na Sarafu ya Euro ziliathirika kutokana na Kodi kuongezeka Nchini Marekani japo lililopelekea Makampuni ya Ulaya na Marekani kupunguza Mzunguko wa Dollar. Matokeo yake,Kulitokea Mtikisiko wa Uchumi Duniani ambao ulipelekea baadhi ya Mataifa Kama China,India,Japani na Korea Kusini kupunguza Purchasing Power.

Kwahiyo Mzee baba,Marekani na Ulaya Ni Sawa na Boti ambayo tumeipanda Binadamu wote kwa Sasa,Hatuwezi kufurahia kwamba Boti izame ili kuwakomoa Ulaya na Marekani Bali Tutazama nao.

Kama Urusi TU Yenye Uchumi wa $ 1.7T kutengwa kwake Kiuchumi kunaitesa Dunia kwa Mifumko ya Bei,Vipi Ulaya na Marekani kwa Pamoja zenye GDP ya $ 40T Zitengwe Kiuchumi harafu ubaki Salama wewe Mkolomije?
 
Back
Top Bottom