Kapuya ajisalimisha polisi

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
Kapuya alijisalimisha jana kwa siri makao makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kubaka na kutishia kumuua mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.

Tangu kuripotiwa kwa tukio hilo Novemba 13, mwaka huu, Kapuya hajawahi kukamatwa na polisi, huku akitumia wakili wake, Yasini Memba, kutoa matamko na kukanusha kutoa vitisho kwa binti huyo kupitia simu yake ya mkononi 0784993930 ambayo hata chama chake kimekiri kuwa anaimiliki.

Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Kamishna Isaya Mungulu, alilithibitishia Tanzania Daima jana kuwa Kapuya alijisalimisha mwenyewe Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kitengo cha Upelelezi na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.

"Kapuya alijisalimisha leo Makao Makuu Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai; amefanyiwa mahojiano ila yuko nje kwa dhamana.

"Taratibu za dhamana zinajulikana; anaweza kujidhamini yeye au kudhaminiwa, ila nieleweke hivyo," alisema Mungulu.

Kamishna Mungulu aliongeza kuwa kwa sasa hawezi kueleza nini kinafuata, kwani hawajamaliza upelelezi.

"Tukimaliza upelelezi na ushahidi ukajitosheleza, tunapeleka kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) ndiye atakayeamua apelekwe mahakamani au la," alisema.

Kapuya ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne, alifunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam tangu Novemba 24 mwaka huu.

Jalada hilo lilifunguliwa na mwanafunzi huyo anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa, lakini Jeshi la Polisi limekuwa likishughulikia suala hilo katika namna ya kumlinda mtuhumiwa.

Siku moja baada ya jalada hilo kufunguliwa, Kapuya alidaiwa kutimkia nchini Sweden, lakini taarifa za uhakika zinasema alirejea nchini Alhamisi na amekuwa akiishi kwa kujificha huku polisi wakidai kuendelea kumsaka.

Ni katika danadana hizo, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa suala hilo ni jinai na linapaswa liende katika mkondo wa kisheria.

Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alikiri kulifahamu jambo hilo akisema walipomsikiliza mtoto huyo waliona ni suala ambalo linahitaji kushughulikiwa kisheria kwa kuwa ni jinai.

"Suala la binti huyo lilifikishwa kwangu kupitia msaidizi wangu ambaye alisikiliza hoja na rai yake na kushauriwa kuwa hilo ni suala la jinai na linapaswa liende katika mkondo huo.

"Hata hivyo, binti huyo alitambulishwa kwa spika kama kiongozi wa wabunge na kuelekeza kuwa tumshauri alifikishe katika mamlaka husika," alisema Dk. Kashililah.

Kabla ya kujisalimisha polisi, Kapuya amekuwa akimpigia simu binti huyo akiomba wayamalize.

Akitumia namba ileile 0784993039 ambayo awali aliikana, Kapuya alimwandikia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) mwanafunzi huyo akimuomba wakutane ofisini kwa DPP na aseme kuwa hana haja na kesi.

Ujumbe unaodaiwa kutumwa ulisomeka hivi: "Ukienda kwa DPP mwambie kuwa hutaki kesi, mimi niitwe, usipokubali nitakuua, yaani siku si nyingi, na hakuna wa kunifanya lolote, umeshasikia vifo vingapi? Unataka kufa wakati huu au kwa ahadi ya Mungu?"

Polisi lawamani kuvujisha siri

Suala hilo likiwa katika hatua za awali, chanzo chetu cha habari kimesema Kapuya alimpigia simu binti huyo na kumwambia anajisumbua, kwani maelezo yote aliyotoa polisi yenye kurasa 16 na kuongezewa baadaye kuwa kurasa 20 anayo na hatafanywa kitu.

Kutokana na hali hiyo, mtoto huyo na dada yake ambao sasa wanaishi kwa hofu, walimwambia mtoa taarifa wetu kuwa Jeshi la Polisi limempatia maelezo yote Kapuya ambaye wao wanamlalamikia, hali ambayo inawaongezea shaka katika upatikanaji wa haki katika tuhuma hizo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Kamishna Mungulu alisema ni rahisi kwa mtuhumiwa kujua kilichompeleka polisi kama tuhuma zikiulizwa kwa mtiririko.

"Unajua mtu anaweza kujua kwa sababu tuhuma zinazoletwa polisi ndizo hizo hizo hutumika kumuuliza maswali mshtakiwa; polisi hawawezi kumpa maelezo ya walalamikaji, lakini kutokana na mtiririko huo anaweza kubaini," alisema Mungulu.

Source: Tanzania Daima
 
HATIMAYE Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) amejisalimisha polisi.
Kapuya alijisalimisha jana kwa siri makao makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kubaka na kutishia kumuua mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Tangu kuripotiwa kwa tukio hilo Novemba 13, mwaka huu, Kapuya hajawahi kukamatwa na polisi, huku akitumia wakili wake, Yasini Memba, kutoa matamko na kukanusha kutoa vitisho kwa binti huyo kupitia simu yake ya mkononi 0784993930 ambayo hata chama chake kimekiri kuwa anaimiliki.
Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Kamishna Isaya Mungulu, alilithibitishia Tanzania Daima jana kuwa Kapuya alijisalimisha mwenyewe Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kitengo cha Upelelezi na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.
“Kapuya alijisalimisha leo Makao Makuu Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai; amefanyiwa mahojiano ila yuko nje kwa dhamana.
“Taratibu za dhamana zinajulikana; anaweza kujidhamini yeye au kudhaminiwa, ila nieleweke hivyo,” alisema Mungulu.

zaidi bofya
Tanzania Daima – Kapuya ajisalimisha

Hiyo single ya Kapuya imeshachuja! Chadema ni saccos inaendeshwa kilaghai!
 
Hivi kesi ya kubaka, kuambukiza UKIMWI kwa makusudi na kutishia kuua, dhamana yake inatolewaje kirahisi rahisi hivyo...
Wanataka kusema, "Asiye mzinzi kati yao, awe wa kwanza kumpiga Kapuya jiwe!" Karibu wote wanaohusika na kesi hiyo wana ukimwi. Mwisho wa siku Kapuya atakuwa hana kesi ya kujibu!
 
...Wa ccm wanabaka watoto wetu wanapewa dhamana makao makuu polisi!duu!!ingekuwa cdm wangehojiwa siku 3 dhamana mahakamani!!hata iweje tunamtaka mahakamani!na jimbo aachie mbakaji hatufai!hata kama serikali yake!
 
Mnaona mambo hayo, wapi mtoto wa malecela? Pamoja na kufanya uhalifu huo anajiwekea dhamana! Ccm imetufikisha pabaya!
 
Hiyo single ya Kapuya imeshachuja! Chadema ni saccos inaendeshwa kilaghai!

Ni utoto tu,ukikua utawezaa kutofautisha pumba na mchele.Lakini pia ukikua utapata mtoto na hapo ndipo utaelewa yalomsibu huyo binti
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom