karata ya urais ndani ya CCM-mawazo yangu


E

engmtolera

Verified Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
5,117
Likes
91
Points
145
E

engmtolera

Verified Member
Joined Oct 21, 2010
5,117 91 145
karata ya urais ndani ya CCM.
kwa upande wangu ndani ya CCM hawa ndio watakao weza kuingia ktk kinyang'anyilo hadi dakika ya mwisho ktk mwaka wa uchaguzi utakaokuja
1.Dr Magufuli
2.Dr Mwakyembe
3.E.Lowasa na
4.Dr Nagu
Na karata ikichezwa vizuri yafuatayo yanaweza tokea
1.kumpata mgombea wa urais mwanamke,lengo ni kuweza kubadilisha upepo wa siasa na kuhimiza ile kauri mbiu ya "wanawake wanaweza,kama wakiwezeshwa" na hii itavuta wapiga kura wengi hususani wakina mama ambao ndio wapiga kura haswa ukilinganisha na akinababa na vijana.na akina baba wenye ndoa zao nao watavutwa na akinamama kwa kuwashauri juu ya kuwaunga mkono ili nao wapate Rais mwanamke kama ilivyo ktk nchi nyingine za kiafrika

2.inawezekana akasimamishwa mpiga kazi,ambaye tayari wananchi wanaimani nae,anayeweza simamia sheria bila woga wala kuteteleka na huyu si mwingine ni Dr Magufuli,kwani wengi wanamwona kama ni jembe na ni mtu mwenye misimamo akifuatiwa na Dr Mwakyembe.
3.Labda kwa kuwa umaarufu nao unavutia watu kupiga kura,basi E.Lowasa anaweza kupata nafasi ya kuiongoza CCM ktk kinyang'anyilo cha urais dhidi ya vyama pinzani.

nikionacho sasa ni nafasi ya kumpata Rais mwanamke ni kubwa mno,kwani maandalizi yanaonyesha hivyo na tayari akina mama wengi wanalisubiri hili kwa hamu ili nao waonyeshe kuwa si wanaume tu,nao pia wanaweza kuongoza nafasi kubwa kama hii ya Urais.
Kura kwa kawaida ni siri,kura yangu pia bado ni siri,hadi hapo tarehe husika itakapofika,na nitafanya maamuzi ya kumchagua mtu na si chama.
 

Forum statistics

Threads 1,250,610
Members 481,419
Posts 29,738,686