Karani huelewi...mke mmoja na nyumba ndogo saba

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Karani mmoja wa sensa amevunjika mbavu baada ya kuangua kicheko cha nguvu alipokuwa katika harakati zake za kudodosa...Amemhoji mzee wa kaya kuhusu makazi vizuri kabisa.Baadaye alimhoji kama ameoa?...Mwenyeji alimjibu ndiyo. Karani alihoji tena...una watoto wangapi?...mwenyeji-ninao 7 wa kwanza anasoma form one...kutokana na idadi kubwa ya watoto ukilinganisha na umri wake Karani alihoji,una wake wangapi? ...Mwenyeji alipotaka kutamka mkewe akawa anasogea basi akawa anaonyesha Kidole GUMBA huku akichora 7 hewani...mkewe alipokuwa anakaribia zaidi basi Mwenye kaya alimvuta karani kuelekea upenuni huku kakunja sura...Karani huelewi nini?...Mke mmoja na nyumba ndogo 7 ebo!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom