Karagwe: Katibu mwenezi wa CHADEMA Nurubet Bakaishumba, ajinyonga kwa kutumia Katani

Inasikitisha! Katibu Mwenezi Wa Chadema Akutwa Amejinyonga Kwa Kutumia Kamba Ya Katani Kwenye Mti.



Katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia naMaendeleo Chadema katika kata ya Igurwa Wilayani Karagwe mkoani Kagera amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani huku sababu za kujinyonga zikiwa hazijafahamika.

Akizungumza katika eneo la tukio Diwani wa kata ya Igurwa Bwana WILBAD ABDALA amesema kuwa katibu huyo NURUBET BAKAISHUMBA (35) ambaye pia alikuwa mjumbe katika serikali ya kijiji cha Bwera amekutwa amejinyonga kwenye mti jilani na nyumba yake.

Amesema kuwa mwili wa marehemu umegunduliwa na baadhi ya wanakijiji july 20 mwaka huu huku akiacha ujumbe wa maandishi unaoeleza kuwa familia yake haihusiki na kifo chake na kumtaka mke wake atunze watoto aliowaacha na kuonesha mali zake zilipo

Bwana Abdala amesema kuwa ujumbe huo aliouacha marehemu amesema kuwa uamuzi huo wa kujinyonga ni wake mwenyewena kwamba wazo hilo alikuwa nalo kwa muda wa mwezi mmoja.

Kwa upande wake katibu wa Chadema Wilaya ya Karagwe bwana AMON MINYANGO amesema kuwa chama hicho kimepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika maendeleo ya chama hicho ulikuwa mkubwa.
 
Kujitoa uhai kwa sababu yoyote ile ni upuuzi na ukomo wa akili kufikiria! Kila tatizo lina mlango wa kutokea ni kosa kukata tamaa mapema kwa maana huko ni kukimbia majukumu!
 
Hivi kwanini watu hupenda kusema "amejinyonga", kwa uchunguzi upi uliofanyika? je, kama kanyongwa nani anajua zaidi. Wosia kila moja anaweza kuandika kwa niaba! mfano mzuri ni yule aliyemchoma mkewe na akawa anatumia namba ya mkewe kutuma sms
 
Naona uzi huu wale waliyokuwa na flat-screen wamepata kalio kubwaa

Ova
 
Back
Top Bottom