Kapuya, Ajira zilizoongezeka ni za mabamedi au wasomi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kapuya, Ajira zilizoongezeka ni za mabamedi au wasomi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 29, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,540
  Trophy Points: 280
  Date::1/29/2009
  Kapuya: Ajira zilizoongezeka ni za mabamedi au wasomi?
  Lauden Mwambona
  Mwananchi​

  HIVI karibuni, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, alikutana na waandishi wa habari na pamoja na mambo mengine, alitangaza kwamba zaidi ya watu milioni moja wamepata ajira nchini tangu mwaka 2005.

  Waziri huyo alisema katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali ya CCM imevuka lengo la ajira milioni moja ilizoahidi kwa Watanzania kupitia Ilani yake ya uchaguzi ya 2005-2010.

  Profesa Kapuya alitoa tambo hizo alipokuwa akielezea mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka mitatu hadi sasa.

  "Tangu 2005 hadi 2008, watu 1,271,923 walipata ajira serikalini na kutoka sekta mbalimbali," alisema na kusisitiza kwamba hayo ni mafanikio makubwa. Lakini asilimia 97 ya waajiriwa hao wapya walipata kazi kwenye sekta binafsi.

  Alifafanua kwamba sekta binafsi iliajiri watu 1,233,747 kati ya 1,271,923 walioajiriwa kipindi hicho. Bila shaka wengi wanatambua kwamba sekta isiyo rasmi ina nafasi kubwa mno katika ajira.

  Bila shaka ajira ya sekta binafsi iliyompa ujiko Profesa Kapuya ni ya walioajiriwa kwenye eneo la vileo ambalo kwa hakika pamoja na imani yangu ya kidini, nalipongeza kwa kusababisha kuwepo kwa wafanyakazi wengi wa baa na grocery ambao sasa wameingizwa kwenye takwimu za kitaifa.

  Sekta hiyo ilitoa ajira katika nyadhifa za wahudumu wa baa au baamedi kama wanavyofahamika, wakati wengine ni wafanyakazi wa majumbani ambao hata yeye si ajabu anao na wafyeka majani ya ng'ombe pamoja na walinzi.

  Lakini pia naamini kwamba Waziri alipata takwimu nyingine nyingi za waajiriwa kutoka kwenye kampuni za simu baada ya kuwaorodhesha watu mbalimbali wanaouza vocha na 'line' katika mitaa mbalimbali nchini.

  Pongezi nyingine ziende kwa kampuni zote za simu kwa kuwatuliza mioyo baadhi ya vijana ambao wamekubali kukaa kwenye jua ili kuwakusanyia fedha kwa njia ya kuuza vocha na line kwa ujira mdogo.

  Waziri Kapuya akiwa na furaha, aliwaambia waandishi wa habari kwamba lengo la kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania milioni moja limetimia kabla ya mwaka 2010 ambao uchaguzi mkuu wa kujieleza mengi utafanyika.

  Lakini wakati akisema hayo, serikali katika kipindi hicho hicho cha miaka mitatu iliyopita iliajiri watu karibu 90 tu. Kwa takwimu halisi za watu waliopata ajira zilizotolewa na Profesa Kapuya kati ya 2005 na 2008 serikalini ni watu 85,571 tu.

  Kapuya ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema waajiriwa hao ni sawa na asilimia 6.7 ya watu wote waliotangazwa kupata ajira kipindi hicho.

  Jamani, serikali kwa kipindi cha miaka mitatu imewaajiri wateule wake 90 tu?, imekuwaje? Kuna nini? Hayo ni baadhi ya maswali ya watu waliosikia taarifa za ajira ya serikali.

  Kwa nini serikali inaajiri watu wachache hivyo wakati ina upungufu wa walimu wa sekondari na shule za msingi? Aliuliza mkazi wa Tabata Bima aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Swaja.

  Je, upungufu wa wauguzi katika Hospitali za Mikoa ya Lindi, Mwanza, Mara, Kigoma na Amana utamalizwa vipi? Alihoji daktari mmoja wa hospitali ya Amana ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

  Kama serikali inaajiri watu 90 je, wasomi wake wa kilimo, watalaamu wa maji wamekwenda wapi? ni swali kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam.

  Maswali hayo na mengine mengi yanatolewa kutokana na ukweli kwamba, pamoja na serikali kuweka mazingira safi ya ajira nchini, nayo inawajibika kuwa na wataalamu wa kutosha kwenye ofisi zake.

  Ni aibu na fedheha, kusikia hospitali ya serikali au shule zake zinakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi. Taarifa za takwimu za wafanyakazi nchini zinaonyesha kuwa wizara na idara za serikali kuu zinakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi jambo ambalo pia linazigusa halmashauri nchini.

  Watu wanajiuliza, kwa miaka mitatu iliyopita ni madaktari wangapi, wauguzi wangapi, walimu wangapi, wahasibu wangapi au wanavyuo vikuu wangapi waliomaliza masomo nchini na kupata ajira alizozitangaza Profesa Kapuya?

  Je, ni busara kutangaza ajira za wafanyakazi wa baa pekee kwenye vyombo vya habari, wakati watalaamu wameachwa mitaani? Bila shaka wizara, imefanya mengi mazuri lakini suala la ajira hata kama ni la kisiasa lingesubiri kutangazwa muda mwingine.

  Wengi wanasema siyo busara kutangaza mafanikio ya ajira, wakati nyumba nne kati ya 10 hapa nchini zinadaiwa kuwa na vijana waliomaliza shule au vyuo wasio na kazi.

  "Profesa Kapuya angetangaza mafanikio ya wizara yake kama vile ya kukamilisha miongozo na kanuni za Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, angetangaza kupungua au kuongezeka kwa migogoro kazini, angetangaza madai ya wafanyakazi kuongezewa mishahara yalifikia wapi," alisema Juma Khamis wa Ubungo Kibangu.

  Hata hivyo, kwa upande wa migogoro, Profesa Kapuya alisema wizara yake ilipokea migogoro 9,624, na kuitatua 8,345 kati ya hiyo sawa na asilimia 86.7. Hayo ni mafanikio ya kutangaza ingawa hakuitaja.

   
 2. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Hapa kuna siasa zaidi kuliko fact, ili kujua iwapo kumekuwa na ongezeko la ajira inatakiwa kuzijua nafasi za ajira ambazo zinajitokeza automatically, mathalani kwa mfanyakazi aliyekuwepo kufa, kustaafu, kufukuzwa kazi, n.k. hizi huwezi kuziweka katika kundi la ongezeko la ajira. Wizara inatakiwa itueleze ajira mpya zilizozalishwa. Kwa mfano, kwa muda mrefu Halmashauri nyingi za wilaya/Manispaa zina upungufu mkubwa sana wa watumishi (kwenye Idara za Afya, Elimu, Ukaguzi wa Ndani, Uhasibu na hata sheria ambako huhitajika mtumishi mmoja tu) kwa sababu mbalimbali. Sasa pale Halmashauri inapotokea kufanikiwa kuajiri watumishi hatuwezi kusema kwamba ajira imeongezeka. Labda kwa halmashauri mpya zilizoanzishwa hilo linaweza kukubalika.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...