Karamagi unangoja nini kujiuzulu?

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,182
1,890
Wakati wa sakata la zito kuhusu Buzwagi, viongozi wa serikali kuanzia rais, waziri mkuu na wengine kibao walizunguka nchi nzima wakitetea kwamba mkataba ni mzuri hauna shida. Sasa leo wanasema Takukuru kibogo inachunguza tena huu mkataba, mbona maigizo haya jamani? Soma chini hapa.

Lakini Karamagi hivi lazima uwe waziri? Jk hivi mpaka Karamagi afanye nini ndio utajuwa kwamba hatufai?

Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni miongoni mwa vigogo wa serikali wanaochunguzwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru). Taarifa za kuchunguzwa kwa Waziri Karamagi aliyesaini mkataba wenye utata wa machimbo ya dhahabu, Buzwagi, zilifichuliwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Philip Marmo.

Bila ya kutaja jina la Waziri Karamagi aliyesaini mkataba huo wa Buzwagi Februari 17, mwaka jana, Marmo aliujumuisha mkataba wa machimbo ya dhahabu katika eneo hilo kuwa miongoni mwa mambo yanayochunguzwa na Takukuru.

Waziri Marmo, alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM) ambaye pamoja na mambo mengine, alitaka kujua dhamira ya serikali katika kukabiliana na tatizo la kukua kwa rushwa, ambalo sasa limesababisha imani ya wananchi kupungua.

Tamko hilo la kwanza kutolewa hadharani na serikali, tangu hoja ya mkataba huo ilipohitimishwa kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa miezi mitano, linaweza kuibua ukinzani mkubwa wa hoja miongoni mwa wadadisi wa mambo.

Aidha, taarifa kwamba mkataba wa Buzwagi unachunguzwa na Takukuru, ni kielelezo kwamba, majibu yaliyotolewa na Waziri Karamagi wakati akijibu hoja binafsi ya Zitto Agosti 14 mwaka jana, kwamba mkataba huo ulikuwa hauna matatizo yoyote, hayakuiridhisha vya kutosha Takukuru au pengine serikali.

Kumbukumbu za 'Hansard' zinaonyesha kuwa, wakati akijibu hoja hiyo ya Zitto Agosti 14, mwaka jana, Karamagi alisema: "Kama nilivyolielezea Bunge lako tukufu wakati nahitimisha hoja ya makadirio ya matumizi ya wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Katika viambatanisho nilivyokupatia sasa hivi, vilevile nimeambatanisha na kauli yangu hii... Kwa kuwa maandalizi yote ya kusaini mkataba yalikamilika nikiwa ziara ndefu nchi za nje, niliona si busara kuhatarisha uwekezaji wa mradi huu, jambo ambalo lingeathiri maslahi ya taifa."

Siku hiyo, Karamagi alikwenda mbali zaidi kuhalalisha mradi huo kwa kusema, uamuzi wa kuingia mkataba huo ulihitajika kufanyika kabla ya Machi 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huo ingepotea.

Dk. Chegeni katika swali lake la jana, lililozaa majibu hayo ya Marmo, alisema suala la rushwa na ufisadi limechukua sura mpya siku za hivi karibuni, na kusababisha manung'uniko kwa jamii licha ya jitihada za kupambana nalo zinazoongozwa na taasisi hiyo nyeti.

Alisema, jitihada hizo hazijatoa dhamira thabiti ya kupigana kikamilifu na tatizo hilo, huku akihoji hatua zilizochukuliwa na serikali kutokana na kashfa za rushwa kubwa zinazohusisha taasisi kama Benki Kuu, mikataba ya madini na nishati.

Aidha, mbunge huyo alitaka kujua idadi ya watu waliofikishwa mbele ya vyombo vya sheria wakihusishwa na rushwa za aina hiyo.

Katika majibu yake, Marmo alisema licha ya baadhi ya wabunge wa upinzani kuibua tuhuma nzito za rushwa wakati wa kikao cha Bunge la bajeti mwaka jana, serikali tayari ilishaanza kuzishughulikia tuhuma hizo, hata kabla hazijatolewa na kambi ya upinzani.

Alizitaja baadhi ya tuhuma nzito ambazo Takukuru inazifanyia kazi kuwa, ni pamoja na mkataba wa ukaguzi wa hesabu za makampuni ya madini kati ya Alex Stewart Assayers na serikali.

Aliutaja mkataba mwingine unaochunguzwa na Takukuru kuwa ni ule wa uchimbaji wa dhahabu katika eneo la Buzwagi mkoani Shinyanga kati ya kampuni ya madini ya Barrick na serikali.

Mkataba mkubwa wa tatu unaochunguzwa na Takukuru, kwa mujibu wa Marmo, ni wa machimbo ya makaa ya mawe na mradi wa uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

"Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, inafanya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za serikali katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya Benki Kuu. Uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea," alisema na kuongeza kuwa, hadi hivi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kuhusu tuhuma hizo.

Kwa majibu hayo, Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (Chadema), alilazimika kusimama na kusema kuwa, kuna maelfu ya watu ambao leo hii wapo rumande wakisubiri kesi zao, huku upelelezi ukiwa haujakamilika.

"Kama wapo Watanzania ambao wameshafikishwa mahakamani na wapo rumande wakati upelelezi wa kesi zao haujakamilika, kwa nini hawa wakubwa wameachwa wapo nje wanatamalaki?" alihoji mbunge huyo aliyekuwa mstari wa mbele kuitolea kauli kashfa ya ufisadi ndani ya BoT.

Swali hilo la Slaa lilijibiwa na Waziri Marmo aliyesaidiwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Mary Nagu.

Dk. Nagu alisema serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa, upelelezi wa kesi unakamilishwa mapema ili watuhumiwa wasikae muda mrefu mahabusu.
 
Kuburi Anamfanyia nani? ...........
Wana muda mfupi sana wa kujitetea...
 
Kaw mujibu wa taarifa ya Dr. Mwakyembe, si karamagi tuu wa kujiuzulu, ni waziri mkuu na baraza lake lote la mawaziri linatakiwa lijiuzulu. Kwa uchache, Lowasa, Msabaha. Karamagi na Meghji, hawa ndio wahusika wakuu.
 
Karamagi anasubiri uteuzi wake utenguliwe na JK!!! teh teh teh....
Nasikitika sana kuona kwamba mtu mwenye level kama ya Karamagi anashindwa kujua kwamba anastahili kujiuzulu kwa maslahi ya Taifa kwa jinsi jina lake lilivyogubikwa na UFISADI wa kila namna.

Karamagi why don't you just get yourself out of that office in peace!?
 
To me ni common sense unapoona umeharibu then unastep down.
Huyu W/Madini ni kheri angengatuka tuu.
Issue ni kwamba ana back up ya JK ndo maana kiburi kimemjaa.
Mbaya zaidi anajiona yuko right si alishazoe ayo toka yuko Twiga Cement and nothing happened.
JK asipokuwa makini huyu jamaa atakuja kufanya ya ajabu zaidi ya haya as to him hakuna wa kumwajibisha.
 
Ila Mwal. 1995 tayari alisema EL sii mwadilifu- kwa hiyo sioni kipya hapa! Mwal. aliwafahamu!

Taabu sasa hivi hakuna mtu mwadilifu- kama Mwal. wa kukemea uteuzi hata kama kuna ushahidi wa anayeteuliwa kutokuwa mwadilifu!

Wazee tulio nao ni Macecela, Kingunge, Butiku, Mkapa, Mwinyi- hawana utashi wa kutosha kukemea rushwa kama Mwal.
 
Ila Mwal. 1995 tayari alisema EL sii mwadilifu- kwa hiyo sioni kipya hapa! Mwal. aliwafahamu!

Taabu sasa hivi hakuna mtu mwadilifu- kama Mwal. wa kukemea uteuzi hata kama kuna ushahidi wa anayeteuliwa kutokuwa mwadilifu!

Wazee tulio nao ni Macecela, Kingunge, Butiku, Mkapa, Mwinyi- hawana utashi wa kutosha kukemea rushwa kama Mwal.

Mkuu,

Mimi nadhani unakumbuka kwamba Mwl. pia aliwahi kusema kwamba mzee Malecela ni mhuni! Sasa sijui ameacha uhuni kiasi cha kukemea mafisadi?

Kauli ile ya Mwl. ilikuwa ni nzito sana.

Mkapa sihitaji kueleza kwani inajulikana amefanza nini tangu 1995 hadi 2005.

Mzee Kingunge ndio ana tabia naweza kusema kwa kiingereza "macho behaviour" ambapo mtu unaona watu wanafanza maduwanzi na unajifanya kama huwaoni vile!

Kwa hio hapa nampa alama angalau 60% mzee Mwinyi. Yeye nafikiri ameona akae atulie ale pensheni yake maana madubwana yanayotendeka katika nchi aliyoiruhusu kuwa na biashara huria ni mazito!
 
Ila Mwal. 1995 tayari alisema EL sii mwadilifu- kwa hiyo sioni kipya hapa! Mwal. aliwafahamu!

Taabu sasa hivi hakuna mtu mwadilifu- kama Mwal. wa kukemea uteuzi hata kama kuna ushahidi wa anayeteuliwa kutokuwa mwadilifu!

Wazee tulio nao ni Macecela, Kingunge, Butiku, Mkapa, Mwinyi- hawana utashi wa kutosha kukemea rushwa kama Mwal.

Mkuu,
Tatizo kubwa la wanasiasa wetu ni kujifanya kusahau mambo kwa haraka. Hata mwaka 2005 tulimwambia Kikwete kwamba Lowassa hafai kuwa katika baraza la mawaziri, achilia mbali kuwa waziri mkuu. Wao wakakazana kuwapaka matope Salim A Salim na Frederick T Sumaye bila huruma. Sasa kiko wapi?
Maonyo ya Mwalimu yatabaki kuwa sahihi tu kuhusu Lowassa!
 
Wanahamisha nawapa kazi ya kufanya wameshindwa kufanya kazi basi sasa nawapa kazi wafanye....Mods MOVE THIS THREAD OR RESIGN
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom