Karamagi adai Bilioni 10!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Hatimaye Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Nazir Karamagi amewasilisha rasmi nia yake ya kufungua mashtaka dhidi ya Dr. Slaa na mwanasheria Tundu Lissu kwa madai ya kumchafulia jina na kumtuhumu mambo kadha wa kadha. Kwa kutumia mawikili wake wa kampuni ya FK Law Chambers ya jijini Dar Bw. Karamagi amewataka Dr. Slaa na Bw. Lissu kumuomba radhi ndani ya siku mbili tangu kupatiwa notisi hiyo na kuchapisha maombi hayo ya msamaha kwenye magazeti makubwa yachapishwayo kila siku. Katika barua hiyo ambayo KLH News imeiona, Bw. Karamagi anadai fidia ya Shilingi Bilioni kumi pamoja na msamaha ambavyo vitamaliza jambo hili nje ya mahakama. Malipo ya bilioni kumi yalitakiwa yalipwe ndani ya siku saba tangu siku ya barua.

Kinyume cha hapo, Mawakili hao wamesema kuwa:

"We are under further instructions to notify you, as we here by do, that our clients intends to institute a suit against you for defamation and recovery of compensation in connection with the said offensive utterances if within the time stipulated above you fail or refuse to heed to any of the demands set above"

Barua hiyo pia inatishia kuchukua hatua nyingine za kisheria ambazo Mhe. Karamagi anaweza kuzitumia. Barua hiyo inamaliza kwa kusema kuwa

"It is our sincere expectation that you will heed to these demands without forcing us to resort to the costly and time consuming court action at your peril at to costs and other consequences"

Barua hiyo iliandikwa tarehe 24 Septemba 2007.
 
Mkuu Mwanakijiji heshima kwako,
Mbona habari hii haijaripotiwa kwenye vyombo vya habari vya huku nyumbani?I mean mpaka jana Ijumaa hakukuwa na taarifa zozte isipokuwa tu kwamba Karamagi yuko Lindi kwenye ziara ya "Uzuri" wa bajeti na huko eti akatoa mipira 3 "kuendeleza michezo".

Hao FK Chambers in watu waadilifu sana kwa ninavyofahamu,ssa kama na wao wanaingia kuwatetea mafisadi,mmhhh....
 
Siku 7 zimeshapita vipi amepatwa na kigugumizi gani? Au kufungua mashtaka nako ni confidential?
 
labda wanasubiri wachague "special jury" kwa kesi hii,si unajua tena mabo ya bongo...
 
Hivi huyu karamavi anafikiri kuwa kila mtu ni fisadi na anaweza kupata shilingi bilioni kumi kama yeye fisadi?

Na je?kuweka hati hii humu kisheria hali itakuwaje?
 
Tusubiri tuone kesi yenyewe kama kweli wataweza kwenda huko kwa pilato.

Huyu FK law chambers ni credible sana, nashangaa hawa kutetea ufisadi kwani hata kama ni pesa waangalie wasije kujikuta kama Mkono na pesa zake chafu za BOT.

Huyu waziri ajiuzulu ili kesi iweze kuwa fair kwani kwa cheo chake anaweza kuinfluence maamuzi ya mahakama.
 
MK,FK Law Chambers sio mtu mmoja bali ni watu wengi,mmojawapo ni Professor Luoga bingwa wa sheria za kodi na mhadhiri pale UDSM,IGP mstaafu Harun Mahundi,Jaji Mstaafu Dan Mapigano na bwana mmoja anaitwa Kibuta Kibwana (ambaye inasemekana ni kati ya majority shareholders wa GTV)...ila kwa ujumla hao wote ni watu WAADILIFU kwa ninavyofahamu,sasa kama na wao wameingia katika kumtetea Karamagi,nasindwa kupata picha kabisa...
unaweza kuwacheki online katika www.fklawchambers.net
 
Kama anadai fidia ya billioni kumi ina maana ana mafungu ya kutisha.
Alafu kuna watu wamemshauri ya kuwa asipoenda mahamkamni watu watazani kuwa ni kweli ameitumbukiza nchi pabaya ni mkataba wa ajabu.
Mtaona sasa kama iyo kesi itaendelea,nguvu ya soda tuu iyo lengo ni kuwapiga jamba jamba akina Slaa na Lissu wauchune.
Slaa and Tundulisu keep it up
 
Napata hofu jinsi ambavyo law chamber zetu zinavyoweza kuchukua fedha chafu , mkono na BOT na FK na BUZWAG, IMMA advocate na mikataba ya makampuni feki ya kufanya money loundering.Nani kabakia msafi?
 
Karamagi yeye ana bilioni kumi za wizi pale kitengo cha Makonteina, anafikiri na wengine ni wezi pia?

Aende tu mahakamani na akaumbuke zaidi
 
Ni mchezo wa kuigiza. Guess what next...ndio itakuwa njia ya kukwepa kujibu maswali, kwani suala lipo mahakamani na kulizungumzia itakuwa ni sawa na kuingilia uhuru wa mahakama. Na suala hilo litakuwa huko kwa muda mrefu kama kesi ya Mrema na milioni 900.
 
Akienda mahakamani basi kinyesi kitakuwa kimegonga panga boi, kwani kitamrukia kila aliye ndani ya chumba hicho. Natumaini tutasikia mengi hata yale tusiyotegemea kuyasikia.
 
Hatimaye Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Nazir Karamagi amewasilisha rasmi nia yake ya kufungua mashtaka dhidi ya Dr. Slaa na mwanasheria Tundu Lissu kwa madai ya kumchafulia jina na kumtuhumu mambo kadha wa kadha. Kwa kutumia mawikili wake wa kampuni ya FK Law Chambers ya jijini Dar Bw. Karamagi amewataka Dr. Slaa na Bw. Lissu kumuomba radhi ndani ya siku mbili tangu kupatiwa notisi hiyo na kuchapisha maombi hayo ya msamaha kwenye magazeti makubwa yachapishwayo kila siku. Katika barua hiyo ambayo KLH News imeiona, Bw. Karamagi anadai fidia ya Shilingi Bilioni kumi pamoja na msamaha ambavyo vitamaliza jambo hili nje ya mahakama. Malipo ya bilioni kumi yalitakiwa yalipwe ndani ya siku saba tangu siku ya barua.

Kinyume cha hapo, Mawakili hao wamesema kuwa:

Barua hiyo pia inatishia kuchukua hatua nyingine za kisheria ambazo Mhe. Karamagi anaweza kuzitumia. Barua hiyo inamaliza kwa kusema kuwa

Barua hiyo iliandikwa tarehe 24 Septemba 2007.

Huyu ana mtindio wa ubongo.Anajua watanzania tunamdai kiasi gani? watukuu wetu na vilembwe,vilembwe kazi vinadai.Anajua hilo huyu Karamagi.

Hivi jamaa ana familia kweli?? alafu inawezekana kafunga Ramadhan

Hajamaliza madeni yetu Watanzania anaanza kuyeyusha kwa "kuwadai" Dr Slaa na Lissu.
 
Kwa sababuba Tindu Lisu na Slaa walionyesha ushujaa kutuwakilisha sisi washikadau katika kilio chetu cha umasikini. Wakati umefika kuwaunga mkono ktk hili, hasa kwa hali zaidi kimali.

Nitafurahi sana kumwona Karamag mahakamani, kwani wengi watatakiwa kutoa ushahidi jinsi wanavyotulia mali zetu. Mkapa aliwatuma wenzake kushtaki kesi ya million mia tisa. Mrema akashinda hakuna aliyeshika bango kina Mkapa kujiuzulu na kwenda jela.

Safari hii tutashika mabango mpaka yatuue, kwani ninauhakika tutashinda kirahisi sana. Mwisho wa kesi hii ni kuanguka kwa serikali ya Kikwete na CCM kwa kiasi kikubwa sana. Tumwombe Mungu Karamag aende mahakamani...
 
kidume ni hivi,,kile kitengo cha kopntena pale bandarini huyu bwana an share asilimia 60,zingine wenye shida ndio wamechangia,,
huyu ndie bwana bunzwagi wa karamagi
 
je mnajua kuwa wanataka kupitisha sheria mpya ya kuhusu kashfa?? mnakumbuka ya takrima???

na kwa nini waende spidi hivyo?? kama watazuia watu wasiseme basi mawe yatazungumza... (shaaban Robert)
 
SASE BOSA!!!

Muda wa FISADI kujikaanga kwa mafuta yake mwenye umefika.
Haombwi msamaha Mtu! Wala mtu halipwi fidia ya hata senti moja ya mkoloni.

Niko Tayari kuchangia hivi $$$ vidola vyangu kwa akina Dr Slaa na Tundu Lisu hadi ushindi.

Huyu Karamagi ni lazima amulikwe na Spot Light ili asije ipa serikali kazi ya kuwalipa Wanasheria wake.

Masikini hajui atendalo.
Kesi ikianza ndo atajua uwezo wake wa kuficha mambo yake yasijulikane ni mdogo kiasi cha kuwa na uwezo wa kuficha mambo yake na mkewe chumbani tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom