Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Hatimaye Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Nazir Karamagi amewasilisha rasmi nia yake ya kufungua mashtaka dhidi ya Dr. Slaa na mwanasheria Tundu Lissu kwa madai ya kumchafulia jina na kumtuhumu mambo kadha wa kadha. Kwa kutumia mawikili wake wa kampuni ya FK Law Chambers ya jijini Dar Bw. Karamagi amewataka Dr. Slaa na Bw. Lissu kumuomba radhi ndani ya siku mbili tangu kupatiwa notisi hiyo na kuchapisha maombi hayo ya msamaha kwenye magazeti makubwa yachapishwayo kila siku. Katika barua hiyo ambayo KLH News imeiona, Bw. Karamagi anadai fidia ya Shilingi Bilioni kumi pamoja na msamaha ambavyo vitamaliza jambo hili nje ya mahakama. Malipo ya bilioni kumi yalitakiwa yalipwe ndani ya siku saba tangu siku ya barua.
Kinyume cha hapo, Mawakili hao wamesema kuwa:
Barua hiyo pia inatishia kuchukua hatua nyingine za kisheria ambazo Mhe. Karamagi anaweza kuzitumia. Barua hiyo inamaliza kwa kusema kuwa
Barua hiyo iliandikwa tarehe 24 Septemba 2007.
Kinyume cha hapo, Mawakili hao wamesema kuwa:
"We are under further instructions to notify you, as we here by do, that our clients intends to institute a suit against you for defamation and recovery of compensation in connection with the said offensive utterances if within the time stipulated above you fail or refuse to heed to any of the demands set above"
Barua hiyo pia inatishia kuchukua hatua nyingine za kisheria ambazo Mhe. Karamagi anaweza kuzitumia. Barua hiyo inamaliza kwa kusema kuwa
"It is our sincere expectation that you will heed to these demands without forcing us to resort to the costly and time consuming court action at your peril at to costs and other consequences"
Barua hiyo iliandikwa tarehe 24 Septemba 2007.