Karamagi Azua Mengine Tena...

mambo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
2,373
5,600
Karamagi azua balaa linginee

2007-10-10 16:51:47
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wakati sakata la kusainiwa kwa mktaba wa Mgodi wa Madini ya Buzwagi likiendelea kuzizima nchini kutokana na tuhuma wanazozitoa wapinzani kuhusu mkataba huo, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi anadaiwa kuzua balaa jinginee.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa
Waziri huyo ametoa idhini kwa kampuni moja ya madini kuendelea na uchimbaji katika eneo lenye leseni za wachimbaji wadogo na hivyo kuzua mapigano makubwa.

Inadaiwa kuwa vurugu hizo zimetokea huko Mahenge mkoani Morogoro kwenye eneo la mgodi ulikanao kama Epanko.

Taarifa zaidi zinadai vurugu hizo zilikuwa kubwa kiasi cha polisi kulazimika kumwaga kikosi chake kwenye eneo hilo ili kuweka mambo sawa.

Inadaiwa kuwa baada ya uamuzi huo unaodaiwa kuwa wa Waziri Karamagi kutolewa, wachimbaji wadogo na wananchi katika eneo husika walikuja juu na kujiingiza kwenye mapigano makali baina yao na wafanyakazi wa kampuni husika.

Hali hiyo ilizusha mapigano makali baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao walilazimika kumwaga risasi na kujeruhi vibaya wachimbaji wadogo wawili.

Imeelezwa kuwa baada ya tafrani hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo alilazimika kwenda haraka eneo hilo na kuwakuta wachimbaji wawili waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa hospitalini.

Wachimbaji hao wametajwa kuwa ni Lazaro Chalo na Issa Ramadhani, ambao wamefanyiwa upasuaji wa tumbo baada ya kutunguliwa kwa risasi na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Taarifa hizo zinasema Waziri Karamagi anadaiwa kutoa maamuzi yaliyoipa umiliki wa mgodi huo wa Epanko kampuni moja binafsi na hivyo kuwaacha wachimbaji wadogo wakijiona kuwa wamekosa chao.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa mgodi huo ulikuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu baina ya kampuni hiyo inayofanya utafiti wa madini na wachimbaji wadogo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inadaiwa amekiri kuwa uamuzi wa wizara ya Nishati na Madini wa kuwamilikisha kampuni hiyo eneo la mgodi huo unaleta utata.

Hata Mkuu wa wilaya ya Ulanga Dk. Rajabu Rutengwe naye inasemekana hakutoa kibali kwa kampuni.

SOURCE: Alasiri
HAYA WANAJF KABLA HAMJAMALIZA NA MTUHUMIWA KUNA HILI TENA....AM TIRED,
 
SOURCE: Alasiri POA!!!
 
Hii ni kampuni ya Hendry Nyiti swaiba ya EL
Inaitwa INTERSTATE MINGING CO.LTD
Hili siyo jipya Karamagi lazima hasaini huu mkataba kulinda kazi yake.
 
Jamani mimi naomba tu kuelimishwa ni Juzi tu tumeshuhudia Rais Joseph Kabila akimutimulia mbali waziri wake baada ya ajari kuzidi.

Inakuwa je Tanzania nchi yenye amani na kula mbivu(kwa wachache) tena tunakuwa na watu ambao kila siku wanasifika kwa mabaya? Tena hao ndio viongozi wetu wanawatetea kila kukicha kuwa wanafanya vizuri sana?

Mimi nimechoka kusoma news za Mzee, bussiness man wa madini mzee Karamagi. Au aliwekeza sana katika uchaguzi sasa anarudisha kwa fujo? Itabidi tutafute mbinu za kumsaidia hili awajibike kwa makosa yake.
 
Huku kwenye madini kushakua hakuna dili tena maana CSI investicagtors wako kila kona kuanzia mtoa fotokopi ofisini mpaka hawa maaskari wa JF ambao wako macho 24/7 kuchunguza mambo haya

Safi sana
 
Alasiri said:
Hali hiyo ilizusha mapigano makali baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao walilazimika kumwaga risasi na kujeruhi vibaya wachimbaji wadogo wawili.

Imeelezwa kuwa baada ya tafrani hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo alilazimika kwenda haraka eneo hilo na kuwakuta wachimbaji wawili waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa hospitalini.

Wachimbaji hao wametajwa kuwa ni Lazaro Chalo na Issa Ramadhani, ambao wamefanyiwa upasuaji wa tumbo baada ya kutunguliwa kwa risasi na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Haya ndio mambo viongozi wetu wanapendezwa kuyaona yakitokea, huwezi leo hii ukafikiria tumbo lako pekee wakati umepewa dhamana ya kuona WTZ wote wanafaidika na rasilimali za nchi. Tutaona mengi kabla ya mwaka kwisha.
 
Hii ni kampuni ya Hendry Nyiti swaiba ya EL
Inaitwa INTERSTATE MINGING CO.LTD
Hili siyo jipya Karamagi lazima hasaini huu mkataba kulinda kazi yake.

Henri Nyiti ana uhusiano fulani wa kikazi na Justin Nyari, au nakosea jama? Nimezisikia habari zake kwa kiasi fulani huyu. Hebu wenye nyongeza mtupatie tuunganishe vipande tupate kitu kizima!
 
Bro,
Ulikuwa una maanisha nini hapo? kwamba Alasiri sio gazeti au? tafadhali nitafurahi kupata ufafanuzi wako.

Usipoteze muda wako bure huwezi kupata ufafanuzi wowote wa maana kutoka kwa huyo jamaa nakuhakikishia.
 
Huyu EL jamani, mbona ndo mdudu anayemaliza hii nchi? kwenye richmond yeye, madini tena yumo na mengine mengi tusioyajua. Anatumia cheo hicho kufanya deal chafu tu. hakuna chema alichofanya. Nakupa onyo EL, hata kama unaona wananchi hatukufanyi kitu, kwa wale tunaomwamini Mungu tunajua your days are numbered, kilio cha waTZ Mungu anakisikia.Utaondolewa na kutupiliwa mbali usipoyaacha madhambi haya.
 
Yupo kwenu sasa.
 
Inasemekana Nazir Karamagi ana Hela hadi za kuweza kuisaidia Bajeti yote ya Tanzania kwa miaka kati ya 7 mpaka 10 na bado Chenji ikabaki ikatusaidia kununulia Bombardier za kutoka mwezini kwenda chini ya Bahari kwa kufanya shughuli za Kutukuka za Kitalii. Pesa kitu kingine Jamani!
 
Huyu EL jamani, mbona ndo mdudu anayemaliza hii nchi? kwenye richmond yeye, madini tena yumo na mengine mengi tusioyajua. Anatumia cheo hicho kufanya deal chafu tu. hakuna chema alichofanya. Nakupa onyo EL, hata kama unaona wananchi hatukufanyi kitu, kwa wale tunaomwamini Mungu tunajua your days are numbered, kilio cha waTZ Mungu anakisikia.Utaondolewa na kutupiliwa mbali usipoyaacha madhambi haya.
Mama weeeeeeeee
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom