Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Nyie mnayatambua haya sababu macho yenu yanaona. SOCRATES aliwahi kuwa anatembea na TAA kubwa mchana wa jua kali.lets say saa sita. Watu wakamwona kuwa ni chizi. But aligundua wengi hawaoni ingawa wana macho. Akaamua kuwamulikia bado hawakuona

Hahaaaaa ukisoma vizuri kazi za kifasihi kwa jicho la kifasihi unafaidi mmbo mengi matamu sana yasio fahamika kwa wanaosoma kazi hizi kama magaazeti na kupita, kazi kama vile Kufikirika, Kusadikika, unaposoma kazi kadha wa kadha na kukutana na wahusika kama Bi Kirembwe, Mtolewa, Bawabu 1&2 unaweza chukulia poa but kuna mambo mazito sana yanayozungumziwa, Umewahijiuliza mhusika Bi Kirembwe ana fananishwa na nanani? Ahsate muheshimiwa
 
Bila shaka nawe umesoma wakati elimu ilipokuwa elimu.

View attachment 863547
nyongeza katika hayo
"Korchnoi" ni jina la Kirusi, "Brown" ya

Bila shaka nawe umesoma miaka ile wakati elimu ilipokuwa elimu.
Kiingereza; hii inarejea njia ya Tanzania ya Nyerere kati ya "mashariki" ya kikomunisti na "magharibi" ya kibeberu
Svoboda: neno la Kirusi la kumaanisha "uhuru"; jina la nchi larejea wito wa mapinduzi ya Kifaransa -taz. chini-
Fraternite: neno la Kifaransa la kumaanisha "undugu" - ni moja ya wito 3 za mapinduzi ya Kifaransa "liberte, egalite, fraternite" (uhuru, usawa, undugu)
 
Hakijaharibika kitu.bado una damu ya kizazi kinachopenda kusoma. Hongera sana
hapana boss nimeidokoa huko wikipedia baada ya kuusoma huu uzi...japo nami nimwesoma zama za vitabu visivyo na rangi wala picha......
 
30576
Nakipata vipi hiki ?
 
Tatizo hivi vitabu sijawahi ona Soft copy zake kitu kinachoongeza kutokupatina.
 
Kuna Wakati nilisikia kuwa Kezilahabi ni mgonjwa WA akili... Sijui ilikua kweli
Kila kitu kina ukomo wa kukitumia...ukizidisha tatizo..! HUYU MZEE WETU NAKIRI ALITUMIA AKILI ZAKE KUPITA MAELEZO ...halafu pana watu WAKAMKATILI...pengine kweli ZIKAPATA UGONJWA
 
Kaptula la Marx ni tamthiliya iliyoandikwa na Prof. E. Kezilahabi kuelezea hali za siasa katika muda wake.

Aliona kiongozi wa muda wake (Kwenye tamthiliya alimuita Rais Kapela) kuwa kaptula la Marx linampwaya kabisa.

Uongozi wa wafia kaptula la Marx bado upo, lakini hivi sasa nawaona wanaendelea kulitukuza kaptula la marx, japo nawaona kuwa wameivua kabisa.

Naongea na wanafasihi.
 
Kaptula la Marx ni tamthiliya iliyoandikwa na Prof. E. Kezilahabi kuelezea hali za siasa katika muda wake.

Aliona kiongozi wa muda wake (Kwenye tamthiliya alimuita Rais Kapela) kuwa kaptula la Marx linampwaya kabisa.

Uongozi wa wafia kaptula la Marx bado upo, lakini hivi sasa nawaona wanaendelea kulitukuza kaptula la marx, japo nawaona kuwa wameivua kabisa.

Naongea na wanafasihi
Naongea na wanafasihi
Wanafasihi wa leo wamekuwa wachumia tumbo na waimba mapambio ya kusifu na kuabudu... HAWANA JIPYA TENA...!!!!
 
