Karagwe inayosifika kwa kulima Kahawa Nchini lakini haina kidato cha tano na sita! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karagwe inayosifika kwa kulima Kahawa Nchini lakini haina kidato cha tano na sita!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaligoma, Aug 8, 2011.

 1. K

  Kaligoma New Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimeuliza swali hili kwa machungu makubwa sana, wakulima wa karagwe pamoja na kuangaika katika kuudumia kahawa, hawapewi chochote mfano pembejeo za kilimo, lakini pamoja na kuhudumia kahawa wenyewe baada ya kupata kahawa hiyo wanapangiwa kahawa na Serikali.Hapa karagwe kilo moja inauzwa wastani kwa shs.1400 wakati kwa Nchi ya Jirani Uganda ni TShs.2500-3000/=
  Ukichunguza kwa umakini kweli hakuna jitihada za kumsaidia mkulima wa jembe la mkono.

  Cha kusikitisha wilaya nzima pamoja na juhudi nzima za serikali za kuimiza kilimo kwanza, Hakuna hata treckita moja au power tiller moja iliyogawiwa kwa wakulima.
   
 2. K

  Kaligoma New Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inashangaza kuona wilaya inayosifika kwa mapato makubwa kutoka katika zao la Bihashara la Kahawa inakosa shule ya Serikali ya kidato cha tano na sita.

  Wilaya ya Karagwe inasifika sana kwa kuwa na hali ya hewa nzuri nawatu wake kuwa wapole sana ila cha kushangaza sana watu kuchulia upole wa watu hawa kutowasaidia kabisa.
  Pamoja na Jitihada za serikali katika ujenzi wa shule za secondari za kata hakuna anayejishughulisha katika uanzishwaji wa kidato cha tano nasita,
  Watendaji wanashangilia kuona shule binafsi zinaanzisha kidato cha tano na sita.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwan kulima kahawa ndio kigezo cha kuwa na kidato cha 5-6,???
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kuna kaujinga fulani kwa watu wa Karagwe. Bei ya mazao inapopanda nchi jirani ya uganda, wanazuiwa kupeleka huko, Kwa mfano juzijuzi wamezuia mahindi, maharage yasivushwe mpakani lakini serikali hiyo hiyo haiwaonyeshi wakulima mnunuzi mbadala tena mwenye bei nzuri. Kuna wakati wanazuia hata ndizi wakati hawaaonyesi teknologia ya kuzihifadhi.
  Tafakari - chukua hatua!
   
 5. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hata tandahimba iliyoingiza bilioni 53 kupitia zao la korosho msimu 2010/2011 haina advanced secondary
   
 6. k

  kajunju JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  karagwe wajilaumu wenyewe.matatizo mengi ya karagwe yanasababishwa na uongozi wa karagwe.ikifika kipindi cha uchaguzi watu wanaongwa rubisi wanachagua bora liende.mtu wa kulahumiwa saana karagwe ni sir george kahama.licha ya kuwa waziri wa ushirika hakuwasaidia wananchi na yeye ndiye aliwadhibiti ili kahawa isipate soko. maswali ya kujiuliza je, ndiye mmiliki wa viwanda vya kahawa???mbunge wa kyerwa katagira ndiye mwenye kiwanda cha kukoboa kahawa pale rugalama. Je maslahi yake na kahama ni nini???ikifika kipindi cha uchaguzi wna karagwe tunafanya nini???ni aibu tupu!!!amechaguliwa brandes je kasaidia nini, kama sio kuchakachua matokeo ya uchaguzi na wananchi mkapigwa fimbo???Tubadili viongozi kwanza na tuache dhana ya eti aliyenipa nikala basi ndiye nitampa kura.kuna jamaa zangu nkwenda ambao niliwauliza swali ili wao walidiliki kusema ni kheri wafe na mbuge katagira kuliko kumtosa.je amewasaidia nini kipindi hiki cha kahawa????ndiye mnunuzi mkuu wa kahawa basi.Je chama cha ushirika bado kinatoa pesa ya kuendesha shule za sekondari???miaka ya 80-90 mkulima alikatwa pesa ili watoto wasome sekondari..karaseco,rwambaizi,bushangaro na nyaishozi seco, je ili linafanyika???kama mbunge ananunua kahawa je anachangia kwenye mifuko ya sekondari hizi???anachangia kiasi gani???sekondari za kidato cha 4-6 zipo ni karaseco na kaisho seco, hapa ni pesa yako tu.chondechonde wana karagwe, mimi nimesoma karagwe sekondari,nimekuwa nafuatilia yanayoendelea karagwe.ninasikitika ikifika wakti wa kuchagua viongozi mnachagua makapi. Dhambi hii itawahukumu nyie na vizazi vyenu vijavyo.
   
Loading...