Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

shule ipo kwenye kusoma vitabu na kupata mafundisho mbalimbali yale mambo ya kupewa cheti yasikuumize sana kichwa. tunafaham usomi wa mtu kwa namna anavyochangia hoja na kupembua. namna anavyotoa masuluhisho kwenye changamoto... mimi nlishaaacha kuulizia ulizia vyetu n.k kuna watu wasomi wa vyeti lakini hawana mchango wowote kwenye jamii.
Bila kusoma ukajifunza mengi ni ngumu kupambana na changamoto fikirishi
 
ni nini kilitokea kwa nguli huyu wa fasihi? ni jambo la kusikitisha sana.
Kiukweli sifahamu. Nilijaribu kumuuliza akaniambia yeye mwenyewe hajui ni nini kilichompata lakini taarifa aliyoipata katika mtandao wao wa IKS ni kwamba, jamaa amepoteza kumbukumbu na uwezo wa kuongea.
 
shule ipo kwenye kusoma vitabu na kupata mafundisho mbalimbali yale mambo ya kupewa cheti yasikuumize sana kichwa. tunafaham usomi wa mtu kwa namna anavyochangia hoja na kupembua. namna anavyotoa masuluhisho kwenye changamoto... mimi nlishaaacha kuulizia ulizia vyetu n.k kuna watu wasomi wa vyeti lakini hawana mchango wowote kwenye jamii.
Hii ni kweli kabisa. mi mwenyewe sikuhizi nimekuwa siamini mtu kuwa kaelimika kwa kuwa ana Degree au ni profesa mpaka nione jinsi anavyojenga hoja na uelewa wake. wasomi wetu wengi wana upeo mdogo sana sababu ya uvivu wa kujitafutia maarifa.
 
sure kuna watu walikuwa wazuri sana wa kukariri wakafaulu vizuri sana lakini ukija kwenye uhalisia hamna kitu. na unajua sometime wasahishaji walikuwa wanaangalia uwezo wa mtu kuandika kile kile alichofundisha. nyie wengine mkichanganya na mawazo yenu tu tayari mnakosea. so hawa wakariri wazuri huwa wakati flani wana faulu mpaka level ya PHD na kuja kuitwa Dr na hatimaye Prof lakini uwezo wa kupambanua mambo na kujenga hoja hamna. wanaishia kuwa wababe,wakorofi na kutamba kwa kiburi cha elimu. kumbe msomi anaweza kuwa aliishia tu hata darasa la saba au kidato cha nne akajisomea sana na kufanya sana tafakuri na upembuzi yakinifu wa mambo ili kuweza kutoa masuluhisho ya msingi.hawa huwa tunawakosea kuwauliza vyeti vyao wakati tungewapima kwa akili zao na uwezo waliokuwa nao katika uwasilishaji wa mawazo jengefu na kuondoa mawazo kondefu.

Hii ni kweli kabisa. mi mwenyewe sikuhizi nimekuwa siamini mtu kuwa kaelimika kwa kuwa ana Degree au ni profesa mpaka nione jinsi anavyojenga hoja na uelewa wake. wasomi wetu wengi wana upeo mdogo sana sababu ya uvivu wa kujitafutia maarifa.
 
Nilikutana na jamaa mmoja wa UDSM- IKS( Institute of Kiswahili Studies) aliniambia Kezilahabi amepata matatizo ya kwenye ubongo, ubungo wake umefuta kumbukumbu zake zote. Mbaya zaidi amepoteza mpaka uwezo wa kuongea, kwa sasa anafundishwa tena kuunda maneno.
Hii ni kweli mkuu? Alipata stroke ama? Atakuwa mtu mzima sasa. Mungu Amsaidie nguli huyu wa fasihi na Mwanafalsa wa Falsafa ya Kiafrika
 
nashukuru na kufurahi kuona kuwa bado tuna watu wengi wamesalia katika ulimwengu huu wa elimu. nashukuru kuwa bado kuna wajuzi na wataalamu wa lugha,fasihi na siasa katika kila aina ya nyanja toka enzi na enzi... hawajapotea.
Unajua. Kulikuwa na sababu zake kwamba hata katika baadhi ya akademia za kale za Wagriki Sarufi, Mantiki (Logic) na Fasihi kuu yalikuwa masomo ya lazima. Fasihi inasaidia sana katika kukomaza uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa njia mbadala mbalimbali. Pia ni njia nzuri ya kutolea povu hasa kwa tabaka gandamizwa.

Sisi leo kila mtoto tunataka awe mwanasayansi pamoja na ukweli kwamba kuna baadhi ya tasnia (mf. Siasa na uongozi) wanasayansi wengi hawaziwezi kutokana na mfumo wao wa kufikiri (kisayansi).
 
ni kweli fasihi inawezesha sana kufikiri. unajua fasihi ni pana.. inasemekana waisrael moja ya mbinu ya kuwafanya watoto wao wawe smart ni kuwasimulia hadith wakiwa wadogo, na kuwafundisha kupiga piano, kujifunza mashairi n.k hii inachangamsha sana akili na hata wazungu utaona kila usiku before sleepimh wanawasomea watoto wao hadith then ndo mtoto alale. sisi huku akili zetu miaka hii zimefubaa sababu ule utamaduni wa kusimuliana hadith na vitendawili wakati wa kuota moto haupo .. na umesababisha watoto wa kizazi hiki wale waliozaliwa late 80s na kuendelea wasiwe na uwezo mzuri wa kufikiri.

Unajua. Kulikuwa na sababu zake kwamba hata katika baadhi ya akademia za kale za Wagriki Sarufi, Mantiki (Logic) na Fasihi kuu yalikuwa masomo ya lazima. Fasihi inasaidia sana katika kukomaza uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa njia mbadala mbalimbali. Pia ni njia nzuri ya kutolea povu hasa kwa tabaka gandamizwa.

Sisi leo kila mtoto tunataka awe mwanasayansi pamoja na ukweli kwamba kuna baadhi ya tasnia (mf. Siasa na uongozi) wanasayansi wengi hawaziwezi kutokana na mfumo wao wa kufikiri (kisayansi).
 
hawa ni moja ya watu ninaotaman sana kuonana nao.. sana. mimi wanasiasa huwa sioni kama wana chochote ambacho kinaweza nifanya nionane nao.. most of them hawana akili.asilimia 80 ya wanasiasa hawana akili. ila wazee wetu hawa waandishi wa fasihi,watunzi wa mashairi na nyimbo wana akili sana sema jamii yetu haiwatambui pamoja na wanasayansi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi

GuDume. ...
Mzee wetu yuko Unguja, ila nimeshindwa kujua ni eneo gani la Unguja.
 
Hii ni kweli mkuu? Alipata stroke ama? Atakuwa mtu mzima sasa. Mungu Amsaidie nguli huyu wa fasihi na Mwanafalsa wa Falsafa ya Kiafrika
Hahahahha mkuu literature ulipata mswaki au?
Jamaa anamaanisha kuwa yule mzee amekengeuka yale alokuwa anayapondea ndo anayatenda yani kiufupi anakula matapishi yake.
 
Back
Top Bottom