Aliona mbali mwandishi

Mfano leo hii kuna vyama vya upinzani hata haviwezi kujiongoza ati wanataka kuongoza Nchi!! Nchi gani waongoze sasa?
Waendelee kujifariji tu
 
Huyu E. Kezihalabi ni nani?

Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.

1967 alijiandiskisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).

1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu "African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation". Sasa (mwaka 2012) ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.

Uandishi wake fikirishi uliowahi mletea shida sana kisiasa

kwa wale wenzangu ambao wamekuwa na utamaduni wa kujisomea bila shaka napotaja jina la Euprase Kezihalabi si geni masikioni mwao. Ukiacha ambao walisoma vitabu vyake wakiwa shule kwenye fasihi. binasfi nilianza kusoma vitabu vyake nikiwa nyumbani nikisoma kama burudani kabla ya kuja kufaham baadaye kile kilichokuwa kimeandikwa na athari zake. Nilisoma vitabu kama Rosa Mistika, Kichwa maji ,Dunia Uwanja wa Fujo,Gamba la Nyoka na Kaptula la Marx.

Vitabu hivi vitatu vilikuwa na ukakasi mwingi sana kufikia hatua viwili kati yake kufungiwa au kuzuiwa kuuzwa. Rosa Mistika na Kaptula la Max.

Nilisoma zamani sana Kichwa Maji...nimesahau kiasi maudhui yake lakini ni moja ya vitabu ambavyo naamini watanzania tunapopata muda wa kusoma tunapaswa kuvisoma na kuilewa fasihi ni nini.

Huwa unasoma vibonzo vya Masudi Kipanya? Ile ni fasihi kama ambavyo ungesoma kitabu ukakielewa kilichozungumzwa.

Kaptula la Marx

Ni kejeli kali kuhusu siasa ya Tanzania hasa ya Ujamaa na rais wa wakati ule Julius Nyerere.

Kutokana na ukali wa ukosoaji wake, tamthiliya haikuchapishwa hadi mwaka 1999 ingawa ilifanyiwa uigizaji wa kwanza Septemba 1988 huko Bagamoyo kwenye Tamasha la 7 la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.

Tamthiliya ina sehemu 6 ambako mchezo hubadilisha mahali pake kati ya gereza lenye wafungwa 6 pamoja na kiongozi wao "Mwangaza Africanus" na serikali ya nchi isiyotajwa jina chini ya Rais anayeitwa Kapera.

Chanzo ni jaribio la wafungwa gerezani kukusanya habari nyingi za "dunia ya nje" iwezekanavyo kwa kuiangalia kupitia shimo dogo ukutani.

Wakati huohuo raisi anayeitwa Kapera baada ya kusoma Max anaamua kubadilisha siasa yake kwa manufaa ya watu wengi. Kwa kusudi hii anaamua kuvaa "Kaptula la Max" na shati ya Mao. Nguo zote mbili ni kubwa mno kwake. Mawaziri wake wanamwitikia na kuvaa vilevile. Pamoja wanaondoka walipo kutafuta nchi ya usawa.

Katika sehemu ya 4 wanaondoka kuelekea nchi ya usawa na undugu. Njiani wanakutana na jitu anayeitwa "Korchnoi Brown" na kuwapa maelekezo. Lakini wanashindwa kufika kwa sababu mawaziri hawafai.

Wafungwa gerezani wakati huohuo wanafanya maigizo kati yao wakijadili siasa ya nchi. Mwangaza Africanus anasoma ujumbe kwa viongozi wa Afrika anapokataa siasa zao.

Mawaziri wanaonyeshwa baadaye jinsi walivyo kama vipofu na kutumia mateso ya wafungwa kama mbinu.

Katika sehemu ya mwisho wafungwa wanatoka nje na kupindua serikali ya Kapera anayesalitiwa na mawiziri wake. Kicheko cha Korchnoi Brown kinafunga thamthiliya.

