Karata turufu kwa Chadema kunusuru ushindi wa kishindo ni hii hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karata turufu kwa Chadema kunusuru ushindi wa kishindo ni hii hapa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 10, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  Baada ya mbinu chafu za CCM kujulikana za kuwaandaa wapigakura kuyapokea matokeo yaliyo batili katika uchaguzi mkuu kwa kupitia vyombo vilivyokithiri kwa ufisadi vya REDET na SYNOVATE yenye kulenga kuonyesha upinzani bado ni dhaifu Tanzania wakati sivyo hivyo hata kidogo, ushauri wangu kwa Chadema ni kucheza karata turufu itakayolinda na kuheshimu matakwa ya watanzania walio wengi ambayo ni hii hapa:-


  a) Kuishinikiza NEC kuwarudishia wapigakura haki yao ya kimsingi ya kulinda kura zao ili zisije kuchakachuliwa kwa kurudisha utaratibu wa wapigakura kuwa mita 200 kutoka vituo vyao walivyopigia kura.

  Lengo ni kuwazuia mashushushu waliotapakazwa nchi nzima kuja kuchakachua matokeo kwenye vituo vya kuhesabia kura kwa kuwarubuni mawakala wao kwa maburungutu ya fedha.

  b) Kuwalipa mawakala wao wote badala ya kuwaachia zigo hilo wagombea ambao wengi wao ni hoehae.

  Gharama za kuwalipa mawakala wote ambao hufikia takribani ya watu 53, 000 kwa siku moja kwa shilingi 12, 000/= kila mtu, Chadema itatumia jumla ya Tshs 1.06 bilioni shilingi.

  BIla ya kufanya haya mawili Chadema itakuwa imetusaliti sisi wapigakura ambao tuna imani nao kuwa ni wakombozi wa Nchi hii kutoka minyororo ya utumwa wa CCM.

  Mabadiliko ya utawala yanahitaji wote tujitume lakini Chadema isitarajie wapigakura tutajituma zaidi ya kupiga kura kama hawatatuwezesha kuwasaidia kulinda kura.

  Kamwe hatuwezi kulinda kura kutoka majumbani ambako ndiko NEC inatuagiza twende kujisitiri wakati wao NEC na CCM wanatufanyizia mambo yao machafu machoni pa Mwenyezi Mungu...................DHULUMA
   
 2. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Yaani hamna imani ya wanajeshi wenu wa mstari wa mbele???

  I thought hamuaamini NEC. Sasa mnataka wapewe chance ya kuwalipa mawakala wenu si ndio kuwapa nafasi ya kuwahonga....

  .

  Wasaliti watakuwa CHADEMA ama wafuasi wake ambao wako mbele kupigia kelele mabadiliko lakini hawako tayari kuchanga gharama zake?? Hivi kweli katika mazingira kama haya ambayo wengi wanaamini ushindi huo wa kishindo kama usemao mtashindwa kuchangia UKOMBOZI hiyo Bilioni moja???

  Mabadiliko ya utawala yanahitaji wote tujitume lakini Chadema isitarajie wapigakura tutajituma zaidi ya kupiga kura kama hawatatuwezesha kuwasaidia kulinda kura.

  Ndio wana ukombozi mamboleo hawa.........
  Wakisema wenye jukumu la ulinzi na usalama mnasema wanatisha wapiga kura ninyi ndio tuseme mnahamasisha tu ama??
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Hivi wewe ni Mtanzania au mgeni? Unaongea kama mtu asiyejali mustakabali wa taifa lake. Watanzania WENGI wanataka mabadiliko. Wamechoshwa na CCM. Wamegundua mbinu zao za kuiba kura, na jinsi wanavyotumia vibaya vyombo vya dola. Wewe UNASHABIKIA uhuni na uhalifu huu?

  Mtatupiga bakora siku ya uchaguzi mkuu; mtatumwagia maji ya upupu; mtatutupia mabomu ya machozi. Lakini tutalinda kura zetu HATA KAMA MTATUJERUHI NA KUTUUA! Damu itakayomwagika itakuwa JUU YENU! Sisi hatutafanya fujo, NINYI ndinyi mliopanga kufanya hizo fujo. Mnaweka mazingira ya kuhatarisha amani!

  Mtalipwa kwa kila tone la damu litakalomwagika!

  Ole wenu!

  -> Mwana wa Haki
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu mmoja kanidokeza; Kuna watu wengi wanasupport chadema sana ila michango hawatoi; sasa haya yatawezekana vipi?
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Najua mnajua na msiojua mjue, na wengi watazidi kujua na hata CCM WANAJUA Kuwa CHADEMA IKO JUU. Habari ndio hiyo.
   
 6. K

  King kingo JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili nalo neno Mkuu inabidi tichange hizo hela kwanamna yoyote ile kama kweli tunataka mabadiliko
   
 7. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Omarlyse, kwa mara ya kwanza nakubaliana nawewe ktk kipengele kimoja tu!

  Muda umefika kwa viongozi wote na wagombea wote wa ticketi ya CHADEMA kuanza kuwaeleza wapiga kura kwamba, wana wajibu wa kuchanga pesa kwa ajili ya kuwalipa mawakala .... vinginevyo kura watakazoipatia CHADEMA zitapotea; kwani tunajua ccm ilivyojipanga kuwanunua kwa pesa yoyote ile hawa mawakala ili waibe ushindi.

  Ktk siku zilizobaki, tunashauri hili lisisitizwe kwenye mikutano yote ya kampeni.
  Na sisi tunaochangia humu kwa maneno tuongoze njia kwa kutoa michango yetu.
   
 8. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Idea ya kuchangia ni nzuri na lazima tukubali kuwa kuna gharama ya kuiondoa sisiemu madarakani. Hatuhitaji kulipa gharama ya kumwaga damu bali tutumie kidogo tulichonacho kutenda jambo jema. Mungu ni mwaminifu atatuwezesha kama kweli ndiyo mpango wake.

  Napendekeza viongozi wa chadema wajuwe kuwa watanzania wengi wanawaunga mkono kwa hali na mali, hivyo wasiogope kuweka kapu kila mkutano ya kampeni kuchangia gharama za uchaguzi huu kama sheria ya uchaguzi inaruhusu. Naamini watu watachangia tu japo kidokidogo! Sisi tuliopo mijini tuendelee kuchangia kwa msg(tuma Neno "chadema kwenda namba 155710) na akaunti za benki. Hatuhitaji watanzania wote milioni 40 ili kuleta mabadiliko ila nia ya wachache ambao hatutazimia mioyo ndio tutakaoleta haya mabadiliko. Tukumbuke hata uhuru wa nchi nyingi umeletwa na wachache siyo kila mtu alishiriki.
  Umati ninao uona kwenye mikutano ya Dr. Slaa unaweza kufanya jambo la kuishangaza dunia kwa kuchnagia hata zaidi ya gharama zinazohitajika. Tunaamini Chadema haina viongozi mafisidi hivyo pesa hiyo itatumika vizuri tu.
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mungu amesikia kilio cha watanzania. Mimi nina imani kabisa kuwa mwaka huu Mungu ataingilia kati kulinda kura za watanzania. Pamoja na jitihada zitakazofanywa na CHADEMA kuzuia wizi wa ccm lazima wananchi wenye imani na wapenda mabadiliko waombe na ikiwezekana kufunga kabisa ili wezi wa kura (ccm) waaibike mchana kweupe.
   
Loading...