mambo
JF-Expert Member
- Jun 11, 2007
- 2,373
- 5,599
Karamagi azua balaa linginee
2007-10-10 16:51:47
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wakati sakata la kusainiwa kwa mktaba wa Mgodi wa Madini ya Buzwagi likiendelea kuzizima nchini kutokana na tuhuma wanazozitoa wapinzani kuhusu mkataba huo, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi anadaiwa kuzua balaa jinginee.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa
Waziri huyo ametoa idhini kwa kampuni moja ya madini kuendelea na uchimbaji katika eneo lenye leseni za wachimbaji wadogo na hivyo kuzua mapigano makubwa.
Inadaiwa kuwa vurugu hizo zimetokea huko Mahenge mkoani Morogoro kwenye eneo la mgodi ulikanao kama Epanko.
Taarifa zaidi zinadai vurugu hizo zilikuwa kubwa kiasi cha polisi kulazimika kumwaga kikosi chake kwenye eneo hilo ili kuweka mambo sawa.
Inadaiwa kuwa baada ya uamuzi huo unaodaiwa kuwa wa Waziri Karamagi kutolewa, wachimbaji wadogo na wananchi katika eneo husika walikuja juu na kujiingiza kwenye mapigano makali baina yao na wafanyakazi wa kampuni husika.
Hali hiyo ilizusha mapigano makali baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao walilazimika kumwaga risasi na kujeruhi vibaya wachimbaji wadogo wawili.
Imeelezwa kuwa baada ya tafrani hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo alilazimika kwenda haraka eneo hilo na kuwakuta wachimbaji wawili waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa hospitalini.
Wachimbaji hao wametajwa kuwa ni Lazaro Chalo na Issa Ramadhani, ambao wamefanyiwa upasuaji wa tumbo baada ya kutunguliwa kwa risasi na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Taarifa hizo zinasema Waziri Karamagi anadaiwa kutoa maamuzi yaliyoipa umiliki wa mgodi huo wa Epanko kampuni moja binafsi na hivyo kuwaacha wachimbaji wadogo wakijiona kuwa wamekosa chao.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa mgodi huo ulikuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu baina ya kampuni hiyo inayofanya utafiti wa madini na wachimbaji wadogo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inadaiwa amekiri kuwa uamuzi wa wizara ya Nishati na Madini wa kuwamilikisha kampuni hiyo eneo la mgodi huo unaleta utata.
Hata Mkuu wa wilaya ya Ulanga Dk. Rajabu Rutengwe naye inasemekana hakutoa kibali kwa kampuni.
SOURCE: Alasiri
HAYA WANAJF KABLA HAMJAMALIZA NA MTUHUMIWA KUNA HILI TENA....AM TIRED,