Karagwe: Mkuu wa Wilaya aamuru kijana wa miaka 12 ashikiliwe na Jeshi la Polisi kwa kosa la kupandisha bendera ya Canada kwenye makazi

Labda DC alichanganya alifikiri ni bendera ya CDM
bendera ya cdm kwa mbali kweli waweza ifananisha na ya canada. hata hivo nahisi habari hii ni fake, hakuna kiongozi hata WA ngazi ya kata anae weza amuru mtoto awekwe ndani.
 
Kuna makosa ambayo mtoto chini ya miaka 12 hawezi kushtakiwa nayo, na hawezi kufungwa (anakua na kinga). Ni sawa na mtoto wa chini ya miaka 8 hata akiua (murder) hawezi akafungwa ana kinga ya umri.

Pili, huyo mkuu wa wilaya hana hekima wala busara wala taaluma ya utawala bora, mtoto kama huyo kwa kosa hilo anapaswa kukemewa tu, ingetosha kujirekebisha.

**Na kuna madhara gani kuweka bendera kama hio ya Canada kwenye mti (ukizingatia alieweka ni mtoto, ambae anaweza akawa hata SHABIKI tu wa hio nchi, au pengine hata haijui hio nchi ilipo duniani wala kuandika jina lake halijui)???

**Unamjenga vipi mtoto huyo ki mapenzi na nchi yake kwa kumweka ndani???

**Unamuandalia mazimgira gani kisaikolojia akikua (kama umri huo usha mtengenezea CV ya kuwahi kukaa rumande)???

NB Tatizo kupewa madaraka bila kua na utiifu wa sheria, uongozi na utawala bora. Unafanya vitu kwa mazoea sio kwa kufata sheria za nchi.
Jibu swali, kupandisha Bendera ya nchi nyingine ni kosa kisheria?
 
Embu weka sawa kwahiyo ilikua ni safari rasmi na operation ya kijeshi kwenda kumkamata kijana huyo, na kuna fununu kwamba alitaka kupindua nchi ama
 
Jibu swali, kupandisha Bendera ya nchi nyingine ni kosa kisheria?
Najua sheria kuliko unavyo fikiria, tatizo muda wangu unathamani sana kuupoteza kujibu swali la kipuuzi kama hilo lako.

Labda cha kukusaidia kufungua akili yako,

Tafakari, na jibu lako utalipata ukijiuliza "Mbona hoteli nyingi zinapandisha bendera zaidi ya 5 za nchi tofauti? Na hakuna aliewahi kuzuiwa wala kukamatwa".
 
Najua sheria kuliko unavyo fikiria, tatizo muda wangu unathamani sana kuupoteza kujibu swali la kipuuzi kama hilo lako.

Labda cha kukusaidia kufungua akili yako,

Tafakari, na jibu lako utalipata ukijiuliza "Mbona hoteli nyingi zinapandisha bendera zaidi ya 5 za nchi tofauti? Na hakuna aliewahi kuzuiwa wala kukamatwa".
Kwanza swali halikutoka kwangu, badala ya kumjibu unanipa maelezo mimi bila ya kujua nipo wapi na ninani.
Anyway, siku zote anayejua sheria huongelea kile kilichopo mbele yake na si vinginevyo, pia hujizuia kuwa na jazba na hasira ili asitoke nje ya hoja kirahisi.
Asante.
 
Nasisitiza tena, huyu mtoto afungwe hata miezi 6 kwa kosa la kuidhalilisha nchi yetu. Hapa ni Tanzania unataka kuwa Mcanada hamia huko, hatutaki ujinga sie. Tanzania kwanza wengine baadaye, hutaki hama nchi.
Utakuwa na position gani iwapo ukija sikia mtoto wa miaka 12 anaombwa msamaha?
 
Back
Top Bottom