Mazingira ya kuandikwa kwa "Kaptula la Marx"

Kezilahabi aliandika "Kaputula la Marx" mara baada ya maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 5 Machi 1978 na azimio la rais Nyerere kuwafukuza wote chuoni na kupioga marifuku umoja wao DUSO.

Kezilahabi aliyekubali hoja za wanafunzi alishtuka sana kutokana na matendo ya viongozi wa chuo na siasa waliokataa kuwasikiliza. Tamthiliya iliandikwa haraka na kusambazwa kwa kopi lakini haikufanyiwa uigizaji wakati ule. Hata hivyo ilisomwa na watu wengi waliipenda. Kampuni ya Tanzania Publishing House ilitaka kuchapisha tamthiliya lakini iliambiwa na serikali kutoendelea.

Nukuu:

Maelezo ya jitu Korchnoi Brown kwa Rais Kapera na mawaziri waku kuhusu njia ya kufikia nchi ya usawa:

“Mtakwenda! Halafu mtapinda, mtapinda tena, halafu tena mtapinda, mwishowe mtapindapinda hadi mtakapofika mabonde yenye matope. Mtapita katikati ya matope. Halafu milima, halafu misitu yenye miiba hadi mtakapofika jangwani. Kutoka jangwani mtaingia tena bondeni chini kwa chini hadi baharini. Hakuna mitumbwi wala ngalawa. Mtaogelea, ingawa kuna papa wengi. Mkishavuka mtafika nchi iitwayo Svoboda. Kabla ya kuondoka katika nchi hii itawabidi kupambana na majitu yanayofanana na mimi. Mkitoka hapo mtafika kwenye njia nyembamba. (Akiwaonyesha mawaziri) Hawa hawatapita hawa! Njia hiyo itawafikisha katika nchi iitwayo Fraternite. Kutoka Fraternite mtafika Usawa. Ulizeni tu watu watawaonyesha! Mkifika Usawa mtawakuta Waswahili wenzenu wameketi nje ya ikulu ndogo ya Ravensto” (Kaptula la Marx uk. 20)"
jaribu kusoma kitabu hiki na kingine uongeze mbolea katika ubongo wako

Kwa hisani ya wikipedia pia

Rosa Misitika nakikumbuka kwakuwa kilisikitisha sana sana! Jama alivyoishia na Rosa ambaye hakuwahi hata kumgusa!

Any way, kwawanaosema Mwl alikuwa dikteta warejee jinsi alivyokuwa anawavumilia wakosoaji wake, nakumbuka hata maandishi mengi ya Ndimara Tegambwage pia ylimkosoa Mwl sana tu(Rejea Duka la Kaya) lkn bado kitabu hicho kilitumika hadi mashuleni wakati huo.

Tujilinganishe na awamu hii, waandishi kama Ngurumo hadi wamekimbia nchi, wabunge wanapigwa risasi hadharani kisa tu fikra mbadala!
 
Kwa maelezo haya huyu KB ni kweli bado yupo na anasumbua na maelezo yake sumbufu kwa njia tuitayo kupotosha maadili na ustawi wetu....! Ila kwa sasa hatutafuata maelezo yake sumbufu...tutatafuta 'shoti kati'...! Ingawa njia tutakayopita itakuwa na vikwazo kadhaa na vinavyovumilika...lakini itakuwa fupi na tutafika haraka. Tukifika huko huyo KB tutam'tag' kwenye mtandao wetu ajionee mapicha na mavideo kedekede ya ustawi wa nchi yetu. Asubiri aone.
vipi tukikwea bombadia au itapotea angani
 
vipi tukikwea bombadia au itapotea angani
Kama bombadia itarahisisha matumizi ya njia ya 'shoti kati' tuitumia. Na tukiitumia 'mbombadia', nakuhakikishia hakuna kitakachoipoteza huko angani. We mean it!! Na tusikilizwe na tueleweke hivyo!
 
Back
Top Bottom