Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Huyu E. Kezihalabi ni nani?

Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.

1967 alijiandiskisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).

1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu "African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation". Sasa (mwaka 2012) ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.

Uandishi wake fikirishi uliowahi mletea shida sana kisiasa

kwa wale wenzangu ambao wamekuwa na utamaduni wa kujisomea bila shaka napotaja jina la Euprase Kezihalabi si geni masikioni mwao. Ukiacha ambao walisoma vitabu vyake wakiwa shule kwenye fasihi. binasfi nilianza kusoma vitabu vyake nikiwa nyumbani nikisoma kama burudani kabla ya kuja kufaham baadaye kile kilichokuwa kimeandikwa na athari zake. Nilisoma vitabu kama Rosa Mistika, Kichwa maji ,Dunia Uwanja wa Fujo,Gamba la Nyoka na Kaptula la Marx.

Vitabu hivi vitatu vilikuwa na ukakasi mwingi sana kufikia hatua viwili kati yake kufungiwa au kuzuiwa kuuzwa. Rosa Mistika na Kaptula la Max.

Nilisoma zamani sana Kichwa Maji...nimesahau kiasi maudhui yake lakini ni moja ya vitabu ambavyo naamini watanzania tunapopata muda wa kusoma tunapaswa kuvisoma na kuilewa fasihi ni nini.

Huwa unasoma vibonzo vya Masudi Kipanya? Ile ni fasihi kama ambavyo ungesoma kitabu ukakielewa kilichozungumzwa.

Kaptula la Marx

Ni kejeli kali kuhusu siasa ya Tanzania hasa ya Ujamaa na rais wa wakati ule Julius Nyerere.

Kutokana na ukali wa ukosoaji wake, tamthiliya haikuchapishwa hadi mwaka 1999 ingawa ilifanyiwa uigizaji wa kwanza Septemba 1988 huko Bagamoyo kwenye Tamasha la 7 la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.

Tamthiliya ina sehemu 6 ambako mchezo hubadilisha mahali pake kati ya gereza lenye wafungwa 6 pamoja na kiongozi wao "Mwangaza Africanus" na serikali ya nchi isiyotajwa jina chini ya Rais anayeitwa Kapera.

Chanzo ni jaribio la wafungwa gerezani kukusanya habari nyingi za "dunia ya nje" iwezekanavyo kwa kuiangalia kupitia shimo dogo ukutani.

Wakati huohuo raisi anayeitwa Kapera baada ya kusoma Max anaamua kubadilisha siasa yake kwa manufaa ya watu wengi. Kwa kusudi hii anaamua kuvaa "Kaptula la Max" na shati ya Mao. Nguo zote mbili ni kubwa mno kwake. Mawaziri wake wanamwitikia na kuvaa vilevile. Pamoja wanaondoka walipo kutafuta nchi ya usawa.

Katika sehemu ya 4 wanaondoka kuelekea nchi ya usawa na undugu. Njiani wanakutana na jitu anayeitwa "Korchnoi Brown" na kuwapa maelekezo. Lakini wanashindwa kufika kwa sababu mawaziri hawafai.

Wafungwa gerezani wakati huohuo wanafanya maigizo kati yao wakijadili siasa ya nchi. Mwangaza Africanus anasoma ujumbe kwa viongozi wa Afrika anapokataa siasa zao.

Mawaziri wanaonyeshwa baadaye jinsi walivyo kama vipofu na kutumia mateso ya wafungwa kama mbinu.

Katika sehemu ya mwisho wafungwa wanatoka nje na kupindua serikali ya Kapera anayesalitiwa na mawiziri wake. Kicheko cha Korchnoi Brown kinafunga thamthiliya.

Mazingira ya kuandikwa kwa "Kaptula la Marx"

Kezilahabi aliandika "Kaputula la Marx" mara baada ya maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 5 Machi 1978 na azimio la rais Nyerere kuwafukuza wote chuoni na kupioga marifuku umoja wao DUSO.

Kezilahabi aliyekubali hoja za wanafunzi alishtuka sana kutokana na matendo ya viongozi wa chuo na siasa waliokataa kuwasikiliza. Tamthiliya iliandikwa haraka na kusambazwa kwa kopi lakini haikufanyiwa uigizaji wakati ule. Hata hivyo ilisomwa na watu wengi waliipenda. Kampuni ya Tanzania Publishing House ilitaka kuchapisha tamthiliya lakini iliambiwa na serikali kutoendelea.

Nukuu:

Maelezo ya jitu Korchnoi Brown kwa Rais Kapera na mawaziri waku kuhusu njia ya kufikia nchi ya usawa:

“Mtakwenda! Halafu mtapinda, mtapinda tena, halafu tena mtapinda, mwishowe mtapindapinda hadi mtakapofika mabonde yenye matope. Mtapita katikati ya matope. Halafu milima, halafu misitu yenye miiba hadi mtakapofika jangwani. Kutoka jangwani mtaingia tena bondeni chini kwa chini hadi baharini. Hakuna mitumbwi wala ngalawa. Mtaogelea, ingawa kuna papa wengi. Mkishavuka mtafika nchi iitwayo Svoboda. Kabla ya kuondoka katika nchi hii itawabidi kupambana na majitu yanayofanana na mimi. Mkitoka hapo mtafika kwenye njia nyembamba. (Akiwaonyesha mawaziri) Hawa hawatapita hawa! Njia hiyo itawafikisha katika nchi iitwayo Fraternite. Kutoka Fraternite mtafika Usawa. Ulizeni tu watu watawaonyesha! Mkifika Usawa mtawakuta Waswahili wenzenu wameketi nje ya ikulu ndogo ya Ravensto” (Kaptula la Marx uk. 20)"
jaribu kusoma kitabu hiki na kingine uongeze mbolea katika ubongo wako

Kwa hisani ya wikipedia pia.

Fungua kiambatanisho kujisomea.
Max.jpg
 

Attachments

  • kaptula la Marx.pdf
    23.3 MB · Views: 191
Last edited:
Korchnoi Brown
Kwa maelezo haya huyu KB ni kweli bado yupo na anasumbua na maelezo yake sumbufu kwa njia tuitayo kupotosha maadili na ustawi wetu....! Ila kwa sasa hatutafuata maelezo yake sumbufu...tutatafuta 'shoti kati'...! Ingawa njia tutakayopita itakuwa na vikwazo kadhaa na vinavyovumilika...lakini itakuwa fupi na tutafika haraka. Tukifika huko huyo KB tutam'tag' kwenye mtandao wetu ajionee mapicha na mavideo kedekede ya ustawi wa nchi yetu. Asubiri aone.
 
Fasihi ni njia pekee iwezayo kutumika kuikosoa serikali na jamii yake kwa uhuru zaidi. Bahati mbaya sana jamii yetu sasa imekosa kabisa wasanii wa maana!
Hata kama wangekuwepo (naamini wapo) vitabu vyao tungevisoma? Sasa waandishi wengi wa fasihi pevu wanatoka Kenya ambako usomaji wa vitabu angalau una unafuu. Hakuna kitu kinachomkatisha tamaa mwandishi kama kuandika kazi ya sanaa halafu isiwe na wasomaji. Tanzania hapa ni mpaka ubahatishe kitabu chako kiingizwe katika mitaala ya shule japo napo nasikia ni mpaka upite njia za mkato na uwe na watu wa kukupigania. Taifa lisilosoma. Taifa lisilojielewa. Taifa lisilo na fikra mpya. Na sasa tumepuuzia masomo ya sanaa na tunataka kila mtoto asome sayansi. Tutakuwa taifa la kwanza hapa duniani kuwa na wanasayansi pekee wakiongoza kila nyanja.
 
SHIMBA YA BUYENZE, Tatizo umagharibi umetuharibu sana. Kwa asili yetu waafrika sanaa ni mali ya jamii nzima, hivyo msanii aliona fahari kuona kazi yake ikielimisha au kuburudisha jamii yake tofauti na sasa ambapo wasanii wanawaza pesa tu.

Naamini wasanii kama watafanya kazi nzuri, jamii itahamasika kupenda kusoma/kusikiliza au kutazama kazi za sanaa kuliko kuacha kabisa kutumia vipaji vyao.

Hivi kwa zama hizi ambazo kumkosoa mh.rais ni kosa la jinai akiibuka mwanafasihi akaweza kutumia kalamu yake vizuri kama walivyokuwa wakifanya akina Kezilahabhi, Chinua Achebe, Ngugi wa Thiongo n.k atakosa wateja?
 
Hicho Kitabu cha 'Kaptula la Marx' sijawahi kukisoma lkn nilipoisikia title yake kwa Mara ya kwanza nikahisi ni kitabu ambacho kinajaribu kuwakosoa viongizi wa kiafrika kwa kuukumbatia ujamaa na kujifanya ni wajamaa wakati kila kitu wanategemea kukipata kutoka kwa wabepari...mwishoni ni lazma huo ujamaa ufe!
 
Yawezekana una softcopy yake!?..
chige Red Giant Malcom Lumumba zitto junior Da'Vinci' hearly kuna fasihi bora kabisa imeletwa huku.
Mkuu zamani wabongo walikuwa wanaandika Fasihi bora sana. Sikuhizi ukikuta riwaya zinazouzwa hazivutii hata kusoma na macover yao ya marangirangi.
Nilibahatika kusoma Dunia uwanja wa fujo.Hicho Kaptula la Marx sijawahi soma. Ni wakati wa serikali na Baraza linalohusika wafungulie vitabu walivyofungia. Kuna kile shamba la wanyama/ Animal farm na kile the dark side of Nyerere. Hakuna haja ya kuendelea kuvifungia. Kuna kitabu kimoja cha zamani kinaitwa Bosi, umewahi kisoma?
 
68 Reactions
Reply
Back
Top Bottom